Hoja kuhusu matapeli wa mtandaoni ambao wakishagundulika hutoa matusi makali

Mimi alinipigia boya mmoja akaniuliza nina TZS ngapi maana kuna pesa imekuaj kimakosa kwangu. Nikamwambia sijui kwani wamenitumia fedha ya malipo ya Korosho kutoka ktk shamba langu huko kijijini. Jamaa akaanza siasa zake eti kuna mtu katuma 280,000/= hivyo nimrejeshee nikambwambia kwa kuwa yeye yupo ktk kampuni achukue mwenyewe tena achukue 300,000/= hapo ndipo mvua ya matusi ikaanza ghafla..
 
Na aligonga?
 
Ile ni hasira ya njaa ndiyo inawafanya wanavurumisha matusi kiasi kile baada ya kugundua mtego wao umefyatuka na huku wakiwa wameshatumia kiasi fulani cha bando au vocha pasipokupata kitu chochote.
 
Magufuli alisema tukisajili kwa finger print hilo tatizo litaisha, mpaka leo bila bila.
 
Mimi huwa wakinipigia nawaambia NENDA KULIMA, JEMBE HALIMTUPI MTU.
 
Makampuni ya simu lazima yawe na namba zinazojulikana ni zao. Mfano namba za 0800 7898990 nk kuzuia utapeli
 
Siku hiyo wamepiga nimepokea nikamwambia akatapeli washamba wenzie. Akaanza nitukania mama angu sikumkawiza na mimi nikamtukana sikujali pembeni kuna nani mpaka akakata simu.
 
Ni wahudumu wa Vodacom hao ndo maana hawataki kublock namba ambazo hazijasajiliwa.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Ulishawahi kujiuliza siku ukienda kutuma fedha kwa wakala anakuambia uandike namba yako kwenye kipande cha karatasi je, disposal ya namba hizo wajua zinafanyikaje?
 
Nami pia yalinikuta haya. Kosa langu ni kumueleza kwamba amekosea namba. Alinishushia mzigo wa matusi naogopa hata kuyaandika hapa.
 
Ni kweli kabisa kuna siku nimetumiwa pesa 750,000 dakika tano zikapita nikapigiwa simu eti wametoka airtel wanataka kunirekebishia kuna vifurushi vipya vya internet akaniaambia nibonyeze *148*88#
Nikabonyeza πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ akaniambia haya sasa umeviona vifurushi sasa nataka nikuunge haya toka ingia *150*60#
Moyoni nikacheka kuwa hii si code ya airtel money πŸ˜‚πŸ˜‚ nikamuambia nibonyeze ngapi. Nakuwa najifanya kaka simsikiii mara namuambia mtandao unasumbua
Mwisho akanitukana huyoo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Baadae tena akaniomba msamaha
 
🀣🀣🀣
 
Mpuuzie tu hawana jipya hakuna wa kumatpeli kwenye simu kipindi hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…