Hoja na maswali utata kwenye uumbwaji wa mwanadamu katika imani ya Kikristo. Je, wenzetu imani zao zinasemaje?

Hoja na maswali utata kwenye uumbwaji wa mwanadamu katika imani ya Kikristo. Je, wenzetu imani zao zinasemaje?

Tumia akili hapo mungu kafumba tu lugha ...sababu ya mwanamke kuitwa msaidizi ni kwamba mungu akumpa mwanamke AKILI YA UONGOZI hivyo mwanamke kanyimwa akili katika kipengere cha uongozi
Akili ya uongozi haichagui mwanaume au mwanamke mkuu... Mungu aliumba watu wote sawa ila kila mtu alimpa majukumu tofauti na mwenzie...

Kuna wanaume wako na sifa za usaidizi kuliko wake zao na familia za namna hiyo zipo nyingi na wengi mnaziona mtaani utakuta mwanamke anakua juu kuliko mwanaume na kwenye maamuzi mwanaume siku zote anakua mtu wa pili na wala yeye haoni tabu wala haoni kama ananyanyasika ila watu wa nje ambao hawajui haya mambo ndio utawakuta wanalaumu kwamba jamaa anaonewa au mkewe kamtawala ila kiuhalisia wala sio kweli ni vile tu yeye na mkewe hawafanani kisifa.
 
Nani kakudanganya ...kikawaida akili ya uongozi ya mwanaume ipo juu ya mwanamke ndiyo maana ya mwanaume kuitwa kichwa ...kichwa ndiyo kinaongoza mwili wote ...sema wapo wanaume wapumbavu hao ndiyo shida ...mtu mpumbavu ni zaidi ya mtu asiye na akili...hivyo mwanamke japo hana akili ya uongozi ni bora zaidi kuliko mwanaume mpumbavu ...
 
Harakari za uumbaji wa mwanadamu kiimani na utata unaojitokeza yapi maswali ya kujiuliza kwa kina. Je nani mwenye majibu yake au nani anaweza kutujibia.

Ndugu zangu.

A) Uumbwaji wa mwanamke na mwanaume bila udogo, tena wenye usawa ndani yake

Tukiangazia kitabu cha mwazo 1: 26-28 tutagundua kwamba Mungu aliumba mwanamume na mwanamke aiku moja bila ya kutumia udogo, tena aliwaumba kwa sura na mfano wake. Mungu aliwabariki pia na kuwapa uwezo wote wawili wa kuzaa. Na zaidi tena walipewa uwezo wa kutawala na kutiisha wote kwa pamoja. Mwanaume alipewa uwezo wa kutawala na kutiisha vivyo hivyo na mwanamke naye alipewa uwezo wa kutawala na kutiisha

NUKUU ( MWAZO 1:26-28)
Mwanzo 1
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

B) Mwazo 2 :5 TUNAONA WALW WALIOUMBWA KWA SURA NA MFANO WA MUNGU HAWAKUWEPO.

Mwanzo 2:5 ..hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;

C) ( Mwazo 2: 7-8, na mwazo 2:15-18) TUNAONA ALIUMBWA MTU KWA MAVUMBI TUSIE IJUA JINSIA YAKE HAPA.
Mwanzo 2
7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
8 Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.

Mwanzo 2
15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

D) Mwazo 2: 19-25 ,UWEPO WA ADAMU TUSIEJUA KATOKA WAPI AMBAPO NDIPO ALIPOTWALIWA MWANAMKE

Mwanzo 2
19 Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.
20 Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.
21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
25 Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.

E) Mwazo 3:6,16-22. UWEPO WA MUME NA MKE TUSIOUJUA ULIKUAJE KUAJE.

