Uchaguzi 2020 Hoja binafsi: Jaji Kaijage apongezwe kwa busara zake zilizombeba Tundu Lissu, busara zaidi itumike kuepuka sintofahamu za makusudi kwenye Uchaguzi

Tatizo kubwa hapo ni ujuaji tu mkuu. We unadhani Tume walikuwa wajinga hawajui hiyo sheria hadi wakatoa maelekezo wadhamini wahakikiwe kwenye ofisi za majimbo? Wagombea woote wa vyama vyote kumi nne walikuwa hawajui hiyo sheria Ila ni Lissu tu na CHADEMA ndio wanaojua sana Sheria?
Alafu Kama haitoshi anakuja kulalamika kakarishwa muda mrefu huoni kama ni unafiki huo?

Mkuu penye haki tutetee lakini pia lazima wakati mwingine tuwaambie CHADEMA na Lissu wapunguze ujuaji mwingi.
 
"We unadhani Tume walikuwa wajinga hawajui hiyo sheria".
Mimi sidhani wala sitaki kuamini kwamba tume ni wajinga. Kiongozi tatizo hapa sio maelekezo ya tume, tatizo ni sheria. Maelekezo ya tume yanatakiwa yaendane na sheria, yasipingane na sheria. Je Lissu na CDM walivunja sheria kutokupeleka fomu kwa wasimamizi wa majimbo ya uchaguzi? Je unadhani kama wamevunja sheria tume ingempitisha Lissu? Na kama imempitisha hali amevunja sheria wagombea wengine wangekubali kugombea na mtu aliepitishwa kienyeji bila kufuata sheria?
 
Bila kuwarudisha wagombea wa Upinzani walioondolewa na makada wa ccm ambao wanaitwa Wakurugenzi , mwisho wa Kaijage utakuwa mbaya sana ! atakamatwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…