Hoja: Ushabiki wa mpira wa miguu una asili ya ushetani

Haya mambo yako peleka Church, huku tuachie mambo yetu. Kila jambo na sehemu yake. ELIMIKA
biblia ilitabiri kua kizazi hiki hakita taka kuambiiwa ukweli .hapa naona nalithibitisha hilo.mtoa mada kasema ukweli kabisa .kwa kusema kwako naona unayakataa maarifa
 
manabii wauongo hamuishi tu,hata komputa na simu unayotumia ni dhambi kwani inatumikaka kuangalia ngono hakuna ambacho si dhambi inategemea na wewe unakichukuliaje, kama ilivyo kusex ni dhambi ila ukioa ruksa,
Nabii Wa uongo ni wewe ambaye huna ufahamu ktk hili na unayetetea kisa Ushabiki,
BIBILIA IMETOA UFAFANUZI KUHUSU TEKNOLOJIA
kuhusu ujio wa tekinolojia, bibilia imeeleza kwa ufupi sana na kumaanisha makubwa kama ifuatavyo; simu,redio, tv, magari ndege tulizonazo leo hayakuwepo nyakati zao za nyuma.lakin neno moja tu linatolewa kuwa MAARIFA YATAONGEZEKA [DAN 12:4].
 
nyie wasabato acheni kupotosha watu na mafundisho yenu hayo maarifa kuongezeka ni pamoja na mpira wa miguu
 
Soma maandiko mpendwa ili uwe na ufahamu maana bibilia haikuishia hapo; inaendelea Kitabu cha DAN 12:10
Screenshot_2016-07-01-10-57-10.png
 
Soma maandiko mpendwa ili uwe na ufahamu maana bibilia haikuishia hapo; inaendelea Kitabu cha DAN 12:10View attachment 361839

1 John 4:1 - Beloved, believe not every spirit, but try the spirits whether they are of God: because many false prophets are gone out into the world.

2 Peter 2:1 - But there were false prophets also among the people, even as there shall be false teachers among you, who privily shall bring in damnable heresies, even denying the Lord that bought them, and bring upon themselves swift destruction.
 
Duh! Kweli tunatofautiana kufikiri.

Hivi kweli hujui UMUHIMU wa michezo kiakili, kiafya, kimwili na kiroho?

BIBLIA imetoa mifano ya ki mafundisho kwa kutumia MICHEZO. Hii inatuonyesha UMUHIMU wa michezo; Angalia hapa chini;

"Hata mtu akishindana katika MACHEZO hapewi taji, asiposhindana kwa halali." - 2 Timotheo 2:5

Hapa chini tunaambiwa Physical training yafaa kwa afya ya mwili;

Na pia katika kumtafuta Mungu tunapaswa tuige JUHUDI + BIDII kama za wana michezo. Sasa mtu utaniambiaje michezo hasa mpira & riadha ni dhambi?!

"Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye." - 1 Timotheo 4:8

"Je! Hamjui, ya kuwa wale WASHINDANAO kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio NAMNA hiyo, ili mpate. Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika." - 1 Wakorintho 9:24-25

Kitu cha msingi ni kuwa, kila jambo litendeke kwa Uzuri & Utaratibu (1 Kor. 14:40)

Mungu anajua umuhimu MICHEZO & mamshukuru kwani kujihusisha kwangu na michezo kumenijenga kitabia, kimwili & kiimani katika ujana wangu. Nimecheza mpira sana..! Na hata uwezo wa shule ukawa mkubwa tu. Mzazi wangu alituhimiza kushiriki michezo.

MWISHO: Kwa taarifa yako, Mungu alipenda michezo na alijenga tabia ya kuwatembelea wanadamu kule EDENI nyakati za jioni (Asomaye na afahamu).

Pia, alicheza MIELEKA na Yakobo usiku kule Betheli.