Mwanzo 3
6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;
18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
20 Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai.
21 Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.
22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;

***
Ukiunganisha kwa pamoja kitabu cha mwazo 1,2 na 3 katika uumbaji wa mwanadamu utagundua ya fuatayo
a) Kulikua na wanawake wawili yule aleumbwa mwenye usawa na mwanaume na huyu alie umbwa kutoka kwa Adamu
b) Tutagundua kulikua na wanaume wawili yule aliyeumbwa kuwa sawa na mwanamke na huyu Adamu aliyeibuka kusiko julikana
c) Tutagundua kulikua na uumbwaji watu wa tano kama ifuatavyo.

- Mwanaume aliyeumbwa sawa na mwanamke (haki sawa)

-mwanamke aliyeumbwa sawa na mwanaume (haki sawa)

-Mtu aliyeumbwa kwa udongo asiye julikana jinsia yake ni mwanaume au ni mwanamke.

-Adamu ambaye hajulikani alitokea wapi na aliumbwaje na hilo jina Adamu alipata wapi

-Mwanamke aliye umbwa kutoka kwenye ubavu wa Adamu ambaye Adamu alikuja kumuita Hawa huko baadae.

YAPI MASWALI YA KUJIULIZA

1: a) Kwakuzingatia uumbaji wa binadamu kwenye mwazo 1: 26-28, je, tunakiri wazi kuwa mwanaume na mwanamke ni sawa na wote wananguvu za kumiliki na kutawala na wanahaki sawa?

b )Kwanini hawakuanza kuzaliana kama walivyobarikiwa na kuambiwa wazaliane , kama walizaliana watoto wao wako wapi na nikina nani?

2: kwa kuzingatia Mwazo 2 :5
a) wale binadamu waliokua sawa baina ya mwanaume na mwanamke hawakuwepo duniani kwenye kuilima ardhi , je, walikua wapi baada ya kuumbwa?

b) Je, kama hawakua popote ni dhairi kwamba uumbaji wa awali kwenye mwazo 1: 26:28 ulifutwa baada ya kugundua wapo sawa , na kama haukufutwa hao watu ndio hawa tunao waona wadai haki sawa au ni wapi?

3: a) Ukisoma Mwazo 2: 7-8, na mwazo 2:15-18 utagundua aliumbwa mtu ambaye bayana jinsia yake haikutajwa, je huyo mtu yupo wapi na alikwenda wapi?

b) Kama wapo je, ndiyo hawa wanaozaliwa na jinsia zaidi ya moja tunawaona kwenye hii dunia ya sasa?

4: a) ukiangalia Mwazo 2: 19-25 utagundua kuna mtu katajwa kwa jina la ADAMU ambaye hajulikani alitokea wapi, je huyu adamu aliyetumika kutolewa ubavu wake na ndipo akaumbwa mwanamke alitoka wapi na chanzo chake kilikua ni nini na ni wapi?

b) Je, Adamu aliumbwa kutokana na nini basi, na hili jina Adamu alilipata wapi?

C)Kama sio "a" na" b". Je, huyu adamu ndiye yule ambaye kule tuliona Mungu walikua wakiongea na kusema tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu. kama sio yeye ni kwanini adamu aje aonekane sahizi., je, na wale walioumbwa kumtangulia wako wapi?

5: Ukifatilia Mwazo 3:6,16-22. Utagudua kuna swala la huyu mwanamke kumuita mwanume Mume. na baadae kulikuwepo n namna ya kuitan a majina matukufu mume na mke .

maswali ya kujiuliza.

a) Huyu mwanamke ambaye baadae aliitwa na Adamu Kwa jina la Hawa. Je, mume wake aliyempa tunda alikua ni yupi na akipata wapi mamlaka ya kujimilikisha jina "mume wake"?

b) Kama Adamu tokea huko alipoibukia ambako hatujui alitokea wapi, tunajua hakuwahi kusema kama ni mume wa huyo mwanamke ambaye baadae alimuita Hawa, je, kwanini basi Adamu akubaliane baadae kumuita Hawa ni mkewe?

c) Kwanini Adamu asingekataa kwamba yeye siyo mume wa mtu wala hana mke pindi walipo adhibiwa maana hakuna mahali mwenyezi Mungu alimuambia kuwa huyo mwanamke ndiye mke wako, ?

