Kwa ushauri hizi ziara ziwe za kikazi, Rais aondokane na haya makampeni. Afike kwa wananchi aulize shida zao na Kama wahusika wapo wajibu tuhuma zao.
Mkuu 'econonist', kidogo mimi ninakushangaa wewe, pamoja na kuwasilisha mada liyojitosheleza kabisa; kwamba wewe ndio kwanza unaiona hali hii ya Samia kuwa kwenye Kampeni.
Huyu Kampeni zake zilianza mara tu aliposhika kiti cha urais, na hata siku moja hajafanya tofauti na kujiuza achaguliwe kuendelea kwenye nafasi hiyo.
Alipoingia, wewe hukuona alivyokimbilia harakaharaka kujiuza kwa wasanii? Hukuona matukio aliyofanya ili awaweke wasanii wamuuze katika kazi zao?
Wewe unadhani hayo mabango yaliyotapakaa mijini ya "Nani kama mama" yapo huko kufanya kazi gani?
Wakati akijaribu kuwanunua CHADEMA, unadhani aliwapenda sana hao jamaa, huoni sasa anavyowanyanyapaa baada ya kuona kuwa mtego wake haukuwanasa?
Nikubaliane na wewe, hizi tabia za kiongozi kufanya kampeni za kisiasa, na kuacha kuhudumu kwa kufuata ratiba za mipango ya kazi ni kuharibu kazi za wananchi.
Hao washangiliaji, wabunge, mawaziri na viongozi wengine wote wateuliwa wa huyu mtu mmoja, kazi zao wote wanazielekeza katika kumpigia kampeni mtu huyo huyo, ili na wao waendelee kujaza matumbo yao, na siyo kuleta maendeleo kwa wananchi.
Lugha zinakuwa ni za huyu mtu mmoja, kaleta hiki na kile, kajenga shule, kaleta barabara, kaleta maji; mwishowe tutaanza kuambiwa hata kwenda chooni tutakuwa tunamtegemea mtu huyu huyu mmoja.
Na kwa baadhi ya watu wetu wajinga ndani ya nchi hii wanauamini upuuzi wote huu!
Hovyo Kabisa.