"Yakobo akakaa peke yake; na mtu (sio mwanadamu) mmoja akashindana naye MWELEKA hata alfajiri..." - Mwanzo 32:24
unasali wapi nikufuate? mleta uzi kichwani kumejaa mihemko kama ya serikali ya Tasmania
 
1 John 4:1 - Beloved, believe not every spirit, but try the spirits whether they are of God: because many false prophets are gone out into the world.

2 Peter 2:1 - But there were false prophets also among the people, even as there shall be false teachers among you, who privily shall bring in damnable heresies, even denying the Lord that bought them, and bring upon themselves swift destruction.
Pole sana Kwa kujifariji na andiko hilo ilimradi tu uhalalishe huo ufree mason
 
biblia ilitabiri kua kizazi hiki hakita taka kuambiiwa ukweli .hapa naona nalithibitisha hilo.mtoa mada kasema ukweli kabisa .kwa kusema kwako naona unayakataa maarifa
ELIMIKA
 
Kama tulivyoona tafakari pale mwanzo, hivi wawezaje shabikia watu kufukuza mpira na ukawa na midadi na ushabiki wa juu kabisa hadi kufikia kujinyonga endapo Timu yako imefungwa pasipo misingi ya ushetani? “ Ni rahisi sana mtu kufa kwa ushabiki wa mpira wa miguu kuliko kufa kwa kumtetea Mungu wake”, “Ni rahisi sana kukesha unaangalia mpira au mapambano ya ngumi kuliko kukesha ukiswali /kusali katika mkesha'', PIA "Ni rahisi sana kutoa ofa ya mpira kwa mashabiki kuliko kutoa futari mwezi mtukufu",
Yaani wewe unaweza kumtetea Mungu?

Well, kwa ninavyomjua Mungu, mimi siwezi kuwa mtetezi wake...yeye ndie mtetezi wangu. Muumba wa mbingu na nchi na kila ukionacho ndani yake. Sasa kama itafikia nimtetee, basi sidhani uMungu wake uko sawa tena.

Umetumia muda mwingi sana kueleza utumbo na mambo irrelevant. Kama hatuchezi mpira kwa kuwa Yesu hakucheza mpira, basi nifafanulie wapi ulimuona Yesu akilima, akifyatua matofali, akitoa photocopy, akipiga selfie na kadhalika.

Hizi mada zingine zilifaa kuwa chit-chat
 
biblia ilitabiri kua kizazi hiki hakita taka kuambiiwa ukweli .hapa naona nalithibitisha hilo.mtoa mada kasema ukweli kabisa .kwa kusema kwako naona unayakataa maarifa
Yaani hizi pumba ndio ukweli? Wewe wa wapi?
 
Watu wengi hawatakuelewa, lkn mimi binafsi huwa naona mpira ni pumbazo la shetani kwa wanaadamu. Mtu yupo tayari alie, ajinyonge, asisali, asitoe sadaka ila aangalie mpira. Kitu kinachoteka akili ya mwanadamu kabisa na kumsahaulisha na Mwenyezi MUNGU mara nyingi kina ubatili. Ukweli ni kuwa wengi hawatakuelewa kwakuwa wengi ni mashabiki wa mpira. Ni wachache sana wapo tayari kuamka usiku kwa ajili ya kusali lakini ni wengi mno watakesha usiku wa manane kuangalia mpira na kamwe hawapo tayari kusali. Watu wanalipia vifurushi vya bei kubwa kuangalia mpira kila mwezi, jirani yake analala na njaa mara kwa mara!! Ni ajabu kuwa shabiki wa mpira ni kama unatekwa akili. Namshukuru Mwenyezi MUNGU kaniokoa na mpira na muziki hakika humo shetani anafanya kazi kubwa mno ya kupotosha watu.
 
Mungu aliifanya hekima ya dunia hii kuwa ni ubatili mtupu nikisema nielimike kwa jinsi unavomaanisha wewe itakua ni kama kujilisha upepo ... kumcha bwana ni chanzo cha maarifa bali wapumbavu hudharau hekima na adabu
 
Habari zenu enyi watu wa Mungu vs Wapenda soka jf. Uzi huu unagusa neon la Mungu na mambo ya Mpira ndio maana nimeuweka hapa jukwaa la hoja mchanganyiko.

