Hoja: Ushabiki wa mpira wa miguu una asili ya ushetani

Kutokana bado kuna watu wana maswali mengi; kwa faida ya wote na kwa kifupi; nimeweka UPDATES kwenye uzi chini fanyeni kupitia, ili muweze kujuwa kwamba Mpira siyo kusudi la Mungu.
MPIRA UPI. MAZOEZI MECHI AU
AU NDIO YALE UKIMPIGA MTU CHENGA NI DHAMBI YA UONGO
 
Ussienende na wenye mizaha; kama jicho lako linakukosea litoe; hapo yamkini jicho likawa tabia yako mbaya yakupasa uiache kama inakupeleka pa wenye dhambi
 
ULAFI NI KULA NJE YA KIWANGO CHAKO; soma maelezo ya suleimani alipokuwa anaomba baraka za Mungu kuhusu kula, Nitaandaa somo juu ya ulafi subiri
 
Huyu jamaa mwenye post kalazimisha hoja yake watu wamemletea vifungu kwenye bible hadi vya riadha na mieleka amekauka hasemi kitu anaruka ruka tu hapa. Asante sana choosen Generation, Ubarikiwe
 
Ebu pitia kisa cha mfalme suleimani, utaelewa mpira ulivyo laaniwa kuwa si kitu; pia usichanganye maada mashangilio mbele za bwana, Kumbuka tunazungumzia Mpira huu wa kujaza upepo, vile shetani aliugeuza kama mashangilio machoni pake; nimekuwekea upates kwenye uzi kwa ufupi sana ebu tumia kama mwongongozo wakati unapitia
 
We kweli mlokole.. daah..

Kwanza:
Inaonekana unaendeshwa na jazba/mihemuko na mizuka zaidi kuliko reasoning... Infact ni haki yako maana umeamua kuwa mrengo wa kulia

Pili:
Ukisema hivo mambo yenye sura ya mpira yapo mengi sana ambayo hayana makatazo kwenye biblia mojakwamoja.. Nadhani hapa waliotangulia kuchangia wamegusia sana. Mfano unaposema mpira ni wa kishetani Je michezo yote duniani ni ya kishetani au ni mpra tu. Mfano kuna wimbi kubwa la technolojia na ubunifu wa mambo mengi je nayo ni ya kishetani maana hayajaandikwa kwenye biblia.? Vitu vingine uache kuwa wa kiroho sana maana hata Mungu alikupa na akili ili ufanye reasoning..

Unataka kutuambia kila kitu tufanyacho lazima kiwe kimefanyika enzi za biblia? Ina maana akili ulizopewa zinakusaidia nini.. Maana hata wabunifu wa majengo na mabarabara na midoli na maroboti Je nao ni wa kishetani maana hayakusemwa kwenye biblia?

Yako mambo mengi ambayo hayana connection mojakwamoja na yaliyoandikwa ktk biblia ila huwezi sema ni dhambi.

Tatu:
Mistari ya biblia uliyoitoa wala haikatazi mpira ila mihemuko yako tu ndo inahalalisha hivo. Inaonekana una exposure ndogo sana ndo maana nikakwambia una low level of reasoning maana wapo wenzako maustaadh wamerekodihadi na cd kabsa kuelezea ushetani wa mpra, ni bora wao wana fact kidogo kuliko wewe unaeendeshwa na mizuka.

Nne:
Nakushauri uache mizuka na mihemuko +jazba, kaa chini utake zaidi kujifunza mambo mengi. KWA UZOEFU MKUBWA NILIONAO WALOKOLE NI WATU WA KUKURUPUKA NA KUENDESHWA NA MIZUKA NA MIHEMUKO KULIKO KUREASON, nyie mnasema ni ukiroho ila kuna maeneo mnakosea sio ukiroho bali ufinyu wa knowledge na elimu dunia(secular education).

Tano: (Conclusion)
Nakushauri ujifunze zaidi kupitia watu ambao ni great thinkers watakusaidia kuliko kuamka na mawazo yako ambayo hayana hata kilo unaanza kutoa conclusion ya mambo..
 
Watumishi mda mwingine mnakata sana stimu za watu.
 
