Hizi pesa kwenye akaunti zetu za simu, mtoa huduma anaweza kuzitumia?

Hizi pesa kwenye akaunti zetu za simu, mtoa huduma anaweza kuzitumia?

Sio hivyo bwashee.

Unajua kwenye ofisi zao kuna dirisha la WAKALA MKUU?

Huyu wakala ni kwa ajili ya shughuli za kifedha, na wana matawi kila sehemu (Super Agents).

Je, ni mradi wa kampuni au ni tenda kwa watu binafsi?
Ni mradi wa kapuni katika kujiongezea mapato pia Hilo dirisha linatoa huduma sawa tu na huduma ile anayoitoa wakala wa mtaani.
 
CRDB wanachukua cash wakati Tigo pesa wao hawachukui cash kwasababu hawana leseni ya kukaa na pesa za watu.

Hizo nyingine ni namba tu.

Unatumia lugha ngumu, ni kama unajihami kukwepa swali la huyu mtoto…. hebu fikiria tena tofauti ya hizo unaita cash na namba kwenye DEPOSITS.

Nikienda benki au wakala mimi nawapatia keshi wanapokea, unasemaje huku cash kule namba?
 
Wakipokea wanapeleka bank. Lakini bank hazifanyi hivyo.
 
Ni ngumu
Pesa za kwenye mobile phone ni e-money sio taslimu kama zile za bank unazodeposit

Unavyokwenda kwa wakala kuweka pesa unaenda kuweka manamba namba kwenye simu yako, yeye unampa cash yeye anakuwekea manamba namba kweny simu so nika kama mna-exchange,

Hivyo zile fedha sio zako na Tigo, Voda, Airtel HQ hawana hela zako cash zaidi ya database tuu ya miamala yako

I will be back, this definement is nkt enough
Bahati mbaya umechoka mapema kueleza, lakini wewe ni mwalimu mzuri sana kuelewesha mtu.
 
Salamu wakuu!

Ni huyu mwanangu mkubwa leo kaniuliza swali hilo, ngoja niliweke vizuri ili tuweze kujadili.

Ni hizi akaunti zetu za M-Pesa, TigoPesa, Airtel-Money, HaloPesa, T-Pesa itifaki imezingatiwa.[emoji28]

Tunaweka kuhifadhi na kutuma kwenda kwa watu wengine, au kulipia huduma mbalimbali. Tukihitaji pesa taslimu tunazitoa kupitia mawakala wa hizo kampuni (service providers).

Hoja iko hivi:

Je, kampuni wanayo 'access' na pesa zetu hizi kama ilivyo mabenki?

Kwamba wanaweza kuzitumia mfano katika biashara zao hata kukopesha na kuzizungusha?

Yaani mtu [mteja] anaweza kwenda kuchukua mkopo Vodacom au pale Nyumbani Kumenoga na kuondoka na kitita kama taratibu za kibenki?

Au ni PESA ambazo zipo kwenye 'line' zetu tu!

Sijui kama nimeeleweka ila nadhani nimejitahidi, naomba nijifunze kwenu.

Ncha Kali.
Mabenk yote yamepewa leseni na BOT ya kufanya biashara za kibenk

Na mitandao ya simu nayo pia imepewa leseni na BOT ya kufanya biashara ya mobile money

Tofauti hapo ni leseni tu kila mmoja anafanya kile ambacho leseni yake inamtaka afanye zaidi hapo hakuna tofauti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesoma na kuelewa mada?
 
Mbona muuliza-swali unachosha sana hivyo na wewe!??? Upoje lakini jamani!??? 🙂 🙂 🙂
 
Mbona muuliza-swali unachosha sana hivyo na wewe!??? Upoje lakini jamani!??? 🙂 🙂 🙂

Sio kosa langu, ni hawa watoto wangu wadadisi wa mambo.

Unataka mtoto mwenye akili…. serious!!

Fanya fanya uzae na Ncha Kali…. genius!![emoji6]
 
Mtoa mada hakueleweka, and of course mada yake ni nzito.

