Afadhali umeliona hilo[emoji2]
Mimi siku moja 2020 kabla ya kuingia mahakamani pale Kinondoni nikasema ngoja nipate staftahi kwenye mgahawa mmoja
Wakati naanza kunywa akaja bibi mzee kikongwe kabisa akaniomba jero, nikaona nisimpe hela bali chakula
Basi nikamuita mhudumu amhudumie, bibi akaenda kukaa meza ya mbali na mimi.. Nikamaliza chai yangu nikaelekea kaunta kulipa, nilikuwa na haraka hivyo nikaacha elfu kumi ili wakate na atakachokunywa bibi kisha nitapitia chenchi yangu
Nimemaliza mishe zangu napitia chenchi napewa 1500.. Kuuliza hesabu nikaambiwa mimi nilitumia 1500 na bibi alitumia 7000..!
Kumbe aliagiza roast maini 3000, chapati 2 1000, kisha akachukua take away supu ya ngo'mbe 3000.. Nikaambiwa ndio tabia yake hivyo nilipaswa kuweka wazi ahudumiwe nini.. Mimi ningejulia wapi yote hayo!? Nilikoma!