Huyu jamaa mwenye post kalazimisha hoja yake watu wamemletea vifungu kwenye bible hadi vya riadha na mieleka amekauka hasemi kitu anaruka ruka tu hapa. Asante sana choosen Generation, Ubarikiwe
Hoja zake hajazungumzia mpira, kazungumzia mashangilio, halafu tambua kwamba si kila kitu alicho kitolea mfano basi kiliruhusiwa, vingine vilitumika kama mfano wa kufundishia, Riadha inayozungumziwa kwenye bibilia ni maelezwe yenye taswila yanayo fundisha namna mtu mshindi alivyo, ...biblia imetaja hadi wezi, lakini haijabariki watu kuiba. mfano "Kesheni mukiomba kama akeshavyo mlinzi maana hajui mda wala saa ajayo mwizi.
 

Chukua hoja ya kilicho bora kwenye kila mfano, hapo kwenye kukesha mlinzi ndicho kilicho bora mwizi hapo kaonekana lofa tu

Vile vile kwenye riadha, tumeambiwa tukazana kama aliyeshinda, yaani mshindi wa kwanza. Sasa wewe mwenzetu mbona unataka kujikandamiza tu??
 
Ni ngumu sana kumshauri mlevi kuacha ulevi na akakuelewa kuriko kahaba mtiifu: shetani hutumia kila njia kutetea uovu na pengine kwa marejeo ya mistari lakini nakusihi Pambana,
Shetani alipo mchukua yesu na kumwamulu Ageuze mkate kuwa jiwe, pia shetani huyo huyo alimpereka kwenye mlima akamwonesha fahari ya dunia ili amtumikie lakini Yesu alimjibu..kwahiyo ndugu yangu na wenzako wanaokuunga mkono, Yamkini shetani anatumia kila njia kuwahakikishia kuwa mpira si ushetani, lakini ni vyema kujipa mda ili mpate kweli na kweli itawaweka huru
BARIKIWA.
 
SHETANI ALIPOKUWA anamlaghai Yesu naye alitumia marejeo ya Biblia kumlaghai, lakini maandiko yake hayakuwa na maana machoni pa bwana; haya maneno yako haya bariki mchezo wa mpira, huenda ni utetezi wa Shetani anaoutumia kwa marejeo ya biblia; Mpira wa miguu ni u-free mason uliotukuka mpendwa.
 
Basketball, handball, rugby, netball nk. Wachezaji wanakuwa wangapi, mipira yao haijazwi upepo?, Hawagombei mpira mmoja?, teknolojia uliyotumia kutulisha ujinga wako Ni ya shetani?, kwa sababu yesu hakuwahi kuitumia!. Hongera kwa kuanzisha uzi umepata/utapata wasomaji wengi.
 
Hem tujuze unasali kanisa gani vile..
Ndugu yangu biblia ni pana sana na sizani kama kuna kitabu Complex kama bible, hivyo sijui kama unalijua hili na unalitendea haki.
Maana wewe unaona tafsiri unazozitoa wewe ziko sawa ila wakitafsiri wengine ktk biblia hyohyo wanatumiwa na shetani... daah hatari sana maana ndio tatizo kuu la walokole kuona they are extremely perfectly compared to others bila kujua kuwa wanachokielewa wao sometimes ni very little kulinganisha na hao wanaowadharau
 
Swali tena:
1. Je maarifa kwa nini yasiongezeke kwenye mpira?
2. Ndoa ni ibada, LAKINI ukweli ni kuwa watu wa ndoa wanajiua.

Mkuu hilo swali namba 1 nilitaka kuuliza madhali umeuliza inatosha.
 
Tafuta kitabu cha da vinci code utapata jibu kuhusu mpira na michezo ya jumuia ya madola, olympic vizuur kbsa kitabu hiki unakipata kwa urahisi kama utadownload PDF
 
manabii wauongo hamuishi tu,hata komputa na simu unayotumia ni dhambi kwani inatumikaka kuangalia ngono hakuna ambacho si dhambi inategemea na wewe unakichukuliaje, kama ilivyo kusex ni dhambi ila ukioa ruksa,
 
hoja yako ni nzuri tena inafikirisha nashangaa wako wanaotoa majibu ya jumla ya tena ya kubeza. ila hili halishangazi maana tumetofatiana.

lakini nina swali la nje mada:

dmkali ndilo jina lako halisi? kama sivyo huoni kwamba unamkosea Mungu kwa kuandika jina la uongo?
 
Haya mambo yako peleka Church, huku tuachie mambo yetu. Kila jambo na sehemu yake. ELIMIKA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…