The utmost mode of conductivity of bank ni utunzaji wa fedha taslimu kwa kikundi au kijumuia na hio ndio dhima mama ya mabank duniani tangia hapo.

Hicho ndio kitu pekee kinachofanya mtu kukopeshwa na banks, unajua a group cash-money kama bank can be so huge kiasi kwamba kinaweza kutumika katika habar nyingine kwa utaratibu fulani, Mfano unawez pewa mkopo bank bila kuwa na account hapo, ila tu kwa kupitia utaritibu( Dhamana,biashara yako, uwe na Account nk).Suprisengly Unaweza kukopeshwa hata hela zake bakhresa kwakua tu mnashare the same kibubu.

Ni kupitia tu mapinduzi katika information technology ndio kuna mambo kama vile kutumiwa meseji ukideposit au ukiwithdraw hela kwny kibubu cha jumuia/kikundi (banks).

Hata habari za kufanya malipo kwa njia ya bank nayo ni katika mabadiriko ya technolojia hiyo. ila MSINGI MAMA wa banks duniani ni utunzaji wa fedha taslimu kwa pamoja na msingi huo ndio unaokukopesha hela wewe na wengine

Makampuni ya simu wamekuja na mobile e-money service lakini katika Mode of conductivity tofaut na ile ya kibank, Hapa hakuna " a Group Cash-money Management " kama kule bank ila tu kuna " a Group e-money Management "

Tigo pesa and the likes wanasimamia na kuratibu those induvidual e-money accounts, ndio maana tunaweza kurudisha pesa ukipoteza sim card, tunaweza kufungiwa huduma na hao watoa huduma

Na Hapa ndipo swali la bwana nchi kali linakuja, Je Tigo pesa(mtoa huduma) na wenzie wanaweza kuzitumia hizo e-money kuendesha biashara na kutoa mikopo nk as what wazee wa group-cash do ?

Ni kama tunaingia kwenye habari financial market hivi.

Washiriki wengine walivyosema kwamba kisheria Tigo pesa na wenzio hawana/hawajapewa mandate ya kumiliki/kukaa na fedha za raia, Binafsi hili sina uhakika nalo.

I admit, i did a rough response yesterday
So the answer is that, it might be nearly POSSIBLE but through their mode of conductivity (modality).
 
Lets keep aside fahari huduma na Nmb chap chap. Hazina maana sana kujadiliwa with the context of your topic
 
Hujaeleweka, dadavua zaidi…. sheria hairuhusu nini?

Nini tofauti ya TigoPesa na NMB? Jikite kwenye mteja kutunza na kutoa pesa, ukiacha ile kwamba M-Pesa ina kiasi cha ukomo.
Hajikite wapi wewe mkaldayo?
 
Ni ngumu
Pesa za kwenye mobile phone ni e-money sio taslimu kama zile za bank unazodeposit

Unavyokwenda kwa wakala kuweka pesa unaenda kuweka manamba namba kwenye simu yako, yeye unampa cash yeye anakuwekea manamba namba kweny simu so nika kama mna-exchange,

Hivyo zile fedha sio zako na Tigo, Voda, Airtel HQ hawana hela zako cash zaidi ya database tuu ya miamala yako

I will be back, this definement is nkt enough
Kwasisi tusiosoma umetuchanganya,,yaani nitoe hela wao wanipe namba namba?.
 
Kwasisi tusiosoma umetuchanganya,,yaani nitoe hela wao wanipe namba namba?.
Unapokwenda kwa wakala Ukampa elfu kumi taslimu ili akuwekee kwenye account yako je wakala anakuwekea hela cash au namba?.
 
Unapokwenda kwa wakala Ukampa elfu kumi taslimu ili akuwekee kwenye account yako je wakala anakuwekea hela cash au namba?.
Ndo maana nimechonga kibubu,,unaweza ukadhulumika huko,,,wanaweza kukuruka mda wowote..😀😀
 
Back
Top Bottom