Hizi hasira za upinzani za kuhisi wanaonewa ni hofu inayowaumiza kisaikolojia juu ya kupuuzwa na Watanzania
Kabla ya Rais Magufuli,Wanaccm walikuwa wanaona aibu kuvaa nguo za chama,na kuna Sehemu walikuwa wakitupiwa makopo wakikatiza mtaani
Wanaccm walificha sare zao ndani kutokana na masuala ya ufisadi kukithiri, kutokana na huduma za kijamii kudhorota
Lakini Upepo ulibadilika ghafla baada ya 2015
Mwenyekiti wa ccm akairudisha Ccm kwenye makali yak,Wananchi wakaanza kurudisha amani na CCM,wakaanza kuwapuuza wale wanaopinga serkali
Wananchi Wengi wamekimbia upinzani kimya kimya wamerudi CCM kutokana na kishindo cha awamu ya tano
Saaa nguo za chama zimetamalaki mtaani,kila mwananchi anajivunia kuwa CCM
Ukweli mchungu ni kwamba wapinzani wanaogopa sana CCM iliyotulia ,wanajua Ccm iliyotulia ni hawana chao
Ukiangalia hata wapinzani kushinda ubunge ilitokana na kukorogeka kwa ccm kulikopelekea kugawanya kura
Ccm iliyotulia,upinzani utaambulia viti vitatu tu vya Ubungo
Hata hii janja janja inayoendelea ya kususia Uchaguzi hisia zangu zinanituma tu hawa jamaa wamepima kina cha maji wakaona hapana hapa tutaaibika
Ndio mambo ya kubeba mpira kwapani yakaja
Tuendelee kumuunga mkono mh Rais katika juhudi zake za kuleta Maendeleo
NADILIKI KUJIBU kama mpinzani japo sina chama, ila mshabiki wa upinzani.
(Rejea kwenye blue hapo juu) Una uhakiki kuwa wananchi wana imani na CCM? Angalia kama wataitikia wito wa kujitokeza kupiga kula hiyo Nov. 24
(Rejea kwenyenjano) Waliorudi ni kwa njaa zao baada ya kuongwa au kuhakikishiwa pesa kwa njia ya madaraka. Tuonyeshe wengine waliorudi kimya kimya, au Nov. 24 tutawaona wakiwapigia kura?
(Rejea kwenye italiki) Wanaovaa nguo za chama ni kukwepa ugaidi wenu na kupata maslahi flani toka vyombo vya usalama. Ukitaka pitisha figisu zako sasa vaa kijani, ndipo mlipotupeleka huko. Mmepiga na kuumiza watu waliovaa jezi zingine.
(Rejea nilipopigia msatari) Jitahidi kuweka hoja nzito sio utoto, kweli wapinzani wanaogopa CCM iliotulia? Hivi ccm unaiona imetulia ........... hivi wanavyolukaluka akina Jafo na Mwenzie Kangi kweli mmetulia nyie au kuna sehemu viti vinawasha apakaliki. Hapo mmewafunga wapinzani mdomo lakini hamjatulia! point yako haina mashiko.
(Rejea kwenye blue italiki hapo juu) Wapinzani kushinda uchaguzi ilitokea na kuaminiwa zaidi na wananchi. Kama mlikorogana ni kwa maovu yenu kutokana na historia ya mfumo wenu na ndivyo mnavyokorogan sasa, hakuna jipya.
Mwisho kaBISA HAKUNA CCM ILIOTULIA KUANZIA KIONGOZ WENU MKUU, kauli hazijatulia vipaumbele havieleweki SIJUI KESHO ATAAMKIA NINI, KUZINDUA KIWANDA ama.... mwenyewe alishukuru wapinzani kujitoa kwenye uchaguzi unafikiri kwa nini?
KATULIA kweli huyu...?
sasa Jafo Kageuza gia angani, Kangi nae nimesikia "Akibwatuka hakuna kuzima simu hiyo 31 Disemba" kwa wasiosajili line.
Yaani Matamko mapya kila siku, tena bila aibu anamsingizia RAIS kataka iwe hivyo!! Mmetulia kweli nyie??!\
NCHI NDIO INAENDESHWA KWA MATAMKO HAYA?
Hakuna hata washauri wenye busara wakawaelimisha namna nchi inavyoendeshwa........ sio kwa matamko Mara hiv mara vile... Uchumi unazidi kuyumba Tulieni
Mwisho kabisa umesema "wapinzani wamepima kina cha maji wakaweka mpira kwapani" Hafadhali wao wameweka kwapani unaonekana, nyie mmeuficha kabisa kwa figisu zenu. Ni afadhali kuweka mpira kwapani kuliko kushindana mbio na NYATI asieelewa alama za nyakati, akijimwambafai kwa maguvu yake(ya dola).
CCM MNAJIARIBIA WENYEWE MSITAFUTE MCHAWI mana mchawi ni nyie wenyewe. Propaganda zenu humu mitandaoni ndio tunawachora vizuri, mnavyokengeuka. Kila anae wajibu CHADEMA, haya na mimi niiteni CHADEMA kwa kupangua hoja zako mfu.