Hofu ya Corona: Rais Magufuli asitisha mbio za Mwenge 2020. Fedha kupelekwa ktk maandalizi ya kupambana na Corona

Hofu ya Corona: Rais Magufuli asitisha mbio za Mwenge 2020. Fedha kupelekwa ktk maandalizi ya kupambana na Corona

Wale tunaobanana na kupigana ngumi ili tuwahi seat ndani ya usafiri wa mwendo kasi hatujapigwa marufuku?

Naona mizaha imezidi kuhusu Corona
 
Jana Rais magufuli alitangaza kuelekeza pesa za mwenge kwenye vita dhidi ya ugonjwa huu hatari uliotikisa dunia, Nikajiuliza hivi hatuna pesa za dharura kama nchi kupambambana na majanga kama haya?

Nchini Marekani bunge lao lilipitisha kiasi cha dola bilioni 50 kutoka kwenye mfuko wa dharura kupambana na huu ugonjwa lakini hapa kwetu sikusikia hata spika akiitisha kikao cha dharura kujadili na kutoa maazimio ya jinsi ya kukabiliana na huu ugonjwa ingawa ugonjwa huu ulipatikana na kuanza kusambaa duniani kabla bunge kuhairishwa.

Hau nchi yetu haina hata dola bilioni 200 kwenye mfuko wa dharura itenge hata dola bilioni 20 kupambana na hili janga la dunia?

Uzuri wa huu ugonjwa ni ugonjwa unaopanda Ndege na kiongozi Mkuu ndiye kinara wa kukutana na waliokuja nchini kwa Ndege hivyo sio kama kipindupindu kinachobagua wachafu tu.

Na inavyo onyesha Nchi haina vifaa ama wataalamu wa kugundua huu ugonjwa kwenye viwanja vya Ndege (tukirejea tukio la Arusha) hivyo tujiandae kufa kama kuku tukianzia na Wakuu hadi raia wa kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashauri pesa za Mwenge zikagawanye kila mkoa ili kujipanga na Corona.
 
Wanaomba tu tumejipanga, kumbe hamna lolote. Wanapiga propaganda za hovyo, mfupi tumejua maabara Ni moja na wagonjwa wa Corona wanapita Airport kilaini tu...hakuna vipimo Airport.

Pesa ya Dharura Haipo, Hata Tetemeko la Kagera, michango ya wasamaria ilikwapuliwa.
 
UTANGULIZI: Akinukuu maneno hayo Sheikh Yahya alisema Forojo alimwambia Nyerere: “Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau.

“Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwalimu Nyerere, Ganze alikata roho na siku chache baadaye Mwalimu Nyerere akayafanyia kazi maneno yake na kuanzisha Mwenge wa Uhuru ambao ulipandishwa Mlima Kilimanjaro na Kapteni Alexander Nyirenda aliyekuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),” alisema Sheikh Yahya.

Hata hivyo, mtaalam huyo wa unajimu alisema kilichowashangaza wengi ni maneno yaliyoongozwa yasemayo “UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU ULETE TUMAINI” akahoji ina maana ndani ya nchi tubaki gizani? Sheikh Yahya Hussein alisema anashangazwa kwa nini Forojo Ganze hakutangazwa kama mwanzilishi wa Mwenge wa Uhuru kwani baada ya mazishi ya Forojo, ulianzishwa ambao ulikimbizwa nchi nzima mara tu baada ya uhuru mwaka 1961 na unaendelea kukimbizwa hadi sasa.

Nyerere alimuagiza Sheikh Yahya Hussein atafsiri maana ya ile namba 115 aliyokuwa ameiandika mkononi Forojo akamwambia:

“Namba 115 maana yake utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na Taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38,” na ndivyo ilivyokuwa. Mwaka 1999 Mwalimu Nyerere alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru na 77+38=115, namba aliyoiandika Forojo Ganze mkononi.

Unaitwa Mwenge wa uhuru na ulikimbizwa nchi nzima mara baada tu ya uhuru. Kuna mtu mmoja muhimu sana kwenye hili jambo naye si mwingine bali ni Mzee Forojo Ganze. Aliekuwa kaandika mkononi mwake no 115. Tafsiri yake ilikuwa hii. Mwalimu Nyerere atakufa akiwa na miaka 77. Wakati wa kifo chake taifa huru la Tanzania litakuwa na umri wa miaka 38. Utabiri huu ulitimia.

Kuna kitu Mzee Ganze hakukisema pengine kwa kupitiwa ama kifo kumuwahi kabla hajakisema. Nacho ninini kitamtokea mtu atakayevunja masharti ya zindiko. Imeshasemwa mara nyingi ya kwamba Mwenge ni zindiko na kafara la kukimbiza moto na lilikuwa maalum kwa ajili ya kumbakisha mwalimu madarakani na kulinda uhuru. Je, kuna ukweli kwenye hili?

Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau.

Je, mwenge umeendelea kuleta tumaini pasipo na tumaini?
Je, mwenge umeendelea kuleta upendo palipo na chuki?
Je, mwenge umeendelea kuleta heshima palipo na dharau?
Je, mwenge umeendelea kuleta tumaini pasipo na tumaini?

Kusitishwa sherehe za uhuru pengine ilikuwa kiashiria cha kwanza cha kuvunja masharti ya zindiko na kafara la moto.. Na kama bado huamini hili ona na mbio za mwenge mwaka huu zimesitishwa kwa sababu ya corona.. Sababu huwa kichokoo kikubwa cha kuvunja agano na masharti yake

Wahusika wote wenye ufahamu na hili jambo hawapo tena duniani.. Wa mwisho alikuwa mnajibu na mtabiri maarufu Sheikh Yahaya. Hakuwahi pengine kuzungumzia au walau kuulizwa nini kitatokea kama zindiko lisipofanyika? I mean la kukimbiza moto. Ni wazi sote tulitiwa upofu na kusahau haya yote.

Zindiko na kafara huwa na kikomo cha kuwa hasa lisipohudumiwa.. Ndio maana waliofanikiwa hawaachi kufanya mazindiko na makafara kila wiki, mwezi au mwaka ili ku boost. Ubaya wake ni mmoja tuu kamwe zindiko na kafara havina rivasi na KIPIMO huongezeka kila wakati. Kikomo cha kuwa kinapofikia ukomo. Nyakati zinapotimia sababu ndogo mno hubatilisha kila kitu.

Kuna sababu nzito za kiroho zilizo juu ya ufahamu wetu wa kawaida wa kibinadamu zilizosababisha kusitishwa kwa mbio za mwenge na sherehe za uhuru. Picha ya mwenge wa uhuru ilitumika vilivyo kwenye mabango ya ccm na PICHA za wagombea wake. Je, ndio ilikuwa matumizi ya mwisho?

Wakati utasema.

a25.jpeg

Jr[emoji769]
Kafara la kukimbiza moto linavyoligharimu Taifa - JamiiForums
 
Laana isiyo na sababu haimpati mtu, watu waendelee kuombea nchi, ikiwa ni wakati ambao Mungu ameruhusu CCM ipatwe na mabaya basi itapatwa, ikiwa yeye hajaruhusu basi haitatokea.

Kikubwa uovu wa nchi umeondolewa kwa sasa, ashukuriwe Mungu aliyeumba mbingu na nchi, tuzidi kuombea Taifa letu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kikubwa uovu wa nchi umeondolewa kwa sasa,..... Thoughtful..

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom