kwahiyo unataka Rais asizingumze hadharini na kusifiwa na watu waliomchagua? wanaona anachofanya Rais wao..
kama hupendezwi nae na actually yawezekana hupendezwi nae na unaghadhabu nae sana, sasa si ukae nyumbani utulie gubu liendelee kukutafuna ndani kwa ndani.
Rais ni Rais tu awe kanisani, msikitini, kwenye mikutano ya hadhara au kampeni ya chama chake,upinzani kwenye msiba, sherehe yeyote ile yule ni Rais tu.
Na atasifiwa sana tu.
Kwan Mbowe au Lisu hawasifiwi? Kuna watu wasifia hadi watukana juu ya hawa viongozi.
sasa eti ukae mahali halafu uanze kujiuliza eti huyu anafanya ziara au kampeni, sijui anasifiwa sana,
Hiyo inabaki kua nadharia na tafisiri yako binafsi isiyoathiri sheria wala taratibu za nchi.
Na sio mbaya, ni vizuri kua hivyo, mwisho wa siku unaweza kuibua wazo linaloweza kusaidia kuondoa hali unayokumbana nayo na pengine inawakumba na wengine wengi tu.