Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,641
- 11,958
Jaji Kaijage na team yake ya Tume ya uchaguzi kama si busara zao za kukubali kufanya uhakiki wa wadhamini wa mgombea urais Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA Mhe. Tundu Lissu jambo ambalo kikanuni lilipaswa kufanyika kwenye ofisi za majimbo za Tume ya Uchaguzi basi ni dhahiri Lissu alitakiwa kutopitishwa na Tume.
Ajabu ni kwamba Mhe Tundu Lissu hakufanya hivyo iwezekana hakujua ama alijua Ila tu ni kiburi na kutaka kuonyesha umwamba mbele ya Tume ya Uchaguzi. Kikawaida hapa alitakiwa kukatwa moja kwa moja kwasababu tayari ameshavunja kanuni lakini busara za Tume zimembeba.
Mwanasheria makini msomi na mjuaji kama Tundu Lissu unawezaje kuvunja kanuni muhimu kama hii? Je hapo angakuta baadhi ya wadhamini ni hewa ingekuwaje ?
Hii inatoa picha kuwa kuna tatizo kubwa sana kwa hawa wagombea wa CHADEMA kwenye utaratibu wa ujazaji wa fomu za Ubunge na udiwani. Hawa wagombea wa ccm wanao pita bila kupigwa si kwamba ni mchezo mchafu wa CCM bali ni uzembe unao fanywa na wagombea wenyewe wa CHADEMA.
Kama imewezekana kwa Rais mtarajiwa kufanya kosa la kiufundi kama hili kwa wabunge je haitakuwaje?
Kama Lissu angekatwa na Tume asingekuwepo wa kulaumiwa makosa ni yake mwenyewe.
Kisha CHADEMA bila aibu wanakuja kusema hivi
Kibaya zaidi mhe Tundu Lissu bila kujali busara zilizotumiwa na Tume bado ametoa lawama nyingi kuwa kwanini amekalishwa masaa mengi kwenye uhakika wakati mhe Rais Magufuli alitumia muda mchache Kama ilivyopangwa.