Hizi nyimbo tumeziimba sana sisi Wanasimba msimu huu

Hizi nyimbo tumeziimba sana sisi Wanasimba msimu huu

CARIFONIA

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2013
Posts
616
Reaction score
1,453
Tangu kuanza kwa msimu huu sisi mashambiki wa simba tulikua na matumaini makubwa sana na timu yetu, na hii ilitokana na ukweli kwamba takribani misimu minne tulikua na timu bora sana na hivyo tulifanikiwa kudominate soka la bongo na hata katika medali za kimataifa tulijaribu kupambana kidogo na sisi tukaonekana tupo, japo kuna mbinu chafu tulizokua tunazitumia kupata matokeo kwa wapinzai wetu hasa pale tulipocheza mechi za nyumbani, lakini tulipoenda ugenini tulikua tukigeuzwa tu kama chapati za mama ntilie.

msimu huu wenzetu wakajipanga wakaingia sokoni wakatoa mpunga wakafanya usajili wa nguvu, uku sisi usajili wetu ukawa tia maji tia maji, kama unavyojua waswahili wanamsemo wao kua kila mtu atavuna alichokipanda.

Ndipo hapo sisi mashabiki wa simba tukaanza kuingia studio na kuanza kufyatua bahadhi ya nyimbo zilizo tufariji sana msimu huu, nakumbuka nyimbo ya kwanza ilikua jamaa wamesjili wacheza mziki kutoka congo, lakini bahada ya kuona kazi ya hao wacheza mziki kutoka congo ndipo tulipo rudi studio nakutoa nyimbo nyingine na hii ilikua bahada ya jamaa kuona wanaongoza ligi ndipo tukaja na wimbo wametangulia tu kwa basikeli ya miti, nyimbo hii ilitufriji sana uku tukisema mbona misimu yote hua wanaanza kwa kuongoza ila mwisho wa ligi mnyama anachukua ndoo, upande wa pili jamaa wakendelea kukaza na wakawa wamedhamiria kutoshuka kileleni, ndipo tukaamua kurudi tena studio na safali hii tukaja na wimbo mwingine maridhawa kwa jina la GSM anatuaribia mpira wetu wimbo huu nao ukatufariji sana kwani licha kuona kile wenzetu wanafanya uwanjani lakini wimbo huu ulifanya tuamini kua ushindi wanoupata ni wa michongo tu na GSM wanatoa fungu kuakikisha jamaa wanakua mabingwa msimu huu.

Kama tunavyojua mfa maji aishi kutapatapa ndipo na sisi tukapata chaka la kujifichia baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya kombe la shirikisho ndipo tulipoanza na tambo za bwana sungura la sizitaki mbichi hizi na maneno mengi ya madharau sisi sio level ya kucheza kombe la mbuzi sis tunawaza zaidi kimataifa na makombe ya mbuzi tumewaachia wenzetu, ndipo bwana mwekiti mstaafu akaamua kuingia studio na kuja na nyimbo nyingine iliyoturudishia matumaini ya kutetea ubingwa wetu jina la nyimbo nimelisahau kdogo ila mistari ndio naikumbuka kidogo kwani kuna bahadhi ya lyrics zilikua zinasema Yanga atafungwa au kusare na KMC, then atafungwa na AZAM then Yanga atafungwa au atasare na Namungo then tutakuja kumaliza kazi sisi wenyewe kwa kumfunga Yanga na kuchukua pointi tatu hivyo tutamshusha kutoka nafasi ya kwanza na kutetea ubingwa wetu.

Kwa sasa naona pumzi imekata kule kwenye kombe la shirikisho maaramia wametuangushia kitu kizito kichwani, uku nako kwenye kombe la mbuzi wale tuliowaita bendi ya mziki walishatuzidi kete hata tukicheza nao atuna uwezo wa kuwafunga labda tu tujitaidi kumzuia bwana Myele asitufunge, kwa sasa ata mzuka wa kwenda studio kutoa nyimboa mpya ndio umekata kabisa, kwa sasa tunajifariji tu na kikombe chetu cha mapinduzi na lile kombe la robo fainali tuliochukua pale bondeni kwa madiba, bila kusahau kua bado tuna mechi ya kimataifa na Pamba ya mwanza.

Dah! ila yule Manara altuweza kweli kumbe sisi ni makolo
 
Pumba tupu! Timu lililogeuzwa asusa nje ndani na Rivers utd leo mnasema ni timu bora. Bangi hizi!
 
Back
Top Bottom