d) i. Je, kama kweli hawa (mwanamke ) alimpa mume wake tunda walilokataza kula. Kwanini huyo mwanamke asinge hojiwa ili aseme wazi huyo mume wake aliyempa tunda pale bustani ya eden ni yupi ili tujue ni Adamu au ni wale walioumbwa kabla ya kuibuka Adamu ambaye hatujui katokea wapi?

ii. Kwanini adamu alipo hojiwa alisema ni huyu mwanamke uliyenipa ila hakusema mke. Je, tutajuaje kuwa Adamu hakua mume wa huyo mwanamke aliyetoa tunda isipo kua aliamua kumsitiri rafiki yake?

6: Je, sisi wanadamu wa sasa nikizazi cha uumbaji ule wa kwanza, wapili au huu wa udongo wa hawa na Adamu asiye julikana. Au ni mchanganyiko wa vizazi vyote na kwanini iwe hivyo.?

KARIBUNI KWA MAJIBU NA HOJA
Kabla ya kwenda mbali zaidi,kwanza unatakiwa kuelewa tofauti kati ya JINSI NA JINSIA( SEX AND GENDER).

Kibiblia ukidoma soma mwanzo 5,mstari wa kwanza hadi wa pili utapata mwanga na ufahamu zaidi juu ya ulichouliza.

Kisayansi iko wazi kabisa mana hata topic ya reproduction ya kidato cha tatu kwenye baiolojia ilishaeleza kwa kina juu ya kinachokupa mashaka.
Kwa mujibu wa biblia,nanukuu: mwanzo 5: 1-2

"1.Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa."

Ukisoma andiko hili kwa herufi kubwa utagundua kuwa,kwa mara ya kwanza Jina Adamu liliwakilisha JINSI na sio JINSIA.

Ifahamike kuwa kila mwanadamu anajinsi mbili( JINSI YA KIKE NA JINSI YA KIUME) ila JINSIA huwa ni moja tu( MWANAMKE AU MWANAUME) Hapa panahitaji maelezo ya kina ambayo kimsingi ili yaeleweke yatatoka nje ya mada.

Hivyo basi kwa ufupi itoshe kusema tu kuwa hao ambao unadhani walikuwa wawili wawili wala hawakuwa wawili wawili kama unavyodhani bali kilichokuwa kinaongelewa ni swala la JINSI NA JINSIA.
 
Nani kakudanganya ...kikawaida akili ya uongozi ya mwanaume ipo juu ya mwanamke ndiyo maana ya mwanaume kuitwa kichwa ...kichwa ndiyo kinaongoza meili wote ...sema wapo wanaume wapumbavu hao ndiyo shida ...mtu mpumbavu ni zaidi ya mtu asiye na akili...hivyo mwanamke japo hana akili ya uongozi ni bora zaidi kuliko mwanaume mpumbavu ...
Vitu vingi ambavyo watu wengi wanaviamini duniani huwa havipo kama ambavyo wao wanavyoamini vipo, kwasababu dunia imejaa propaganda sana na yote hii nI kuendelea kutengeneza puzzle ambazo zitaendelea kuwafanya watu waendelee kubaki katika eneo la kuelea elea kifikra kila wakati wanapotamani kuujua ukweli.

Kwahiyo hiyo ni imani yako mkuu na ni ngumu sana kumbadilisha mtu kiimani kwasababu imani ni matokeo ya kusikia jambo moja kwa muda mrefu sana na kuliweka akilini kama lilivyo.

Ila nikuhakikishie tu kwamba hizo ambazo unazileta wewe ni propaganda ambazo zilitengenezwa tu but asili ya ulimwengu huwa haibadiliki tangu hapo awali hadi sasa.

Kwa maana ya kwamba jambo lolote ambalo halipo katika misingi ya kiulimwengu haliwezi kutokea hata kwa bahati mbaya na hii ni sheria ambayo haiwezi kuvunjwa na mtu yeyote wa dunia hii.

