Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mshana ,sio wote tunamfahamu Forojo...namna ulivoandika Ni Kama vile wote tunamjua...hebu tudondlee. Huyu Ni Nani,kulikuwa na Nini Hadi akatoa utabiri huu
Wewe ndio pita mbali kwa unayoona hayakuhusu.Mambo mengine yawe yanakupita
Sio kila jambo unalijua
Kuliundia Story Za hovyo
Sasa ndio umeandika nini ewe punguani? Inaonekana na wewe ushafanywa zindiko tayariMnao Amini Ushirikina shauri yenu, mtashindwa kufanya mambo yenu kisa mwenge umezuia Chadema ushindi,
Na kama ni mwenge umezuia ushindi wa Chadema, iweje watu wanakesha kulaumu muundo wa Tume?
Kwa nini kulaumu Magufuli anawanunua wapinzani?
Kama kweli mwenge ndio kikwazo cha Vyama pinzani kutokushika Dola, Kwa nini sasa vinahangaikia mambo ambayo hayana sababu?
Tatizo letu sio mwenge na Wala sio mazindiko, Sisi ni watu waoga na ni watu duni, Sina hakika na Elimu yetu kama huwa inatusaidia
Elimu yetu imekuwa ndio sababu ya haya yoote, tafiti zetu zote ni za uongo na hatujawahi kujiamini hata kama tukifanya utafiti sahihi bado tutataka aje mtu mweupe atuthibitishie utafiti wetu
Mnao Sema Mwenge kwamba Ni Zindiko, mwenge umezindika Akili zetu Watanzania hembu thibitisheni hapa, leteni utafiti wa kisayansi na mthibitishe hapa, na utakuta mtu amekomalia Mwenge kuwa ni Zindiko la akili zetu naye ni msomi
Acheni uoga na sababu zisizo na Maana, jipangeni, tengenezeni Sera zenye kushawishi watu, mwenge si lolote ni kibatali tu kile kinamaliza Kodi zetu Ila hauwezi kuathiri akili na ufahamu wetu
umeanza lini kuwa hivi, Kwa hiyo na wewe unaamini nguvu za Giza siyo?Wewe ndio pita mbali kwa unayoona hayakuhusu.
Inaelekea hujui kuwa chama chako kimekuwa kinaendeshwa kwa nguvu za Giza na makafara kila kukicha.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nilijua Zindiko linatuhusu sote Mimi na wewe na Watanzania wote, kumbe ni mmojammoja? Okey Sawa mwelevuSasa ndio umeandika nini ewe punguani? Inaonekana na wewe ushafanywa zindiko tayari
Sent using Jamii Forums mobile app
UNATUCHANGANYA MKUUU...WACHAWI SIO WATU WA DINI ILA NI WACHAWI.WATU WA SHETANIWanaomuabudu shetani ni watu wenye dini.. Wachawi hawamwabudu kwakuwa sio watu wa dini
Jr[emoji769]
Mnaamini nguvu za giza sana[emoji34][emoji34][emoji34]
Mshana Jr. Wewe na sinni mtaalam? Tupe kidokezo basi.
Binafsi ningependa Tanzania iwe ya Bwana Mungu muumba mbigu na nchi
Sent using Jamii Forums mobile app
Tuachane na kafara za kukimbiza moto
Jr[emoji769]
Rushwa imeisha? Mauaji ,utekaji na kufunguliwa kesi za uongo kwa Wapinzani vimeshamiri sana awamu hii.Laana isiyo na sababu haimpati mtu, watu waendelee kuombea nchi, ikiwa ni wakati ambao Mungu ameruhusu CCM ipatwe na mabaya basi itapatwa, ikiwa yeye hajaruhusu basi haitatokea.
Kikubwa uovu wa nchi umeondolewa kwa sasa, ashukuriwe Mungu aliyeumba mbingu na nchi, tuzidi kuombea Taifa letu.
Sent using Jamii Forums mobile app
UTANGULIZI: Akinukuu maneno hayo Sheikh Yahya alisema Forojo alimwambia Nyerere: “Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau.
“Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwalimu Nyerere, Ganze alikata roho na siku chache baadaye Mwalimu Nyerere akayafanyia kazi maneno yake na kuanzisha Mwenge wa Uhuru ambao ulipandishwa Mlima Kilimanjaro na Kapteni Alexander Nyirenda aliyekuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),” alisema Sheikh Yahya.
Hata hivyo, mtaalam huyo wa unajimu alisema kilichowashangaza wengi ni maneno yaliyoongozwa yasemayo “UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU ULETE TUMAINI” akahoji ina maana ndani ya nchi tubaki gizani? Sheikh Yahya Hussein alisema anashangazwa kwa nini Forojo Ganze hakutangazwa kama mwanzilishi wa Mwenge wa Uhuru kwani baada ya mazishi ya Forojo, ulianzishwa ambao ulikimbizwa nchi nzima mara tu baada ya uhuru mwaka 1961 na unaendelea kukimbizwa hadi sasa.
