Nilidhani tatizo liko kwangu tu, kumbe hata kwa wengine? Mtoto wangu ameanza darasa la kwanza 'medium school'. Mbali na ada kuna tuition. Halafu naona kwamba watoto wanafundishwa kwa kukaririshwa na siyo kuelewa. Nijuavyo mimi tuition inahitajika labda kwa mtoto mwenye mahitaji maalumu na siyo kwamba ni aina ya ku'catch up' kwa mwanafunzi darasani. Ada tunalipa kubwa, mtoto haelewi na hata anayofundishwa tuition haelewi na tuition iko kwenye Sh25,000 kwa mwanafunzi. Watoto wanapewa diary kuleta nyumbani, halafu unakuta mtoto ndiye anayeambiwa aandike kwenye diary. Sasa kama mtoto hajaelewa anachotakiwa kufanya, mzazi hajui mwalimu anachohitaji. Watoto pia wanafundishwa na walimu ambao wako trained kufundisha madarasa ya juu, lakini hawana skills za kuwafundisha watoto wadogo. Ni shida na inanipa hasira sana maana naona kama ada ninayolipa inakufa bure!