Kwakweli nianze kwa kutafakarisha kidogo; Hivi kama binadamu wote duniani tungekuwa hatuja wahi kuona mpira wa miguu kabisa tangu kuzaliwa kwetu, ikatokea siku ukapelekwa katika sayali ukakuta kuna mechi watu wanacheza mpira, Ungewaelewaje?” Yamkini pengine ungewaona kama wamechanganyikiwa kwamba mibaba mikubwa inafukuza mpira kama kuku wa kienyeji halafu, na huenda waweza hata ukaukamata na kuwaambia kinachowasumbua hiki hapa Tulieni;

Historia ya mpira wa miguu kwa ufupi;

Hiki tunachokiita mchezo wa mpira wa miguu si kitu cha zamani kama wengine wanavyofikiria.ebu tuangalie historia fupi ya mchezo huu ndipo nitakueleza kwa nini mpira ni dhambi. Huko zamani kile walichokuwa wanakiita mpira hakikuwa
hivyo kwa sheria tulizo nazo kwa namna ya sasa.kitu hichi kinachoitwa mpira kilianza mwaka 1863 mwezi 10,walikuwepo watu kadhaa waliotoka katika shule kadhaa uingereza na club chache zilizokuwapo hapo,wakawa wamewakilisha vikundi11 na ndio wakakusanyika mwezi 10,1863 na kuanza kutunga sheria za kupatana za mchezo

Hawa ndio waliosababisha kiundwe chama cha mpira ambacho kinaitwa FA (FOOTBALL ASSOCIATION) cha England mwaka huu 1863 ambao ni mwaka wa karibun sana Baada ya Kristo.

JE; UNATAMBUA KUWA USHABIKI WA MPIRA NI KUSHABIKIA SHETANI?

Kama tulivyoona tafakari pale mwanzo, hivi wawezaje shabikia watu kufukuza mpira na ukawa na midadi na ushabiki wa juu kabisa hadi kufikia kujinyonga endapo Timu yako imefungwa pasipo misingi ya ushetani? “ Ni rahisi sana mtu kufa kwa ushabiki wa mpira wa miguu kuliko kufa kwa kumtetea Mungu wake”, “Ni rahisi sana kukesha unaangalia mpira au mapambano ya ngumi kuliko kukesha ukiswali /kusali katika mkesha'', PIA "Ni rahisi sana kutoa ofa ya mpira kwa mashabiki kuliko kutoa futari mwezi mtukufu",

BIBLIA INASEMAJE?

Ili kuweza kujua vitu kama hivi, tunatakiwa tuangalie kanuni.MUNGU ameweka kanuni ambazo zinatuongoza kupata ufahamu mapenzi ya MUNGU kwa kila jambo.

Pale ambapo jambo halijatajwa moja kwa moja, kanuni hizi zinaweza zikatuongoza

Yako maandiko kadha wa kadha ambayo yanaweza kutuongoza katika kujua mapenzi ya MUNGU katika mipira hii.

1) (WAKOLOSAI 3:17) “KILA MFANYALO KWA NENO AU KWA TENDO, FANYENI LOTE KWA JINA LA BWANA YESU NA KUMSHUKURU MUNGU BABA“Ni muhimu kuelewa ndani yetu tuliokoka kuna mafuta au tuna dhamiri ambayo inatufundisha kujua mema na mabaya (1PET2:26-27).Hata kama jambo hatujajifunza kwa undani juu ya jambo fulani,ndani yetu kutakuwepo roho mtakatifu akitufundisha kuwa hapa siyo na hapa ndiyo.

Sasa kila tunalolifanya kwa neno au kwa tendo, anasema tulifanye hayo yote kwa kufungua kwamaombi.sasa kutokan na mafuta ndani yetu JE TUNAWEZA KUFUNGUA MECHI YA MPIRA KWA KUSHUKURU BABA KWA MAOMBI?
Utaona ndani yetu inakataa.

