Brainmachine
Member
- Oct 31, 2017
- 16
- 9
Mh! Wasiojulikana wamefanya yao nini??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anatafuta kiki huyoo, mbona mwaka mzima hatumsikii mnaleta mambo ya siku tatuWasalaam wana jamvi....
Msanii Q-Chillah toka juzi hajulikani alipo na watu wakaribu yake wameshindwa kumpata hadi sasa si kwenye simu au uso kwa uso na hawana taarifa yeyote popote alipo.
Taarifa za kupotea Kwa Q-chief zimeripotiwa jana na msanii mwenzie T.I.D kupitia E-fm radio akitaka kuujuza Umma au yeyote mwenye taarifa ya alipo Q-chief awajuze maana wana hangaika kumtafuta hadi sasa wameshindwa kumpata.
T.I.D anasema yeye mara ya mwisho waliahidiana na Q-chief wakutane sehemu fulani lakini baadae alimpigia kumwambia atapita sehemu fulani mara moja hivyo watakutana baadae , Hivyo T.I.D alibidi amsubiri pale lakini muda ulipita bila Chillah kutokea hivyo kuanza kumtafuta hewani lakini hakupatikana na hivyo akamtafuta mchumba wake lakini mchumba wa q-chillah alisema na yeye hampati hewani hivyo wakaanza kumtafuta bila mafanikio jana ilikuwa ni siku ya pili wameshindwa kumpata na hawajui alipo.
Mchumba wa Q-chilllah alisikikia kupitia radio E-Fm kuwa alibidi apige simu pale aliposema atapita kabla ya kukutana na T.I.D alijibiwa kuwa Q-chillah alichukuliwa na gari fulani hivyo wao hawajui amekwenda wapi na hawana mawasiliano nae tena...
T.I.D anasema ameshatoa taarifa polisi toka jana lakini ameona awajuzi watanzania ili kama kuna mtu anajua Q-chief alipo asaidie kutoa taarifa hata kituo cha polisi ili awezeshe kupatikana kwakwe...
Bado najiuliza
Hivi Q-chief atakuwa amedhurumu?
Hivi Q-chief atakuwa amekula vya watu?
Hivi Q-chief atakuwa amejificha kutafuta kiki?
Hivi Q-chief anapenda ugomvi au ana ugomvi na mtu?
Hivi Q-Chief atakuwa na tabia ya ulevi wa kupindukia?
Hivi Q-chief aatakuwa anafanya biashara ambayo watu wake wa karibu hawafahamu?
Hayo ni maswali tuu nimejiuliza lakini binafsi namuona Q-chief kama mtu mpole na humble sana..
Tuombe Mungu ndugu yetu apatikane akiwa salama.
Wasalaam wana jamvi.
Source: E-fm (ubaoni)
Hivi hajapatikana hadi leo?Kila mtu sikuhizi akiamua kupotea anapotea,.. eg Fatma lamore (yule mtangazaji)
Kwani Mlimani city ni mali ya nani na iligawanywa kwa nani ?Wasiojulikana ni kundi la watu(mafia) waliozuka /wanazuka Tanzania baada ya kukosa marupurupu, mali za magendo, walikuwa wamezoea kula bila kinawa mikono( kama waligawa Airtel, Mlimani City) na kujitajirisha na sasa wamekosa nafasi kama hizo, wanafanya maasi ili raia wa kawaida na waliowaadilifu wachukie serikali ya Dr Rais Magufuli lakini yote haya yatafichuka tu.
Kwani Mlimani city ni mali ya nani na iligawanywa kwa nani ?Wasiojulikana ni kundi la watu(mafia) waliozuka /wanazuka Tanzania baada ya kukosa marupurupu, mali za magendo, walikuwa wamezoea kula bila kinawa mikono( kama waligawa Airtel, Mlimani City) na kujitajirisha na sasa wamekosa nafasi kama hizo, wanafanya maasi ili raia wa kawaida na waliowaadilifu wachukie serikali ya Dr Rais Magufuli lakini yote haya yatafichuka tu.
Hayo aliyaongea aliyekuwa nao huko Dom..Qchillah hakua nae
Mi namuona hapa live kabisa. Mzimaaaaa wala hana hata chembe ya maumivu.Ametekwa na yeye
alipatikana lengo ilikuwa ni kucreate attention ili kipindi chake kipya kitazamwe/kisikilizwe na watuHivi hajapatikana hadi leo?