Salaam, shalom!!
1. Tulipokuwa tukisubiri kupokea Mikataba mliyoiita HGA ya mkataba wa Bandari mlisema mikataba hiyo itakuwa wazi italetwa na kujadiliwa bungeni, hatujakaa sawa, tukasikia mikataba imeshasainiwa huko Dodoma kimya kimya na siku hiyo hiyo akateuliwa Katibu Mwenezi wa chama tawala!!
Tukaachana na Bandari, tukaanza kumjadili kijana machachari.
2. Tuliambiwa na Rekodi ziko humu kuwa, wafanyakazi wa bandarini ajira zao hazitaguswa ajapo DP world, Cha kushangaza wameambiwa wachague kusuka au kunyoa, tukiwa Bado tunatafakari hayo, ghafula tunasikia ndugu zetu huko Zanzibar wanacharazwa bakora Kwa kosa la kula chakula Chao peupe!!
3. CAG analeta Ripoti mezani, mara tunasikia hati chafu zote zimekuwa safi Kwa 99%, tunaambiwa mashirika yote yanepata HASARA, pesa ni za mikopo na mkopo ndo kwanza hata robo hatujalipa.
Tukiwa tunatafakari hayo, ghafula tunasikia uteuzi na utenguzi, Mwenezi ghafula Kawa mkuu wa mkoa Arusha,Mara waziri kawekwa pembeni.
Mimi najiuliza, tujadili kipi tuache kipi?
Rais Mstaafu KIKWETE: Nchi haipoi kama ugali!!
Nchi yangu Tanzania nakupenda sana , Ubarikiwe, Nitaendelea kukuombea.
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Pasaka njema.
Karibuni 🙏