2.) (YOHANA 5:19) “MWANA HAWEZI KUTENDA NENO MWENYEWE ISIPOKUWA AMEMUONA BABA

ANALITENDA”.
(YOH 14:6-9) Hivyo hatuna budi kujiuliza kutokana na maisha ya YESU, JE INAWEZEKANA YESU AKAWA ANACHEZA MPIRA? YESU KASHIKA MPIRA, MARA BEKi FULANI KAMKATA MTAMA AU TIMU YA YESU IMEPIGWA MAGOLI 6-0? kama dhamiri inakataa kuwa YESU hawezi kufanya hvyo na sisi hatuwezi kufanya hvyo.Tunatenda neno ambalo YESU anaweza kulitenda.

3) Mashabiki wengi wa jambo hilo,vinara wa jambo hilo ,JE NI MATAIFA?Kama wanaongoza ni mataifa,basi nyuma ya jambo hilo kuna mashetani (UFUNUO 18:2-3,23). Mataifa yote yanapokuwa wanachukuliwa hivyo katika jambo hilo, ndio vinara, mashabiki, kwa namna hiyo hiyo uchawi unavyotajwa lazima tujue kuna roho za mashetani.ukiona vinara au viongozi ndio waasherati au walevi,wavuta bangi.

Hawa wanaotajwa washauri wa mambo ya kifundi katika timu hizo ndio wachawi wa timu

watakatifu wa kanisa la kwanza walilijua vema jambo hili na kutokana na jinsi walivyokuwa wakamilifu hawakushiriki katika michezo na walichukiwa na jamii iliyowazunguka kwasababu walionekana “washamba” haya ni maelezo kuhusu watakatifu wa kanisa la kwanza” The Christians were charged with being unsocial and came to be hated and counted as enemies of societies, they were simple and modest in dress, strictly moral in their conduct and would not go to the games and feast “maneno haya yanapatikana katika biblia iitwayo THOMPSON CHAIN REFERENCE BIBLE(NIV)”

MWISHO;

Misingi ya ushetani pekee ndiyo inayo ufanya ushabiki wa mpira uwe na nguvu na kushangiliwa na mataifa;

Ni rahisi sana kutoa ofa ya mpira kwa mshabiki na ukashangliwa kuliko kusaidia masikini wanaoteseka na adha ya dunia hii ukasifiwa, Huu mwezi mtukufu”Ni heri mtu Yule atoae sadaka na kufutulisha wanyonge kuliko anaetumia milioni za fedha kufadhili mpira kwa dk 90 tu ..yamkini huenda ndiyo maana juzi ile timu ilifungwa chanzo kikawa ni hiki (washabiki kumladhi)
View attachment 361495

Mungu awaongoze msiwe na jaziba kuchangia, maana Jazba ni mizizi ya dhambi!
Karibuni!

