Hizi sio mboga ni jaza tumbo

Hizi sio mboga ni jaza tumbo

Kuna baadhi ya majani tumeamua kuyatunuku cheo kwamba ni mboga za kushushia na chakula.
Ila mimi nazipinga.

Mfano:
Majani ya maboga
Kisamvu
Mchunga
Majani ya kunde
Matembele
Mlenda

Mengine nimesahau majina.

Tuache kuyapakazia kuwa ni mboga, tunayasingiziq na hayana manufaa yoyote mwili bali ni shushia ugali tu.
Sasa mkuu ukitoa hizo mboga zote za majani itabaki mboga gani natural?
 
You know nothing about nutrients

Dig more knowledge as to get rid from the ignorance hole.
Mkuu, huenda hajui kweli lakini kupitia uzi wake atapata majibu ya vitu asivoona havina maana kwake. Mfano mmoja

Bamia kwa wasioijua ambayo ikipikwa huja kutengeneza mlenda huo mleta mada anaousema ni kishushio cha ugali ni grisi ya mwili. Kama uko na viungo vyako ukivinyoosha iwe ni mkono au ni mguu ukiunyoosha unasikia kwenye joint kama umevunjika, jua kwamba grisi yako eneo hilo imeisha na unatakiwa uwongeze grisi ili kuzui msuguano eneo hili na maeneo mengine ya mwili pili unyooshapo viungo vyako.

Grisi unaipataje sasa kupitia kula bamia? Katakat vipisi vidogo, weka maji kidogo na uchemshe, uache ipoe kisha kula... Hiyo kula mara moja au kula mara 2 after 2 day njoo namajibu hapa.....
 
Mchunga ndio funga kazi, km una maralia wewe piga huo 🤣🤣🤣
 
Aisee me siwezi kula ugali au wali bila mbogamboga aisee,,, Napenda sana... Wewe mwenzetu unakulaga nini kama mbadala wa hizo tujuze na Sisi tujue
 
Nmekaa kwa masai uko oldonyo nmeshangaa wanakula majan ya sungura asee ngoja niyatafute pch yake
 
Screenshot_20240405-205730_1.jpg
 
Back
Top Bottom