Kwahiyo hoja yako ingekua kweli hakuna hata sehemu moja ya dunia ungeweza kuona hata kwa bahati mbaya katika mfumo wowote wenye lengo la kuijenga na kuiendesha dunia yupo mwanamke aliyetambulishwa kwenye uongozi na akapata muunganiko wa moja kwa moja na dunia kwasababu ulimwengu huwa unakawaida ya kuvikataa vitu vyote ambavyo vinakwenda kinyume na mfumo wake.
 
Maswali hayana logic ...ni sawa sawa na mtu aseme amepika wali kisha asame tena nimepika mchele kisha aseme tena nimepika mpunga kisha wewe useme ni mkanga nyiko
Hayana logic kutokana na uelewa wako
 
Tumia akili hapo mungu kafumba tu lugha ...sababu ya mwanamke kuitwa msaidizi ni kwamba mungu akumpa mwanamke AKILI YA UONGOZI hivyo mwanamke kanyimwa akili katika kipengere cha uongozi
Mwanamke wa kwanza alipewa nguvu sawa za kiungozi (kutawala) na kutiisha

Mwanzo 1
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
 
Nionyeshe logic ni ipi hapo...yani genius nisione logic wewe kiazi mbatata uweze kuona logic? Nipe logic moja tu nione
Kitendo cha kutumia lugha chafu ya kukashifu kwa kuniita "kiazi mbatata" kinaonyesha wewe ni mjinga, mpumbavu, usiejielewa na unapenda sifa zisizo za stahiki yako kama unavyojisifia wewe ni genius
 
Kitendo cha kutumia lugha chafu ya kukashifu kwa kuniita "kiazi mbatata" kinaonyesha wewe ni mjinga, mpumbavu, usiejielewa na unapenda sifa zisizo za stahiki yako kama unavyojisifia wewe ni genius
True genius
 
Nani kakudanganya ...kikawaida akili ya uongozi ya mwanaume ipo juu ya mwanamke ndiyo maana ya mwanaume kuitwa kichwa ...kichwa ndiyo kinaongoza mwili wote ...sema wapo wanaume wapumbavu hao ndiyo shida ...mtu mpumbavu ni zaidi ya mtu asiye na akili...hivyo mwanamke japo hana akili ya uongozi ni bora zaidi kuliko mwanaume mpumbavu ...
Mwanamke na mwanaume waliumbwa sawa. Tena waliagiza kwa pamoja wakatawale na kutiisha. Maana yake kiutawala, uongozi ni sawa. Ndo maana tunaambiwa tuishi nao kwa akili

Mwanzo 1
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
 
Mwanamke na mwanaume waliumbwa sawa. Tena waliagiza kwa pamoja wakatawale na kutiisha. Maana yake kiutawala, uongozi ni sawa. Ndo maana tunaambiwa tuishi nao kwa akili

Mwanzo 1
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Kasome upya kuhusu huyo huyo mungu anasemaje kuhusu nafasi ya mwanaume na mwanamke kiuongozi baina yao siyo baina ya wanyama wa porini ...mwanamke ni kichwa kwa wanyama pori nk maana amewazidi akili ila siyo kichwa kwa mwanaume
 
Kwa hiyo ushoga unavyo zidi kukubalika unataka kusemaje ...tabia za binadamu zinaweza kubadilika kuelekea AKILI au kubadilika KUELEKEA UPUMBAVU....hivyo kukubali kuongozwa na mwanamke ni upumbavu...
Vitu vingi ambavyo watu wengi wanaviamini duniani huwa havipo kama ambavyo wao wanavyoamini vipo, kwasababu dunia imejaa propaganda sana na yote hii nI kuendelea kutengeneza puzzle ambazo zitaendelea kuwafanya watu waendelee kubaki katika eneo la kuelea elea kifikra kila wakati wanapotamani kuujua ukweli.

