TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Hahaa..🤣🤣 mmenikumbusha miaka ya nyuma kidogo kuna taasisi moja nilikua nimeajiriwa. Bosi wetu alikua mwanamke ni mkali kama pilipili! Kichekesho kilitokea siku imenyesha mvua na radi aisee yule mama ni muoga wa radi sijawahi kuonaa! Kitendo cha radi kupiga kufumba na kufumbua tulimkuta mama yupo chini ya meza, mikono kaziba masikio, macho kafumba na ukunga kama kuna msiba vile... Watu wote tuliokuwa ofisini (na wateja kibao) tulibaki kucheka kuanzia siku hiyo tukawa hatumuogopi tena 😀
Anyway, mimi binafsi huwa sipendi kelele za aina yoyote so mara nyingi mvua zikianza huwa navaa "earplugs" nalala zangu.
Anyway, mimi binafsi huwa sipendi kelele za aina yoyote so mara nyingi mvua zikianza huwa navaa "earplugs" nalala zangu.