Hofu ya Corona: Rais Magufuli asitisha mbio za Mwenge 2020. Fedha kupelekwa ktk maandalizi ya kupambana na Corona

Hofu ya Corona: Rais Magufuli asitisha mbio za Mwenge 2020. Fedha kupelekwa ktk maandalizi ya kupambana na Corona

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
8,926
Reaction score
17,880
Habari zenu wakuu,

Kutokana na kusambaa kwa virus vya Coron, Rais wa Jamhuri ya Muungano amepiga marufuku mbio za Mwenge kwa mwaka huu ili kuzuia mikusanyiko isiyo rasmi

Very nice for our caring president ,long live baba
---

Rais amesema Mbio za Mwenge zinakusanya watu wengi sana na katika kupambana na #Coronavirus amesitisha mbio hizo hadi tatizo hilo litakapo koma na kuhakikisha halipo

Amesema Mbio za Mwenge zilikuwa zianze Zanzibar ila hazitaanza na fedha zilizokuwa zitumike katika mbio hizo zitapelekwa Wizara ya Afya ili kusaidia katika maandalizi ya kupambana na Corona

Amesema "Inawezekana hata akatayeshika Mwenge huo akawa na corona na badala ya Mwenge kuwa wa amani na matumaini ukageuka kuwa Mwenge wa kuhatarisha maisha ya Watanzania

Aidha, amesema kama hatua hizi za corona zitaisha kabisa basi mbio za mwenge zinawea kufanyika kwa siku hata tatu ila kwa sasa tahadhari ni lazima
 
Hana nia ya dhati kuzuia Corona isiingie nchini kwa kuzuia mbio za mwengu huku mikusanyiko mingene ikiachwa iendelee.

Angekuwa serious,angezui ndege, hasa kutoka katika mataifa yaliyoathirika vibaya na corona, kuingia nchini.

Semeni tu kama lengo ni kuacha iingie alafu uchaguzi uairishwe.
 
Rais Jpm amesitisha mbio za mwenge 2020 na fedha kuelekezwa katika mapambano dhidi ya homa hatari ya Corona. Big up Mh. Rais
 
Nasikia hata wafanyakazi wa jf wakuwa wanafanya kazi majumbani mwao, sijui nini kinaendelea aisee.
 
Back
Top Bottom