Nyerere alimuagiza Sheikh Yahya Hussein atafsiri maana ya ile namba 115 aliyokuwa ameiandika mkononi Forojo akamwambia:
“Namba 115 maana yake utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na Taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38,” na ndivyo ilivyokuwa. Mwaka 1999 Mwalimu Nyerere alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru na 77+38=115, namba aliyoiandika Forojo Ganze mkononi.
Unaitwa Mwenge wa uhuru na ulikimbizwa nchi nzima mara baada tu ya uhuru. Kuna mtu mmoja muhimu sana kwenye hili jambo naye si mwingine bali ni Mzee Forojo Ganze. Aliekuwa kaandika mkononi mwake no 115. Tafsiri yake ilikuwa hii. Mwalimu Nyerere atakufa akiwa na miaka 77. Wakati wa kifo chake taifa huru la Tanzania litakuwa na umri wa miaka 38. Utabiri huu ulitimia.
Kuna kitu Mzee Ganze hakukisema pengine kwa kupitiwa ama kifo kumuwahi kabla hajakisema. Nacho ninini kitamtokea mtu atakayevunja masharti ya zindiko. Imeshasemwa mara nyingi ya kwamba Mwenge ni zindiko na kafara la kukimbiza moto na lilikuwa maalum kwa ajili ya kumbakisha mwalimu madarakani na kulinda uhuru. Je, kuna ukweli kwenye hili?
Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau.
Je, mwenge umeendelea kuleta tumaini pasipo na tumaini?
Je, mwenge umeendelea kuleta upendo palipo na chuki?
Je, mwenge umeendelea kuleta heshima palipo na dharau?
Je, mwenge umeendelea kuleta tumaini pasipo na tumaini?
Kusitishwa sherehe za uhuru pengine ilikuwa kiashiria cha kwanza cha kuvunja masharti ya zindiko na kafara la moto.. Na kama bado huamini hili ona na mbio za mwenge mwaka huu zimesitishwa kwa sababu ya corona.. Sababu huwa kichokoo kikubwa cha kuvunja agano na masharti yake
Wahusika wote wenye ufahamu na hili jambo hawapo tena duniani.. Wa mwisho alikuwa mnajibu na mtabiri maarufu Sheikh Yahaya. Hakuwahi pengine kuzungumzia au walau kuulizwa nini kitatokea kama zindiko lisipofanyika? I mean la kukimbiza moto. Ni wazi sote tulitiwa upofu na kusahau haya yote.
Zindiko na kafara huwa na kikomo cha kuwa hasa lisipohudumiwa.. Ndio maana waliofanikiwa hawaachi kufanya mazindiko na makafara kila wiki, mwezi au mwaka ili ku boost. Ubaya wake ni mmoja tuu kamwe zindiko na kafara havina rivasi na KIPIMO huongezeka kila wakati. Kikomo cha kuwa kinapofikia ukomo. Nyakati zinapotimia sababu ndogo mno hubatilisha kila kitu.
Kuna sababu nzito za kiroho zilizo juu ya ufahamu wetu wa kawaida wa kibinadamu zilizosababisha kusitishwa kwa mbio za mwenge na sherehe za uhuru. Picha ya mwenge wa uhuru ilitumika vilivyo kwenye mabango ya ccm na PICHA za wagombea wake. Je, ndio ilikuwa matumizi ya mwisho?
Wakati utasema.
Jr[emoji769]
Kafara la kukimbiza moto linavyoligharimu Taifa - JamiiForums
Kwaamaana hiyo sasahivi nikiona namba moja mbele yangu basi niamini kwamba nimoja?Kikubwa uovu wa nchi umeondolewa kwa sasa,..... Thoughtful..
Jr[emoji769]
Kwaamaana hiyo sasahivi nikiona namba moja mbele yangu basi niamini kwamba nimoja?
Namaanisha kwasasa tutakuwa tunaona nakusikia vitu halisi maluelue ndio basi tena?
Mnamaanisha giza lilipozidi ndio ilikuwa dalili yahaya yote?
Mnamaanisha mchawi kayaula kasahau nguvu zake zilipo?
Au Mnamaanisha wazee wamemzira nahawajamwambia nini siri yaurembo?
Au yawezekana nayeye anamacho kama yetu yakuutazama mwenge kama kibatari kikubwa au limoto lisilokuwa namaana kumbe kuna kingine nyumba yapazia?
Nakama mwenge kumbe ulikuwa hauna maana yoyote zaidi yakuwaka2 kwanini isiwe ndio mwanzo na mwisho wake kurandaranda mitaani kila mwaka? Vilevile tukae Chini tutasmini toka uanzwe kukimbizwa miaka yote hiyo umetutia hasara kiasi gani kama taifa.
Sent using Jamii Forums mobile app