AggerFirminho
JF-Expert Member
- Sep 17, 2019
- 2,318
- 4,106
#Hapingwi na mtu yyte# mbona alikoswakoswa kupinduliwa mara 2Forojo Ganze ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Forojo Ganze aliyezaliwa mwaka 1902 alifuatana na wazee wengine kwenda kwenye zindiko Bagamoyo ili Mwalimu Julius Nyerere aweze kutawala vema.
Wazee hao na miaka yao ya kuzaliwa kwenye mabano ni Mzee Ramadhan (1920), Ally Tarazo (1929), Komwe wa Komwe (1918) na Shehe Yahya Hussein (1925).
Wazee hao walipewa kazi hiyo na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam enzi hizo kuhakikisha rais aliye madarakani hapingwi na mtu yeyote, zindiko hilo lilifanyika Bagamoyo katika moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo na baadaye Mwalimu Nyerere alipelekwa Bagamoyo, akachinjwa mbuzi na Nyerere akaambiwa atambuke (aruke damu) baada ya kutokula kutwa nzima, jambo ambalo aliwahi kukiri hadharani katika moja ya hotuba zake.
Jr[emoji769]
Sent using Jamii Forums mobile app