UPDATES
Kwa wale wanakumbuka kisa cha mfalume suleimani hapo utagundua ndipo mpira siyo kusudi la Mungu;
1. ukisoma hiki kisa vizuri utagundua kile kisa cha mfalme suleiman na taranta za dhahabu 666 na zilivyopokwa na mpinga kristo,ambapo makombe ya dunia ya mpira yanaandaliwa kwa dhahabu,
2. ukiendelea kusoma vizuri utaona kuwa mfalme suleimani akawa kaulaani upepo, na alisema pia pamoja na utajiri wote huu ni sawa na kujilisha upepo, hilo neno upepo, lilikuwa na maana ya bure kabisa, na baada ya hapo kilitengenezwa kitu mithili ya mpira kikajazwa upepo ili kuzihilisha u-bure huo usiofaa machoni pa Mungu...HUO UPEPO ndio unaojazwa mipira hadi leo na kukimbizwa kwa kulenga magoli
3. kile kitufe mithili ya mpira chenye upepo, kilichezwa kwa kulenga ktk ya milingoti miwili mithili ya magoli na kushangiliwa na kerubi akiwa ndiyo mwamuzi REFA.
4. wanafunzi wa yesu walikuwa 12, ukiondoa yule mmoja YUDA, walibaki 11 wenye Haki- hao 11 ndio waliofungwa nira za kriso, Lakini shetani hapo Kageuza, kwa kuweka wachezaji 11 katika team ya mpira, jiulize kwanini asingeweka 15? hao kumi na moja ndiyo wanaoshindana na kufungwa kwa mchezo wa kulenga ktk ya milingoti (magoli)
5. Katika mchezo shetani ndipo alipouteka ulimwengu kwa kugeuza ahadi za Mungu;
Ukisoma bibilia Mungu kasema "Nitabariki kazi ya mkono yenu" lakini hapo shetani akageuza, wacheza mpira ndiyo wanaolipwa pesa ndefu zaidi kwa mda mfupi sana..maanake Hapo shetani aligeuza baraka za mikono kuwa za miguu (Agano la mapinduzi);Kama vile kule bustani ya edeni nyoka alivyogeuza.
BARIKIWA!
kwa maana hiyo vitu vingi vinavyofanyika duniani kwa sasa ni ushetani mfano,muziki ,movies,technlogy na hivyo basi kila mtu anamshabikia shetani.Nani anaikwepa technology? leo hii unainjoy na smart yako ,computa,huduma za mawasiliano nazo,au unasemajejuu ya hilo
 
Habari zenu enyi watu wa Mungu vs Wapenda soka jf. Uzi huu unagusa neon la Mungu na mambo ya Mpira ndio maana nimeuweka hapa jukwaa la hoja mchanganyiko.

Kwakweli nianze kwa kutafakarisha kidogo; Hivi kama binadamu wote duniani tungekuwa hatuja wahi kuona mpira wa miguu kabisa tangu kuzaliwa kwetu, ikatokea siku ukapelekwa katika sayali ukakuta kuna mechi watu wanacheza mpira, Ungewaelewaje?” Yamkini pengine ungewaona kama wamechanganyikiwa kwamba mibaba mikubwa inafukuza mpira kama kuku wa kienyeji halafu, na huenda waweza hata ukaukamata na kuwaambia kinachowasumbua hiki hapa Tulieni;

Historia ya mpira wa miguu kwa ufupi;

Hiki tunachokiita mchezo wa mpira wa miguu si kitu cha zamani kama wengine wanavyofikiria.ebu tuangalie historia fupi ya mchezo huu ndipo nitakueleza kwa nini mpira ni dhambi. Huko zamani kile walichokuwa wanakiita mpira hakikuwa hivyo kwa sheria tulizo nazo kwa namna ya sasa.kitu hichi kinachoitwa mpira kilianza mwaka 1863 mwezi 10,walikuwepo watu kadhaa waliotoka katika shule kadhaa uingereza na club chache zilizokuwapo hapo,wakawa wamewakilisha vikundi11 na ndio wakakusanyika mwezi 10,1863 na kuanza kutunga sheria za kupatana za mchezo

Hawa ndio waliosababisha kiundwe chama cha mpira ambacho kinaitwa FA (FOOTBALL ASSOCIATION) cha England mwaka huu 1863 ambao ni mwaka wa karibun sana Baada ya Kristo.

JE; UNATAMBUA KUWA USHABIKI WA MPIRA NI KUSHABIKIA SHETANI?

Kama tulivyoona tafakari pale mwanzo, hivi wawezaje shabikia watu kufukuza mpira na ukawa na midadi na ushabiki wa juu kabisa hadi kufikia kujinyonga endapo Timu yako imefungwa pasipo misingi ya ushetani? “ Ni rahisi sana mtu kufa kwa ushabiki wa mpira wa miguu kuliko kufa kwa kumtetea Mungu wake”, “Ni rahisi sana kukesha unaangalia mpira au mapambano ya ngumi kuliko kukesha ukiswali /kusali katika mkesha'', PIA "Ni rahisi sana kutoa ofa ya mpira kwa mashabiki kuliko kutoa futari mwezi mtukufu",

BIBLIA INASEMAJE?

