Hizi ni ziara za Rais au ni kampeni za uchaguzi?

Sidhani kama watu wanapinga yeye kufanya kampeni.

Watu wanahoji yeye kufanya kampeni wakati ilisemekana anakwenda mikoa ya kusini kwa ziara ya kiserikali.

Angekwenda kwa ziara ya kuimarisha chama chake wala hakuna ambaye angehoji.
Serikali ni ya CCM
 
Walitumia Bil 300 kubandika mabango nchi nzima! Haikutosha, ndo kwanza wananchi walichoshwa na ugumu wa maisha. Zile hela bora wangewekeza kwa wananchi hawa, leo unaenda kujisifu umeleta maendeleo! Ni maendeleo gani zaidi ya tozo kwa maskini!
 
Kweli kabisa
 
Alafu mwananchi akisimama na kuomba kutoa dukuduku lake Saa 100 anamkemea na kumwambia onana na mbunge wako miye sina muda. Kweli yule alisema mtanikumbuka
 
Acha uswahili. Nimuonee husda Rais?. Mimi siko hivyo. Ninatoa ushauri tu, kwamba ziara za rais zitenganishwe na kampeni basi. Rais anakuja Mtwara kikazi afanye kazi hiyo basi. Sio kuandaa mikutano ya CCM kwa jina la ziara ya Rais
Hii ndiyo mada yenyewe uliyowasilisha, lakini kuna watu hawataki kuielewa hivyo.

Haya yanatokea kwa sababu ya muundo wa hovyo wa kiutawala wa nchi yetu chini ya CCM.
 
Hii ndiyo mada yenyewe uliyowasilisha, lakini kuna watu hawataki kuielewa hivyo.

Haya yanatokea kwa sababu ya muundo wa hovyo wa kiutawala wa nchi yetu chini ya CCM.
Kweli kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…