Hizi pesa kwenye akaunti zetu za simu, mtoa huduma anaweza kuzitumia?

Hapana awawezi kutumia ....

Makampuni ya simu yanafanya kazi na mawakala wakuu ambao ndo wanatoa mitaji, hupeleka bank kiasi wanapewa float sawa kiasi walichokabizi.

Hizo floats huzisambaza kwa mawakala wa mitaani wanotoa huduma na kupokea cash, mawakala huudumia wateja kama ilivyo desturi....

Kwa iyo tutaona kwamba mwenye axcess ya kutumia fedha izo bado ni Benki si makampuni ya simu.
 
Salamu wakuu!

Ni huyu mwanangu mkubwa leo kaniuliza swali hilo, ngoja niliweke vizuri ili tuweze kujadili.

Ni hizi akaunti zetu za M-Pesa, TigoPesa, Airtel-Money, HaloPesa, T-Pesa itifaki imezingatiwa.[emoji28]

Tunaweka kuhifadhi na kutuma kwenda kwa watu wengine, au kulipia huduma mbalimbali. Tukihitaji pesa taslimu tunazitoa kupitia mawakala wa hizo kampuni (service providers).

Hoja iko hivi:

Je, kampuni wanayo 'access' na pesa zetu hizi kama ilivyo mabenki?

Kwamba wanaweza kuzitumia mfano katika biashara zao hata kukopesha na kuzizungusha?

Yaani mtu [mteja] anaweza kwenda kuchukua mkopo Vodacom au pale Nyumbani Kumenoga na kuondoka na kitita kama taratibu za kibenki?

Au ni PESA ambazo zipo kwenye 'line' zetu tu!

Sijui kama nimeeleweka ila nadhani nimejitahidi, naomba nijifunze kwenu.

Ncha Kali.
Zinatumiwa kibiashara, hazikai tu muda wote kwenye akaunt zetu. Ndio maana kila baada ya kipindi fulani kupita wanajifanya kutoa gawio kwa wateja zao (sehemu ya faida waliochuma)Chakushangaza licha yakutumia pesa zetu kibiashara na kujipatia kiasi kikubwa cha faida bado wanatukata pesa zetu wakati sisi ndio tunaowawezesha.
 
Watazitoaje bilq kujua password yako. Kumbuka unapoingiza password kule inaonyesha nyotanyota tu na wala hakuna mfanyakazi wa kampuni anyeweza kujua namba yako ya siri
 
Wanapata Faida kwa njia ya makato wanayokata kila muamala sio kwamba wanatumia hela za wateja.
 
Watazitoaje bilq kujua password yako. Kumbuka unapoingiza password kule inaonyesha nyotanyota tu na wala hakuna mfanyakazi wa kampuni anyeweza kujua namba yako ya siri

Kuhusu password napingana na wewe, ingekuwa hawana 'access' wasingeweza hata kukutajia SALIO lako ukiwapigia.
 
Je, kampuni wanayo 'access' na pesa zetu hizi kama ilivyo mabenki?
Hapana hawana access kama mabenki. Wao wanahifadhi na kurahisisha kutumiana pesa.

Kwamba wanaweza kuzitumia mfano katika biashara zao hata kukopesha na kuzizungusha?
Hawazungushi pesa yako, faida yao wanaipata kwenye makato unapotoa ama kutuma pesa. Na sidhani kama wanaweza kuzungusha pesa ambayo inakaa chini ya lisaa, mfano mtu kakutumia pesa chap na wewe umeenda kuitoa iyo ela itazungushwa vipi!?

Ni tofautu na mabenki ambapo kuna fixed accounts na pia kuna kiasi ambacho mteja hutakiwi kutoa, kuna makato ya kuendesha account na makato makato mengine ambayo yanaiendesha hiyo kampuni(benki) na kufanya hata ukiwapa pesa yako wana uwezo wa kuizungusha kwasababu ukiitaka muda wowote wanayo ya kukupa. Tofauti na izi e-money hizi ni kama papo kwa hapo transactions.
Yaani mtu [mteja] anaweza kwenda kuchukua mkopo Vodacom au pale Nyumbani Kumenoga na kuondoka na kitita kama taratibu za kibenki?
Mikopo wanatoa kwa njia hiyohiyo ya kimtandao mfano m-pawa, timiza, nipige tafu na kama hizo. Nadhani sheria inawaruhusu kufanya ivyo. Hawawezi kukupa kitita mkononi kwasababu wao hawatunzi cash mkuu ndio maana unapewa kwa njia ile ile. Na hata mikopo yao sio mikubwa kama benki.
Nadhani risk ya hiyo mikopo ni kubwa ndio maana hawatoi kiasi kikubwa, na sio sawa kwa wote.

Au ni PESA ambazo zipo kwenye 'line' zetu tu!
Mi nadhani ni hivo mkuu, ni pesa iliyo kwenye laini yako tu. Ni kama vile udeposit pesa m-bet, inakua sio yao mpka pale utapobet ukaliwa. Pale inakua km umeihifadhi tu. So na wao ukituma/ kutoa pesa ukakatwa na wao wanapata chochote
.
 
Salamu wakuu!

Ni huyu mwanangu mkubwa leo kaniuliza swali hilo, ngoja niliweke vizuri ili tuweze kujadili.

Ni hizi akaunti zetu za M-Pesa, TigoPesa, Airtel-Money, HaloPesa, T-Pesa itifaki imezingatiwa.[emoji28]

Tunaweka kuhifadhi na kutuma kwenda kwa watu wengine, au kulipia huduma mbalimbali. Tukihitaji pesa taslimu tunazitoa kupitia mawakala wa hizo kampuni (service providers).

Hoja iko hivi:

Je, kampuni wanayo 'access' na pesa zetu hizi kama ilivyo mabenki?

Kwamba wanaweza kuzitumia mfano katika biashara zao hata kukopesha na kuzizungusha?

Yaani mtu [mteja] anaweza kwenda kuchukua mkopo Vodacom au pale Nyumbani Kumenoga na kuondoka na kitita kama taratibu za kibenki?

Au ni PESA ambazo zipo kwenye 'line' zetu tu!

Sijui kama nimeeleweka ila nadhani nimejitahidi, naomba nijifunze kwenu.

Ncha Kali.

Kwa mtindo wa tarakimu kugezwa pesa ni ndiyo. Ni kwa msingi huo Mpawa kuna mkopo. Ila kiasi kinakuwa kidogo kutokana na risk kuwa kubwa. Ni suala la kufata taratibu na sheria.

Ukitimiza masharti, unaenda kwa wakala kuchukua hela yako kama mwakilishi wa kampuni husika ya simu. Kama unavyokwenda kwenye tawi la benki.
 
Back
Top Bottom