Kwahiyo hiyo ni imani yako mkuu na ni ngumu sana kumbadilisha mtu kiimani kwasababu imani ni matokeo ya kusikia jambo moja kwa muda mrefu sana na kuliweka akilini kama lilivyo.

Ila nikuhakikishie tu kwamba hizo ambazo unazileta wewe ni propaganda ambazo zilitengenezwa tu but asili ya ulimwengu huwa haibadiliki tangu hapo awali hadi sasa.

Kwa maana ya kwamba jambo lolote ambalo halipo katika misingi ya kiulimwengu haliwezi kutokea hata kwa bahati mbaya na hii ni sheria ambayo haiwezi kuvunjwa na mtu yeyote wa dunia hii.

Kwahiyo hoja yako ingekua kweli hakuna hata sehemu moja ya dunia ungeweza kuona hata kwa bahati mbaya katika mfumo wowote wenye lengo la kuijenga na kuiendesha dunia yupo mwanamke aliyetambulishwa kwenye uongozi na akapata muunganiko wa moja kwa moja na dunia kwasababu ulimwengu huwa unakawaida ya kuvikataa vitu vyote ambavyo vinakwenda kinyume na mfumo wake.
 
Mungu mmemtunga vichwani mwenu ndio maana mnahangaika kumwelezea.

Mungu alitungwa na watu wa kale tu, Na watu wakaendelea kuaminishana na kukaririshana imani hizo vizazi kwa vizazi.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Ndio maana mnapata tabu sana kuelezea uwepo wake.
 
Kwa hiyo ushoga unavyo zidi kukubalika unataka kusemaje ...tabia za binadamu zinaweza kubadilika kuelekea AKILI au kubadilika KUELEKEA UPUMBAVU....hivyo kukubali kuongozwa na mwanamke ni upumbavu...
Simply ni kwamba shoga ni mwanaume anaetamani kuwa mwanamke lakini sheria ya ulimwengu ni kwamba mwanamke hujifungua ila shoga hajifungui kwasababu mfumo unamkataa kwahiyo mwanaume hata aigize vipi kuwa mwanamke hawezi kuwa mwanamke kwa maana kuna sifa za asili ya uumbaji wa mwanamke atazikosa... anyways.

Na mimi sijazungumzia tabia ila nimezungumzia nguvu nne za asili ya uumbaji wa ulimwengu na ndio ambazo nimezitaja kwenye andiko langu hapo juu na ukituliza akili na kusoma vizuri utaona kuna pahala nimekuwekea msisitizo ya kwamba nguvu mbili ya usaidizi na maono au uwezo wa kutengeneza mawazo yenye tija huwa ni asili ya nani na nani kutokana na uumbaji na ni kwanamna gani hizi nguvu baadae zilikuja kuvurugika na kuanza kutokea kiprobability.
 
Mungu mmemtunga vichwani mwenu ndio maana mnahangaika kumwelezea.

Mungu alitungwa na watu wa kale tu, Na watu wakaendelea kuaminishana na kukaririshana imani hizo vizazi kwa vizazi.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Ndio maana mnapata tabu sana kuelezea uwepo wake.
Mungu ni jina tu ila kiuhakika ni kwamba sisi sio viumbe original wa dunia na ndio maana kila jambo lipo kama puzzle kwa maana ya kwamba yapo mambo ambayo unaweza ukajua mwanzo wake ila mwisho hauwezi kuujua lakini pia yapo mambo ambayo yanajulikana kuanzia hapo yalipo ila mwanzo wake haujulikani.

Na kiuhalisia ni kwamba duniani mambo mengi ambayo yanafanyika ni very basic, it means huu ni upukupuku ambao unapokelewa kutoka somewhere.

Na mabadiliko mengi ambayo yanatokea duniani huwa yanakuja ghafla bila kujua chanzo chake halisi na mfano mzuri ni kwenye hizi language za programming.

