Munambefu
JF-Expert Member
- Jun 24, 2012
- 2,811
- 7,200
Nani Kakudanganya kayumba hawawezi kufikiri?Hehehehehee mtoe hapo mpeleke kayumba aje awe kama wewe...asiweze kufikiri zaidi
English medium ni kiingereza tu anaongeza sio maarifa, Kama mwanao ni kiazi English medium haiwezi kumfanya genius, Na Kama ni genius Hata akisoma kayumba atatamba tu.
Hebu tafakari, kuna mtoto A anasoma primary na secondary Kwa gharama ya mil 20+,na kuna mtoto B anasona kayumba primary, Kata secondary halafu wanakutana chuo kikuu wote wanagraduate degree ile ile.
Wakishagraduate wote wanakuwa jobless, yule aliyesoma akiwa anaenda Kwa school bus anajikalia zake Nyumbani Mara Kwa uncle, hawezi kujiongeza kwasababu amezoea kulishwa kila kitu, aliyesoma kayumba anajiongeza kwasababu ni mpambanaji tangu mwanzo.
Huo ndio uhalisia uliopo mtaani, sasa Nani mwenye akili hapo?
Na Kwa Mzazi mwenye akili kuliko kupeleka mwanao akajifunze kiingereza,kuchora na kuimba Kwa mamilioni huko English medium ni bora Kama unaona ana uwezo mzr ukampekeka kayumba ukamfungulia fixed account, hiyo pesa ya ada ukawa unamuwekea Kwa uaminifu, akifika chuo atakuwa Na mtaji mkubwa sana wa kujiajiri.