Loading failed
JF-Expert Member
- Sep 14, 2023
- 2,603
- 7,501
Harakari za uumbaji wa mwanadamu kiimani na utata unaojitokeza yapi maswali ya kujiuliza kwa kina. Je nani mwenye majibu yake au nani anaweza kutujibia.
Ndugu zangu.
A) Uumbwaji wa mwanamke na mwanaume bila udogo, tena wenye usawa ndani yake
Tukiangazia kitabu cha mwazo 1: 26-28 tutagundua kwamba Mungu aliumba mwanamume na mwanamke aiku moja bila ya kutumia udogo, tena aliwaumba kwa sura na mfano wake. Mungu aliwabariki pia na kuwapa uwezo wote wawili wa kuzaa. Na zaidi tena walipewa uwezo wa kutawala na kutiisha wote kwa pamoja. Mwanaume alipewa uwezo wa kutawala na kutiisha vivyo hivyo na mwanamke naye alipewa uwezo wa kutawala na kutiisha
NUKUU ( MWAZO 1:26-28)
Mwanzo 1
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
B) Mwazo 2 :5 TUNAONA WALW WALIOUMBWA KWA SURA NA MFANO WA MUNGU HAWAKUWEPO.
Mwanzo 2:5 ..hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;
C) ( Mwazo 2: 7-8, na mwazo 2:15-18) TUNAONA ALIUMBWA MTU KWA MAVUMBI TUSIE IJUA JINSIA YAKE HAPA.
Mwanzo 2
7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
8 Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.
Mwanzo 2
15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
D) Mwazo 2: 19-25 ,UWEPO WA ADAMU TUSIEJUA KATOKA WAPI AMBAPO NDIPO ALIPOTWALIWA MWANAMKE
Mwanzo 2
19 Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.
20 Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.
21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
25 Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.
E) Mwazo 3:6,16-22. UWEPO WA MUME NA MKE TUSIOUJUA ULIKUAJE KUAJE.
Mwanzo 3
6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;
18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
20 Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai.
21 Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.
22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;
***
Ukiunganisha kwa pamoja kitabu cha mwazo 1,2 na 3 katika uumbaji wa mwanadamu utagundua ya fuatayo
a) Kulikua na wanawake wawili yule aleumbwa mwenye usawa na mwanaume na huyu alie umbwa kutoka kwa Adamu
b) Tutagundua kulikua na wanaume wawili yule aliyeumbwa kuwa sawa na mwanamke na huyu Adamu aliyeibuka kusiko julikana
c) Tutagundua kulikua na uumbwaji watu wa tano kama ifuatavyo.
- Mwanaume aliyeumbwa sawa na mwanamke (haki sawa)
-mwanamke aliyeumbwa sawa na mwanaume (haki sawa)
-Mtu aliyeumbwa kwa udongo asiye julikana jinsia yake ni mwanaume au ni mwanamke.
-Adamu ambaye hajulikani alitokea wapi na aliumbwaje na hilo jina Adamu alipata wapi
-Mwanamke aliye umbwa kutoka kwenye ubavu wa Adamu ambaye Adamu alikuja kumuita Hawa huko baadae.
YAPI MASWALI YA KUJIULIZA
1: a) Kwakuzingatia uumbaji wa binadamu kwenye mwazo 1: 26-28, je, tunakiri wazi kuwa mwanaume na mwanamke ni sawa na wote wananguvu za kumiliki na kutawala na wanahaki sawa?
b )Kwanini hawakuanza kuzaliana kama walivyobarikiwa na kuambiwa wazaliane , kama walizaliana watoto wao wako wapi na nikina nani?
2: kwa kuzingatia Mwazo 2 :5
a) wale binadamu waliokua sawa baina ya mwanaume na mwanamke hawakuwepo duniani kwenye kuilima ardhi , je, walikua wapi baada ya kuumbwa?
b) Je, kama hawakua popote ni dhairi kwamba uumbaji wa awali kwenye mwazo 1: 26:28 ulifutwa baada ya kugundua wapo sawa , na kama haukufutwa hao watu ndio hawa tunao waona wadai haki sawa au ni wapi?
3: a) Ukisoma Mwazo 2: 7-8, na mwazo 2:15-18 utagundua aliumbwa mtu ambaye bayana jinsia yake haikutajwa, je huyo mtu yupo wapi na alikwenda wapi?
b) Kama wapo je, ndiyo hawa wanaozaliwa na jinsia zaidi ya moja tunawaona kwenye hii dunia ya sasa?
4: a) ukiangalia Mwazo 2: 19-25 utagundua kuna mtu katajwa kwa jina la ADAMU ambaye hajulikani alitokea wapi, je huyu adamu aliyetumika kutolewa ubavu wake na ndipo akaumbwa mwanamke alitoka wapi na chanzo chake kilikua ni nini na ni wapi?
b) Je, Adamu aliumbwa kutokana na nini basi, na hili jina Adamu alilipata wapi?
C)Kama sio "a" na" b". Je, huyu adamu ndiye yule ambaye kule tuliona Mungu walikua wakiongea na kusema tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu. kama sio yeye ni kwanini adamu aje aonekane sahizi., je, na wale walioumbwa kumtangulia wako wapi?
5: Ukifatilia Mwazo 3:6,16-22. Utagudua kuna swala la huyu mwanamke kumuita mwanume Mume. na baadae kulikuwepo n namna ya kuitan a majina matukufu mume na mke .
maswali ya kujiuliza.
a) Huyu mwanamke ambaye baadae aliitwa na Adamu Kwa jina la Hawa. Je, mume wake aliyempa tunda alikua ni yupi na akipata wapi mamlaka ya kujimilikisha jina "mume wake"?
b) Kama Adamu tokea huko alipoibukia ambako hatujui alitokea wapi, tunajua hakuwahi kusema kama ni mume wa huyo mwanamke ambaye baadae alimuita Hawa, je, kwanini basi Adamu akubaliane baadae kumuita Hawa ni mkewe?
c) Kwanini Adamu asingekataa kwamba yeye siyo mume wa mtu wala hana mke pindi walipo adhibiwa maana hakuna mahali mwenyezi Mungu alimuambia kuwa huyo mwanamke ndiye mke wako, ?
d) i. Je, kama kweli hawa (mwanamke ) alimpa mume wake tunda walilokataza kula. Kwanini huyo mwanamke asinge hojiwa ili aseme wazi huyo mume wake aliyempa tunda pale bustani ya eden ni yupi ili tujue ni Adamu au ni wale walioumbwa kabla ya kuibuka Adamu ambaye hatujui katokea wapi?
ii. Kwanini adamu alipo hojiwa alisema ni huyu mwanamke uliyenipa ila hakusema mke. Je, tutajuaje kuwa Adamu hakua mume wa huyo mwanamke aliyetoa tunda isipo kua aliamua kumsitiri rafiki yake?
6: Je, sisi wanadamu wa sasa nikizazi cha uumbaji ule wa kwanza, wapili au huu wa udongo wa hawa na Adamu asiye julikana. Au ni mchanganyiko wa vizazi vyote na kwanini iwe hivyo.?
KARIBUNI KWA MAJIBU NA HOJA