Hizi njemba(hawa ma-legend) za JF zinatufanya kizazi cha sasa tuonekane tuna upeo mdogo wa kufikiri

Hizi njemba(hawa ma-legend) za JF zinatufanya kizazi cha sasa tuonekane tuna upeo mdogo wa kufikiri

Unafiki kufikisha miaka 40 ukabaki timamu wa Akili ni KAZI ndogo?😀😀😀
Angalia Vijana wa sasa miaka 25 tuu mtoto maisha yashamtoa Knockout, kijana kachanganyikiwa, wengine wanataka kujiua, wengine wamejiingiza kwenye ushoga, wengine madawa ya kulevya, n.k.

Miaka 40 alafu mtu bado yupo timamu huyo ni Legend.
Hivi unadhani misalaba aliyonayo Kijana wa Sasa ni kama enzi zetu...

Acha kabisa vijana wa sasa wana mengi vichwani..., hakuna ajira, future yao haijulikani and they are not even pensionable....

Bado guilty conscious wamesomeshwa kwa wazee wao kuuza mali bado wanarudi mtaani kuomba / kumuomba mzee wao....

Na hapo bado gap in classes / vishawishi kuwa vingi leo hata mtu akipewa milioni kadhaa bado hazitoshi zamani ukiwa na pesa zako nyingi (choices za shule ni zilezile) pia education bure kwahio pesa inabaki unaweza kusomesha ndugu zako wote (feel good factor) na bado utakula bata na pesa utasahau kwenye suruali mkeo akifua wala hakusumbui kuomba pesa ya mboga zile tu kwenye mfuko wa nyuma zinatosha....

All in all kizazi hiki kinapitia mitihani ambayo kizazi kilichopita hakikupitia (anyway hata hivyo sio mbaya mababu zetu utumwani walipitia wakati mgumu zaidi) In short we had it easy....
 
Kuna watu wana madini sana sema sio wapenzi wa kuandika nyuzi bali utaona madini yao kwenye comments...

Kuna watu wana madini sana sema kwa kuwa wanaona hakuna hadhira ya kuweza kutafsiri watachowakilisha, huishia kuwa wasomaji tu...
 
Hivi unadhani misalaba aliyonayo Kijana wa Sasa ni kama enzi zetu...

Acha kabisa vijana wa sasa wana mengi vijwani..., hakuna ajira, hakuna future and they are not even pensionable....

Bado guilty conscious wamesomeshwa kwa wazee wao kuuza mali bado wanarudi mtaani kuomba / kumuomba mzee wao....

Na hapo bado gap in classes / vishawishi kuwa vingi leo hata mtu akipewa milioni kadhaa bado hazitoshi zamani ukiwa na pesa zako nyingi (choices za shule ni zilezile) pia education bure kwahio pesa inabaki unaweza kusomesha ndugu zako wote (feel good factor) na bado utakula bata na pesa utasahau kwenye suruali mkeo akifua wala hakusumbui kuomba pesa ya mboga zile tu kwenye mfuko wa nyuma zinatosha....

All in all kizazi hiki kinapitia mitihani ambayo kizazi kilichopita hakikupitia (anyway hata hivyo sio mbaya mababu zetu utumwani walipitia wakati mgumu zaidi) In short we had it easy....
Very true, kizazi hiki kinapitia changamoto nyingo mno, kuanzia malezi (ambayo sisi wazazi wao hatuwapi ipasavyo) kwenda kwenye social interaction (uwepo wa dunia kiganjani), elimu(ambayo manufaa ya moja kwa moja hayaonekani kwa kijana), ajira(ambazo kwa sasa hakuna) na mengine mengi ambayo kiuhalisia wanapitia.

Vijana wa 90' pamoja na kuwa tunaweza kuwaona wapumbavu, wa apitia mengi, na mengine chanzo ni sisi wazee wa 60,70 na 80's tumesababisha.
 
