Hizi njaa mbaya

Hizi njaa mbaya

Wakuu usije kumuuliza mwanamke umekula ni kosa kubwa.

Nimeuliza umekunywa chai? anataka nimtumie hela ya chai na vocha sijamjibu

Maendeleo hayana chama
Yaani sina haja kabisa ya kusalimia demu wa kibongo mpaka anisalimie yeye mwenyewe na akinisalimia namjibu kwa haraka haraka nasepa zangu. Mtu umezaa na kibaka mwenyewe kwa tamaa zako za kijinga, leo kibaka kafungwa ama kuuliwa unakuja kujitongozesha kwangu ili nikutunzie watoto uliozaa na kibaka. Kwendraaaa kule.
 
Kuna maswali ya kumuuliza mtu unapokuwa unataka kumnyandua!" Sasa Chai na Kunyanduana wapi na wapi?
 
Afadhali umeliona hilo[emoji2]

Mimi siku moja 2020 kabla ya kuingia mahakamani pale Kinondoni nikasema ngoja nipate staftahi kwenye mgahawa mmoja
Wakati naanza kunywa akaja bibi mzee kikongwe kabisa akaniomba jero, nikaona nisimpe hela bali chakula
Basi nikamuita mhudumu amhudumie, bibi akaenda kukaa meza ya mbali na mimi.. Nikamaliza chai yangu nikaelekea kaunta kulipa, nilikuwa na haraka hivyo nikaacha elfu kumi ili wakate na atakachokunywa bibi kisha nitapitia chenchi yangu

Nimemaliza mishe zangu napitia chenchi napewa 1500.. Kuuliza hesabu nikaambiwa mimi nilitumia 1500 na bibi alitumia 7000..!
Kumbe aliagiza roast maini 3000, chapati 2 1000, kisha akachukua take away supu ya ngo'mbe 3000.. Nikaambiwa ndio tabia yake hivyo nilipaswa kuweka wazi ahudumiwe nini.. Mimi ningejulia wapi yote hayo!? Nilikoma!

nimecheka sana, ingekuwa pesa yake angetumia hivyo... binadamu tuna taabu sana
 
Back
Top Bottom