Kwamba language zilitumika kutengeneza language zingine sasa language ambayo ilitengeneza language ilitengenezwa na language gani... it's a puzzle ambayo majibu yake huwa ni mepesi mepesi yasiyo ingia akilini.

Kaa katika hali ya utulivu wa akili utagundua kwamba kuna chanzo cha siri cha mambo yote yanayotokea duniani.
 
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo, Hata chanzo cha kila kitu lazima kiwe na chanzo chake kingine.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho exist chenyewe tu pasipo chanzo.
 
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo, Hata chanzo cha kila kitu lazima kiwe na chanzo chake kingine.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho exist chenyewe tu pasipo chanzo.
Nashukuru kwa kujipa jibu... ingawa najua hoja yako ikitoka hapo itakwenda kwenye kutaka kujua chanzo cha huyo kiumbe original ni nini.
 
Nashukuru kwa kujipa jibu... ingawa najua hoja yako ikitoka hapo itakwenda kwenye kutaka kujua chanzo cha huyo kiumbe original ni nini.
Ulimwengu na vyote vilivyomo except man-made things Havina chanzo.

Ni wewe tu unajaribu kufosi Mungu awe chanzo.
 
Ulimwengu na vyote vilivyomo except man-made things Havina chanzo.

Ni wewe tu unajaribu kufosi Mungu awe chanzo.
Kuamini kwamba ulimwengu na vyote vilivyopo havina chanzo ni uvivu wa kufikiri tu.

Nimekutolea mfano mdogo wa hizo language za compyuta na utata uliopo ndani yake ambao unapingana na hoja yako ya kasoro man made things.

Ukiachana na huo mfano lakini pia kuna vitu vingi sana ambavyo vilitokea kwa ghafla sana kuanzia miaka 1950 hapo hadi sasa, ambavyo vilisaidia kuleta mabadiliko makubwa katika maendeleo ya dunia kuliko kipindi cha hapo awali.

Anyway, endelea kukaa katika hali ya utulivu wa akili mara kwa mara kuna siku utakuja kugundua kuna kitu hakiko sawa.

Na siku hiyo utakayojua hilo ndio utakayojua ya kwamba kuna nguvu iliyojificha ambayo ndio inauendesha huu ulimwengu.
 
Kuamini kwamba ulimwengu na vyote vilivyopo havina chanzo ni uvivu wa kufikiri tu.
Kwanza siamini kwenye kuamini.

Sina imani ya aina yeyote ile.

Sihitaji kuamini, Nahitaji kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.

Hakuna uthibitisho wowote ule wa kwamba ulimwengu una chanzo.

Zilizopo ni nadharia za kidini, kihistoria na kisayansi tu zisizo na uthibitisho wowote ule.
Nimekutolea mfano mdogo wa hizo language za compyuta na utata uliopo ndani yake ambao unapingana na hoja yako ya kasoro man made things.
Kwani hiyo computer ilijitengeneza yenyewe ikiwa na hizo languages?

Si ziliwekwa kwenye system ya kompyuta?
Ukiachana na huo mfano lakini pia kuna vitu vingi sana ambavyo vilitokea kwa ghafla sana kuanzia miaka 1950 hapo hadi sasa, ambavyo vilisaidia kuleta mabadiliko makubwa katika maendeleo ya dunia kuliko kipindi cha hapo awali.
Kwani hivyo vitu vilivyo tokea kwa ghafla miaka ya 1950 si vilitengenezwa?

Au viliibuka tu vyenyewe from no where?
Anyway, endelea kukaa katika hali ya utulivu wa akili mara kwa mara kuna siku utakuja kugundua kuna kitu hakiko sawa.

Na siku hiyo utakayojua hilo ndio utakayojua ya kwamba kuna nguvu iliyojificha ambayo ndio inauendesha huu ulimwengu.
Hiyo nguvu unayodai inaendesha ulimwengu haipo, Ni wewe tu unalazimisha na kufosi ionekane ipo.
 
Back
Top Bottom