Ili kuweza kujua vitu kama hivi, tunatakiwa tuangalie kanuni.MUNGU ameweka kanuni ambazo zinatuongoza kupata ufahamu mapenzi ya MUNGU kwa kila jambo.

Pale ambapo jambo halijatajwa moja kwa moja, kanuni hizi zinaweza zikatuongoza

Yako maandiko kadha wa kadha ambayo yanaweza kutuongoza katika kujua mapenzi ya MUNGU katika mipira hii.

1) (WAKOLOSAI 3:17) “KILA MFANYALO KWA NENO AU KWA TENDO, FANYENI LOTE KWA JINA LA BWANA YESU NA KUMSHUKURU MUNGU BABA“Ni muhimu kuelewa ndani yetu tuliokoka kuna mafuta au tuna dhamiri ambayo inatufundisha kujua mema na mabaya (1PET2:26-27).Hata kama jambo hatujajifunza kwa undani juu ya jambo fulani,ndani yetu kutakuwepo roho mtakatifu akitufundisha kuwa hapa siyo na hapa ndiyo.

Sasa kila tunalolifanya kwa neno au kwa tendo, anasema tulifanye hayo yote kwa kufungua kwamaombi.sasa kutokan na mafuta ndani yetu JE TUNAWEZA KUFUNGUA MECHI YA MPIRA KWA KUSHUKURU BABA KWA MAOMBI? Utaona ndani yetu inakataa.

2.) (YOHANA 5:19) “MWANA HAWEZI KUTENDA NENO MWENYEWE ISIPOKUWA AMEMUONA BABA ANALITENDA”. (YOH 14:6-9) Hivyo hatuna budi kujiuliza kutokana na maisha ya YESU, JE INAWEZEKANA YESU AKAWA ANACHEZA MPIRA? YESU KASHIKA MPIRA, MARA BEKi FULANI KAMKATA MTAMA AU TIMU YA YESU IMEPIGWA MAGOLI 6-0? kama dhamiri inakataa kuwa YESU hawezi kufanya hvyo na sisi hatuwezi kufanya hvyo.Tunatenda neno ambalo YESU anaweza kulitenda.

3) Mashabiki wengi wa jambo hilo,vinara wa jambo hilo ,JE NI MATAIFA?Kama wanaongoza ni mataifa,basi nyuma ya jambo hilo kuna mashetani (UFUNUO 18:2-3,23). Mataifa yote yanapokuwa wanachukuliwa hivyo katika jambo hilo, ndio vinara, mashabiki, kwa namna hiyo hiyo uchawi unavyotajwa lazima tujue kuna roho za mashetani.ukiona vinara au viongozi ndio waasherati au walevi,wavuta bangi.

Hawa wanaotajwa washauri wa mambo ya kifundi katika timu hizo ndio wachawi wa timu

watakatifu wa kanisa la kwanza walilijua vema jambo hili na kutokana na jinsi walivyokuwa wakamilifu hawakushiriki katika michezo na walichukiwa na jamii iliyowazunguka kwasababu walionekana “washamba” haya ni maelezo kuhusu watakatifu wa kanisa la kwanza” The Christians were charged with being unsocial and came to be hated and counted as enemies of societies, they were simple and modest in dress, strictly moral in their conduct and would not go to the games and feast “maneno haya yanapatikana katika biblia iitwayo THOMPSON CHAIN REFERENCE BIBLE(NIV)”

MWISHO;

Misingi ya ushetani pekee ndiyo inayo ufanya ushabiki wa mpira uwe na nguvu na kushangiliwa na mataifa;

Ni rahisi sana kutoa ofa ya mpira kwa mshabiki na ukashangliwa kuliko kusaidia masikini wanaoteseka na adha ya dunia hii ukasifiwa, Huu mwezi mtukufu”Ni heri mtu Yule atoae sadaka na kufutulisha wanyonge kuliko anaetumia milioni za fedha kufadhili mpira kwa dk 90 tu ..yamkini huenda ndiyo maana juzi ile timu ilifungwa chanzo kikawa ni hiki (washabiki kumladhi)
View attachment 361495

Mungu awaongoze msiwe na jaziba kuchangia, maana Jazba ni mizizi ya dhambi!
Karibuni!