I can argue wao sio wa hovyo na sisi ndio wa hovyo...

Huu ujinga ujinga wanaofanya wewe ulifanya kulingana na mazingira yako..., wewe ulichagua kazi.., wewe kwa kukosa kazi kuna kipindi ulidhani ubabe ndio ujanja yaani kugombana na kugombanishana watu (bullying) wewe huenda ulidhani kuzamia meli ndio ujanja..., Mavazi yote ni recycling....

Wewe wakati uliona ujanja kurudia kuimba nyimbo za wacongo madogo ni creative wanatoa vibao / vionjo vyao (ingawa msingi unaweza kusema uliweka wewe)

In short ukiona unaanza kuwashangaa vijana wa sasa jua kwamba umezeeka (yaani wakati umekupita) na wewe babu zako walikushangaa... Ila all these is repetition (nothing new under the sun)

Unachoweza kusema labda vijana hawana adabu wenyewe wanahoji kuliko wewe na mimi (to me which is an advantage); Kwenye migomo na utukutu it depends kama unaona hio ni pro au cons (naweza kusema ni pro kwamba they are more civilised than we were)
 
Kiranga na cheaf mkwawa

Ni malegend hawa
Unamaanisha Chief au ? yale yale ya mtoa mada
Usipende kuhukumu hizo ni typing errors tu yeyote inaweza kumtokea.

Kukubalika na watu ni pamoja na kuyaona mapungufu yao kuyaelewa na kuyarekebisha smoothly,huwezi kuniambia hapa hukuelewa toka mwanzo content ya uliyem-quote hapo juu.
 
Tatizo, nyakati hizi vijana wanakutana na changamoto nyingi. Na changamoto hizo, kwa asilimia kubwa zinatatuliwa na rasilimali fedha.

Kijana, kupoteza muda kwa kufanya utafiti, na kuweka uzi uliojaa 'nondo' itamlazimu kujiuliza, ananufaika na nini? Kama hanufaiki, ataweka mada nyepesi, ile itakayokuja kichwani kwa muda ule.

Ni sawa na kujiuliza, kwa nini wakufunzi wa vyuo vikuu hawatungi vitabu au kufanya 'publication' zilizoshiba n.k​
 
Tatizo vijana au niseme watoto wetu humu wakiishiwa hoja wanaanza kejeli na matusi

Nyuzi nyingi za maana baada ya kuchangia wanaishia kutukana
Tunajua wengi maisha yamewapiga na wanajiuliza kweli watatoboa?

Wasomi wamo ila wanasubiri waajiriwe na ni mwaka wa kumi anasubiri tu, huyo ukimzingua utakoma
 
muda hubadirika, mifumo ya maisha hubadirika na kila mabadiriko yana faida na hasara zake.

Dunia hii huwezi kuifananisha na dunia ile, mifumo ya dunia hii iko kwenye mikono ya watawala wa dunia ambao huamua nini kifanyike wapi na wapi waishi vipi.

Madhara uyaonayo sasa ni ujinga na uzembe wa zamani, faida uzionazo sasa kwa wengine ni akili kubwa iliyowekezwa zamani na manufaa ya baadaye.

Unapolaumu vijana wa sasa ni vyema pia ukalaumu walezi aka wazee wa zamani ambao ndio wazazi wa vijana hawa.

Tunaposifu vizazi bora vya mataifa makubwa yaliyoendelea hatuna budi kusifia malezi bora na uwekezaji madhubuti wa mababu na mabibi zao.
 
Halafu unaposema sisi kizazi cha miaka ya 90 unamaanisha nini? Kuna watu wamejiunga JF miaka ya karibuni, na bado hawapo kwenye kizazi chenu cha miaka ya 90!

Sema tu nyinyi madogo mnapenda sana kutukana tukana hovyo kila mtu aliye mbele yenu. Halafu mna u much know sana.
Umeandika upupu tu.

Kipi ujaelewa wewe
 
Back
Top Bottom