Hizi projects zitaifanya Dar kua unbeatable lifetime modern city in East Africa

Hizi projects zitaifanya Dar kua unbeatable lifetime modern city in East Africa

REDEEMER.

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
8,925
Reaction score
14,890
STENDI YA MBEZI LUIS YATENGEWA BILIONI 50, KUANZA KUJENGWA ‘SOON’
May 10, 2018 by Denis Mtima

2-5.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akizungumza jambo.

4-6.jpg

Taswira ya Mwonekano itakavyoonekana katika stendi hiyo ikiwemo pia gorofa za hoteli zitakazojengwa eneo hilo.

3-8.jpg

Mmjoa wa viongozi wa jiji la Dar es Salaam akimwonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda (hayupo pichani) mchoro wa stendi hiyo mpya ya Mbezi-Luis itakavyokuwa.

5-5.jpg

Makonda na viongozi wengine wakiangalia runinga iliyokuwa ukutani ikionyesha ramani ya ujenzi huo.

6-5.jpg

Michoro mbalimbali ya stendi hiyo.



STENDI ya Mabasi yaendayo mikoani Ubungo ambayo inahamishiwa Mbezi-Luis jijini Dar es Salaam tayari imetengewa Shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kuanza ujenzi mwezi ujao, ambapo kituo hicho kitakuwa cha kisasa na chenye huduma mbalimbali za jamii ikiwemo mahoteli.



Makubalino hayo yametolewa na Mkurugenzi Wa jiji lake Spora Liana ambaye amemweleza mkuu wa mkoa mikakati mbalimbali ya manispaa zake zilivyotengewa fedha kutoka ofisi ya Rais Dkt.John Magufuli.



Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul makonda amesema kuwa manispaa za jiji lake zimetengewa bajeti ya bilioni 250 kutoka mfuko wa Rais ili fedha hizo zitumike kujenga vitega uchumi vilivyo ndani ya manispaa za jiji hilo ili hapo baadaye manispaa zenyewe ziweze kujiendesha kwa mapato zenyewe bila kuhitaji mikopo tena zenye liba kubwa.



Makonda, amesema kuwa wananchi waendelee kumpa ushirikiano Rais Magufuli kwani amedhamiria kwa dhati kuweka mazingira bora kwa wananchi wake.



Amesema Stendi hiyo ya kisasa iliyotengewa bilioni 50 lengo ni Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na kituo bora na kutengeneza ajira kwa vijana pamoja na wageni mbalimbali kuweza kufika kwa ajili ya utalii wa ndani.



Pia soko la kisutu, machinjio ya Vingunguti na mambo mengine yametengewa bajeti kutoka ofisi ya rais tayari kuanza kwa ujenzi ili wakazi wa jiji la Dar waweze kunufaika.



Ameeleza lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na raslimali ya nchi yake japokuwa wapo baadhi ya watu wasioipenda maendeleo ya nchi na kuzungumza mambo yasiyokuwa na manufa kwa Taifa.



Makonda amewataka wakurugenzi kusimamia fedha hizo zilizotolewa na Rais kwani ambaye atakwenda kinyume hatasita kumripoti kwa rais kutokana na kwenda kinyume.



Na Denis Mtima/Gpl.
Screenshot_20180511-081020.png
Screenshot_20180511-080540.png
Screenshot_20180511-080521.png
Screenshot_20180511-080311.png
Screenshot_20180511-080357.png
Screenshot_20180511-080238.png
Screenshot_20180511-080052.png
Screenshot_20180511-080040.png
Screenshot_20180511-080348.png


DMDP Mega city project worthy almost 1 trillion
 
This should be integrated with the sgr station.

I hope it's not isolated.

How far is this bus stand from the SGR station at Dar?
 
Kujazana upepo tu,hiyo stand na hizo hotels zitamsaidia nini mwananchi aliyeko kule Mpitimbi huku kg 1ya sukari akiinunua Tsh2,600/= mafuta ya kupikia kipimo 1,000/=

Sasaivi kuna hiko mnachoita mwendokasi,bora mtu akapanda guta atawahi anakoenda kuliko kusubiri hayo madude,hakuna tunachoweza kusimamia kikaenda straight vyote hovyo hovyo tu.
 
Hivi kwa akili yako unamuamini BASHITE? Bashite hajawahi kufanikisha Projects yake hata MOJA anafanya hivyo kwa ajili ya Agenda Settings / KIki kwa Pikipiki.

Issue ya Pili ni Kupiga pesa tu kwa kutumia MAYANGA Constructions Company au Kampuni Zake Zilizojificha Kujenga hizo projects nyie fuatilieni tu kwa umakini hizo kampuni kubwa zilizochukua tenda ya kujenga lazima zina mikono ya wakolomije na mziramkende.
 
This should be integrated with the sgr station.

I hope it's not isolated.

How far is this bus stand from the SGR station at Dar?
This is for regional busses which mainly will be suitable for travelers from or to Southern Highlands regions like Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe and those from Northern regions where SGR is not reaching them and they allocate this terminal from city center to avoid traffic congestion
 
Kujazana upepo tu,hiyo stand na hizo hotels zitamsaidia nini mwananchi aliyeko kule Mpitimbi huku kg 1ya sukari akiinunua Tsh2,600/= mafuta ya kupikia kipimo 1,000/=

Sasaivi kuna hiko mnachoita mwendokasi,bora mtu akapanda guta atawahi anakoenda kuliko kusubiri hayo madude,hakuna tunachoweza kusimamia kikaenda straight vyote hovyo hovyo tu.
Wazee wakulalamika mmeanza😀😀 Uliambiwa serikali inagawa sukari ?? 😀😀Huwezi kumlizisha kila mtanzania😀😀 Endelea kulilia sukari😀😀 Maendeleo Chap Chap😀😀
 
Saaafi sana
Mwenye Enzi Mungu atuongoze milele yote
 
Back
Top Bottom