Hizi pesa kwenye akaunti zetu za simu, mtoa huduma anaweza kuzitumia?

Hizi pesa kwenye akaunti zetu za simu, mtoa huduma anaweza kuzitumia?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Salamu wakuu!

Ni huyu mwanangu mkubwa leo kaniuliza swali hilo, ngoja niliweke vizuri ili tuweze kujadili.

Ni hizi akaunti zetu za M-Pesa, TigoPesa, Airtel-Money, HaloPesa, T-Pesa itifaki imezingatiwa.[emoji28]

Tunaweka kuhifadhi na kutuma kwenda kwa watu wengine, au kulipia huduma mbalimbali. Tukihitaji pesa taslimu tunazitoa kupitia mawakala wa hizo kampuni (service providers).

Hoja iko hivi:

Je, kampuni wanayo 'access' na pesa zetu hizi kama ilivyo mabenki?

Kwamba wanaweza kuzitumia mfano katika biashara zao hata kukopesha na kuzizungusha?

Yaani mtu [mteja] anaweza kwenda kuchukua mkopo Vodacom au pale Nyumbani Kumenoga na kuondoka na kitita kama taratibu za kibenki?

Au ni PESA ambazo zipo kwenye 'line' zetu tu!

Sijui kama nimeeleweka ila nadhani nimejitahidi, naomba nijifunze kwenu.

Ncha Kali.
 
Hizi kapuni za simu hazikai na pesa zetu cash kinachofanyika pale ni sawa na mchezo wa namba tu. Ndio maana ukitaka kuchukua au kuweka pesa unaenda kwa wakala. Pia hata kampun za simu nao wakitaka kutoa hiyo pesa wanaenda bank.
 
Kwahiyo hizi tunazotunza M-Pawa sijui, sio Pesa?
Ni takwimu tu za pesa zako ndizo zilizomo kwenye makampuni hayo. Labda tuseme hivi, unapokuwa na kampuni inayohusika na pesa kwa namna fulani hiyo kampuni inaweza pia kuwa kama benki. Kisheria benki inatakiwa iwe na minimum amount of money ambayo muda wote inatakiwa iwe benki, ukihitaji unapata. But kuna mambo mengiiiiii hapa (kama benki na benki kukopeshana ama hata kusaidiana kwa dharura, nk).

So, cha msingi ni kujua kwamba benki ina wajibu wa kuhakikisha kwamba fedha yako ipo muda wote. Ukihitaji unapewa. Kama ni kiasi kikubwa sana, kisheria huwezi kuivuta yote kwa wakati mmoja, maana ili benki iendelee lazima ifanye biashara kwa hizohizo fedha zako. Na faida ya benki ni mzunguko wa hela wanayoikusanya kutoka kwa wateja.
 
Asante kwa maelezo mengi, ila katika yote hayo umejikita kuelezea benki kama benki…. hoja mezani ni PESA kwenye mitandao ya SIMU.
 
Ni ngumu
Pesa za kwenye mobile phone ni e-money sio taslimu kama zile za bank unazodeposit

Unavyokwenda kwa wakala kuweka pesa unaenda kuweka manamba namba kwenye simu yako, yeye unampa cash yeye anakuwekea manamba namba kweny simu so nika kama mna-exchange,

Hivyo zile fedha sio zako na Tigo, Voda, Airtel HQ hawana hela zako cash zaidi ya database tuu ya miamala yako

I will be back, this definement is nkt enough
 
Hizi kapuni za simu azikai na pesa zetu cash kinachofanyika pale ni sawa na mchezo wa namba tu. Ndio maana ukitaka kuchukua au kuweka pesa unaenda kwa wakala. Pia hata kampun za simu nao wakitaka kutoa hiyo pesa wanaenda bank.

Kwenda kwa wakala ni kwa vile huyo ni wakala wa kampuni husika, hata benki zina mawakala wao kwa kazi ile ile.

Una maelezo mazuri ila ni ya kawaida sana, unaweza kufikiria zaidi?
 
Ni ngumu
Pesa za kwenye mobile phone ni e-money sio taslimu kama zile za bank unazodeposit

Unavyokwenda kwa wakala kuweka pesa unaenda kuweka manamba namba kwenye simu yako, yeye unampa cash yeye anakuwekea manamba namba kweny simu so nika kama mna-exchange,

Hivyo zile fedha sio zako na Tigo, Voda, Airtel HQ hawana hela zako cash zaidi ya database tuu ya miamala yako

I will be back, this definement is nkt enough

Speaking of manamba namba tu, hata benki procedure ni zile zile…. unampa keshi anakuwekea namba tu kwenye akaunti yako.

Ukizitaka hela zako, unampa namba namba wakala (simu/benki) anakupa cash…. this knowledge is way too general.

Can you go beyond that?

Nitasubiri ukirudi.
 
Kwenda kwa wakala ni kwa vile huyo ni wakala wa kampuni husika, hata benki zina mawakala wao kwa kazi ile ile.

Una maelezo mazuri ila ni ya kawaida sana, unaweza kufikiria zaidi?
Jibu la msingi nimesema hivi makampun ya simu hayana uwezo wa kutumia pesa ya mteja kwa sababu hayakai na pesa cash za mteja. bali wanakua na kumbukumbu ya kiasi chako cha pesa kwa njia ya namba tu, tofauti na bank ambao wao wanabaki na hela cash. Pia kuna tofauti kati ya wakala wa bank na wakala wa mitandao ya simu hatakama kazi zao zinafanana.

Wakala wa bank akiishiwa cash anaenda bank husika kuchukua pesa. ila wakala wa simu akiishiwa cash haendi kwenye mtandao wake kuchukua pesa ila nae ataenda bank kutoa salio ili apate cash kwa sababu mitandao ya simu haimiliki pesa cash.
 
mkuu kila mtandao wana acc zao benk uko sasa usije ukawaza siku kuvamia pale Hq ya voda/airtel/tigo ukazani utakutana na Cash kweny ofis zao hapana

[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Hujaeleweka, dadavua zaidi…. sheria hairuhusu nini?

Nini tofauti ya TigoPesa na NMB? Jikite kwenye mteja kutunza na kutoa pesa, ukiacha ile kwamba M-Pesa ina kiasi cha ukomo.
BoT wana taratibu zao ambazo taasisi zilizotimiza tu ndizo zinazoruhusiwa kukusanya pesa za wateja na kukaa nazo ( depositing )

Ndio maana hata mitaani kuna taasisi za mikopo ambazo haziruhusiwi kupokea akiba za wateja wao.
 
mkuu kila mtandao wana acc zao benk uko sasa usije ukawaza siku kuvamia pale Hq ya voda/airtel/tigo ukazani utakutana na Cash kweny ofis zao hapana

Sio hivyo bwashee.

Unajua kwenye ofisi zao kuna dirisha la WAKALA MKUU?

Huyu wakala ni kwa ajili ya shughuli za kifedha, na wana matawi kila sehemu (Super Agents).

Je, ni mradi wa kampuni au ni tenda kwa watu binafsi?
 
BoT wana taratibu zao ambazo taasisi zilizotimiza tu ndizo zinazoruhusiwa kukusanya pesa za wateja na kukaa nazo ( depositing )

Ndio maana hata mitaani kuna taasisi za mikopo ambazo haziruhusiwi kupokea akiba za wateja wao.

Mkaruka, kwa mujibu wa maelezo yako…. nini tofauti ya ku-deposit TigoPesa na CRDB?

Swali uliulizwa hivyo.
 
Back
Top Bottom