Hizi njemba(hawa ma-legend) za JF zinatufanya kizazi cha sasa tuonekane tuna upeo mdogo wa kufikiri


Uliowataja ni theluthi au ni idadi ndogo sana ya malegend wa kweli waliomo humu, inawezekana hukubahatika kusoma maandiko yao au bado ulikuwa mdogo au umewasahau

1. Barafu
2. Nguruvi3
3. Mzee Mwanakijiji
4. MtiMkavu
5. NyaniNgabu
6. MsemajiUkweli
7. Habíb Hanga ( The Bold)
8. MTAZAMO
9. Paschal

Hawa ni baadhi ya watu wenye kuanzisha/kucomment vitu sensitive sana, huwa na nawakubali sana michango yao/nyuzi zao

Baadhi yao JF imewamiss sana sana
 
Kadiri unavyosoma Sana ndivyo ubongo wako unavyozidi kutumika na kuwa Bora zaidi.[emoji1752][emoji1545]
 
Utandawazi na mabadiliko ya kimifumo ya kimaisha pamoja kumezalisha kizazi Cha aina mbili Cha vijana......

1) kizazi Cha hovyo
Hiki ni kile kizazi kinachosukumwa na upepo wa matukio ya kijamii na mabadiliko ya kimifumo ya maisha kwenye jamii pasi na kutumia fahamu zao.......wimbi hili huzalisha kundi la vizazi jeuri, wabishi, wasio na adabu na wenye viburi.....wao hufanya kile wanachoona kinafaa nafsini mwao bila kuangalia matokeo ya matendo yao......hawana adabu na heshima hata chembe........ kuishi vyema na vijana hawa ni kukaa nao mbali na kuheshimu maamuzi hasa yakiwa hayana muingiliano na mambo yako..... kujaribu kuwashauri au kuwarekebisha kunaweza kukugharimu heshima yako, utu wako na hata usalama wako.......

2) Vijana wenye weledi
Hili ni kundi la vijana walioupokea utandawazi na mabadiliko ya kimifumo ya kimaisha kwenye jamii katika mlengo chanya na ni wanufaika wa mchakato huo kwani wao kwenye hayo huangalia yanayowafaa na kushikamana nayo kuachana na yasiyowafaa........

Vijana hawa hawaoni uzia kutaka ushauri au muongozo Kwa wale waliowatungulia na hujisikia fahari kufanya hivyo.... daima wako kwenye njia sahihi.......

Matunda yake yanaonekana Kwa ustawi wa maisha yao kwenye jamii kwenye yale waliyoshikamana nayo.........
 
Mfumo dume umekuathiri, bila kwenye orodha hii kumuweka AshaDii basi Uzi wako ni batili.
 
Nliwataja hapo baadhi ya watu kuwa binafsi walinivutia sana humu ndani. Tutoto twa siku hizi tukaanza mwaga mapovu. Mi nashukuru nawe umeyaona hayo. Maana hawachelewi kusema hizo ni IDs zako pia. GuDume MALCOM LUMUMBA Nyani Ngabu , Chief-Mkwawa ni jamaa ninaowakubali sana. Gudume huwa narudia kusoma tena na tena threads zake natamani siku moja nionane naye ni mtu wa namna gani.
 
Umeniheshimisha. 🙏
 
Hakika hao ni malegends ila kila jukwaa humu kuna mwamba mfano;
Jukwaa la uchumi kuna @Ontorio
Jukwaa la MMU kuna rikiboy
Jukwaa la tech kuna CHIEF MKWAWA
Jukwaa la Inteligency kuna @Da'vinci @Rakism Kiranga e.t.c
 

Watoto wa siku hizi wasikuvuruge, mambo Yao hayawaendei vile walivyopanga hivyo lazima wawe Kama unavyowaona.
Alafu hawajahitimu Jando na unyago hivyo kuhimili misukosuko kwao ni shida
 
Watoto wa siku hizi wasikuvuruge, mambo Yao hayawaendei vile walivyopanga hivyo lazima wawe Kama unavyowaona.
Alafu hawajahitimu Jando na unyago hivyo kuhimili misukosuko kwao ni shida
Hapa umezungumza jambo la msingi sana. Kuna haja ya watoto hawa kupelekwa jandoni na unyagoni pia. Umeliona jambo la maana sana. Zamani haikuwa hivi kabisa.
 
Wapo pia kina Mag3. Nguruvi. Britannica. Bagamoyo. Mohamed Said na wengineo.

Nguruvi
Mag3
Britannica

Mzee wangu Mohamed said kidogo sijamuweka Kwa sababu Dini imemuathiri pakubwa. Ni Kama Dadaetu Faizafoxy.

Ila hao watatu ninaweza kukubalia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…