Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

1. SEDENTARY AGRICULTURE
2. SHIFTING CULTIVATION
 
1. Sedentary farming
2. Nomadic farming

Kwa nini wanaulizwa maswali magumu badala ya wafundishwe.
 

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mi nimempiga mkwara akija na homework zake aje na text book ya Hilo somo coz majibu lazima yawemo umo. Maana anakawaida ya kuacha vitabu shule. Sitakangi ujinga.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nilidhani tatizo liko kwangu tu, kumbe hata kwa wengine? Mtoto wangu ameanza darasa la kwanza 'medium school'. Mbali na ada kuna tuition. Halafu naona kwamba watoto wanafundishwa kwa kukaririshwa na siyo kuelewa. Nijuavyo mimi tuition inahitajika labda kwa mtoto mwenye mahitaji maalumu na siyo kwamba ni aina ya ku'catch up' kwa mwanafunzi darasani. Ada tunalipa kubwa, mtoto haelewi na hata anayofundishwa tuition haelewi na tuition iko kwenye Sh25,000 kwa mwanafunzi. Watoto wanapewa diary kuleta nyumbani, halafu unakuta mtoto ndiye anayeambiwa aandike kwenye diary. Sasa kama mtoto hajaelewa anachotakiwa kufanya, mzazi hajui mwalimu anachohitaji. Watoto pia wanafundishwa na walimu ambao wako trained kufundisha madarasa ya juu, lakini hawana skills za kuwafundisha watoto wadogo. Ni shida na inanipa hasira sana maana naona kama ada ninayolipa inakufa bure!
 
Mtoa upo sahihi kabisa,kazi yako ni kumfundisha Mtoto maadili yanayotakiwa kijamii.ualimu ni kitu professional ndio maana watu husomea kazi hizo na wanalipwa mishahara.

Nashangaa wanao kubeza humu Elimu zao hazijawasaidia,na hawajajua ulicho kisema.ni vyema kila moja atimize wajibu wake.
Na mbaya zaidi Mtoto anaondoka sa 12 asubuhi anarudishwa na 11 jioni,yani Mtoto anakosa hata muda wa kucheza na kufanya kazi ndogo ndogo kukuza ubongo wake hadi watoto wengine siku wanamaliza form 4 hawajawi shika hata kwanja.
 
Dogo aliwahi kuja na hii, "Parents use mobile phones, ___________, ___________ and ________.

😂😂😂😂😂!

Utopolo mtupu.

Swali ambiguous lisilokuwa na mbele wala nyuma!
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Mtoto wangu Homework ya Kiswahili alikosa methali na nahau, mtoto akaulizwa nani kakusaidia akajibu baba... Mwalimu akamwambia babaako na wewe wote akili hamna....

Taarifa ikanifikia, nikaona isiwe tabu, kwakuwa ni class VII nimemhamisha mkoa yupo boarding na homework hainihusu tena.
 
Kama mfumo umebadilika na sisi wazazi kuwa sehemu shirikishi mbona ada zinaendelea kupanda bila kufikiria tunafanya kazi ya ualimu pia.!!
Hivi unadhani ni wazazi wangapi wanajua kila kitu watoto wao wataulizwa.!?
Kwanza masomo mengi.
Walimu wafundishe wanafunzi namna ya kupata majibu kutokana na walichowaelekeza.
Sio kuwapa tu homework waje kuuliza nyumbani.
Inaonesha mwanafunzi hajaelewa ulichomuelekeza
 
Niliwahi jibu swali la Ubepari vs Ujamaa nikiwa darasa la tano na kwenye mtaala hakuna tena. Mwalimu alishangaa nimejuaje, kata nzima walikosa swali. Mitihani ya kushirikisha shule nyingi huwa kuna maswali baadhi magumu kimakusudi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hizo shule za bei kubwa kuna wanaochukua sylabus ya in cambrdge . Kule uigerza mzazi ni mwalimu wa homework mila siku mtoto anakuja homework. Vumklia ndiyo gharama ya kusomesha international.
 
Elimu shirikishi,pole usichoke

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
Hii elimu shirikishi inaendana na tunacholipia?!?

Nina jamaa yangu aliwafuata walimu shuleni na kuwaambia ukweli baada ya kuona mwanaye anaandika sentence kwa kuunganisha maneno.
Yaani nilipe ada aafu nianze kumfundisha mtoto namna ya kuandika maneno.
Namna ya kutenganisha maneno
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Unaona Sasa.
Tutakuwa tunauliza vingapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…