Hizi radi leo kazini kwangu kuna kazi

Hizi radi leo kazini kwangu kuna kazi

Sauti ya radi tu ndio yakutisha...

Ile makitu inatangulia umeme/mwanga halafu sauti huja baadaye ikishakuwa imelamba kitu ilichokishukia...
ni kweli lakini sauti ndio inatesa kisaikolojia na ndio inaogopeka, mwanza kuna nyumba ipo mlimani ilianguka kwasababu ya mtetemo wa ile ngurumo waliokuemo waliumia sana nusura wafariki
 
Astraphobia naskia huwa mara nyingi inaisha yenyewe me pia mkuu nimejitahidi imepungua, lakini bado ipoipo mvua ya radi zile kali kali ikinyesha huwa inanipa wakati mgumu
Mkuu astraphobia ni nini ama ndiyo hiyo hali ya kuogopa radi?
 
Mimi ule muungurumo naogopa na siwezi kuzoea najiona kabisa ndo ishakua udhaifu wangu 🥺
Wewe ndiyo mimi kabisa.
Kuna kipindi huwa tunakwenda usiku baharini.

siku moja ikashuka mvua kubwa sana yenye upepo na radi, ah ile siku nilishahesabu nimekufa, ule umeta halafu ni usiku bahari yote inaonekana kama mchana, zikija hizo ngurumo ndio nasema, hii ishashuka ipo utosini.
 
Huwa ikianza mvua ya radi nazima simu, nikiona mtu anatumia simu natamani hata niikwapue niizime chaajabu unashangaa anapiga simu hata hawazi dah 😀 napagawa!...
 
Wewe ndiyo mimi kabisa.
Kuna kipindi huwa tunakwenda usiku baharini.

siku moja ikashuka mvua kubwa sana yenye upepo na radi, ah ile siku nilishahesabu nimekufa, ule umeta halafu ni usiku bahari yote inaonekana kama mchana, zikija hizo ngurumo ndio nasema, hii ishashuka ipo utosini.
Kama ni mdada uje tuliwazane jamani, hizi radi na ngurumo zinatisha sana🥲😄
 
Wanasema eti therapy yake unaweka sauti za ngurumo na radi unasikiliza nishafanya sana wapi!!! Sema kila mtu ana msala anaouogopa wadada wanaogopa mamdudu kama jongoo,nyoka,mende, na buibui ila siviogopi kabisa
wengine wanaogopa kuwa juu kama ghorofani na kutazama chini
Wengine wanaogopa mtihani [emoji3]
Vyote vidogo kwangu mchawi radi [emoji3]
 
Kama ni mdada uje tuliwazane jamani, hizi radi na ngurumo zinatisha sana🥲😄
Screenshot_20250201_171915_Google.jpg
 
Wanasema eti therapy yake unaweka sauti za ngurumo na radi unasikiliza nishafanya sana wapi!!! Sema kila mtu ana msala anaouogopa wadada wanaogopa mamdudu kama jongoo,nyoka,mende, na buibui ila siviogopi kabisa
wengine wanaogopa kuwa juu kama ghorofani na kutazama chini
Wengine wanaogopa mtihani [emoji3]
Vyote vidogo kwangu mchawi radi [emoji3]
Yaani unasikiliza sauti za kwenye radio?
 
Back
Top Bottom