UPDATES
Kwa wale wanakumbuka kisa cha mfalume suleimani hapo utagundua ndipo mpira siyo kusudi la Mungu;
1. ukisoma hiki kisa vizuri utagundua kile kisa cha mfalme suleiman na taranta za dhahabu 666 na zilivyopokwa na mpinga kristo,ambapo makombe ya dunia ya mpira yanaandaliwa kwa dhahabu,
2. ukiendelea kusoma vizuri utaona kuwa mfalme suleimani akawa kaulaani upepo, na alisema pia pamoja na utajiri wote huu ni sawa na kujilisha upepo, hilo neno upepo, lilikuwa na maana ya bure kabisa, na baada ya hapo kilitengenezwa kitu mithili ya mpira kikajazwa upepo ili kuzihilisha u-bure huo usiofaa machoni pa Mungu...HUO UPEPO ndio unaojazwa mipira hadi leo na kukimbizwa kwa kulenga magoli
3. kile kitufe mithili ya mpira chenye upepo, kilichezwa kwa kulenga ktk ya milingoti miwili mithili ya magoli na kushangiliwa na kerubi akiwa ndiyo mwamuzi REFA.
4. wanafunzi wa yesu walikuwa 12, ukiondoa yule mmoja YUDA, walibaki 11 wenye Haki- hao 11 ndio waliofungwa nira za kriso, Lakini shetani hapo Kageuza, kwa kuweka wachezaji 11 katika team ya mpira, jiulize kwanini asingeweka 15? hao kumi na moja ndiyo wanaoshindana na kufungwa kwa mchezo wa kulenga ktk ya milingoti (magoli)
5. Katika mchezo shetani ndipo alipouteka ulimwengu kwa kugeuza ahadi za Mungu;
Ukisoma bibilia Mungu kasema "Nitabariki kazi ya mkono yenu" lakini hapo shetani akageuza, wacheza mpira ndiyo wanaolipwa pesa ndefu zaidi kwa mda mfupi sana..maanake Hapo shetani aligeuza baraka za mikono kuwa za miguu (Agano la mapinduzi);Kama vile kule bustani ya edeni nyoka alivyogeuza.
BARIKIWA!

Shetani ni nan?? Anaishi WAP?? Nan alimtengeneza shetan?? Na kwann alimtengeza amuache shetani asumbue watu kwann asimuangamize???
 
Bas ht simu ni u shetani Je mda unatumia kutumia simu unazidi mda wa ibada?
 
biblia ilitabiri kua kizazi hiki hakita taka kuambiiwa ukweli .hapa naona nalithibitisha hilo.mtoa mada kasema ukweli kabisa .kwa kusema kwako naona unayakataa maarifa

Wapi yesu katumia simu, kopyuta, wap yesu katumia jf
 
Hoja zake hajazungumzia mpira, kazungumzia mashangilio, halafu tambua kwamba si kila kitu alicho kitolea mfano basi kiliruhusiwa, vingine vilitumika kama mfano wa kufundishia, Riadha inayozungumziwa kwenye bibilia ni maelezwe yenye taswila yanayo fundisha namna mtu mshindi alivyo, ...biblia imetaja hadi wezi, lakini haijabariki watu kuiba. mfano "Kesheni mukiomba kama akeshavyo mlinzi maana hajui mda wala saa ajayo mwizi.

WAP yesu kasema uchat jf?
 
Kutokana bado kuna watu wana maswali mengi; kwa faida ya wote na kwa kifupi; nimeweka UPDATES kwenye uzi chini fanyeni kupitia, ili muweze kujuwa kwamba Mpira siyo kusudi la Mungu.

Bac Hata ww mwenyew co kusudio la mungu
 
Back
Top Bottom