Hoja: Ushabiki wa mpira wa miguu una asili ya ushetani


Katavi nimeanza kuufahamu mpira miaka ya 90+ taratibu miaka ya 2000+ ndo ulianza kuwa damuni. Nilikuwa mfuatiliaji mzuri sana wa ligi za nyumbani na barani ulaya sambamba na timu shiriki za mataifa mbalimbali.... Nilikuwa shabiki mzuri sana nisiekosa mechi yoyote ya timu yangu xxxx barani ulaya. Ushabiki huo ulinifanya wakati mwingi kuchelewa kurudi nyumbani hasa ukizingatia mara nyingi mpira huchezwa jioni mpaka usiku.... Baadae ilitokea fununu tu kama hizi ikiuhusisha mpira na masuala ya kishirikina, aah nilichukulia poa tu kwani mbona hata biashara nyingi zinaendeshwa hivyoo! Ila baadae ilibidi nitafute ukweli kuhusu hili. Baadae nilipata jawabu kuwa aisee ni kweli timu nyingi sana hasa hizi kubwakubwa zinashiriki kwa namna moja ama nyingine na masuala ya kichawi. Sikushauri uache kushabikia timu yako NO! Endelea mpaka na wewe utakapo gundua kitu.... narudia tena si rahisi ila ni kwa wale watakao weza tu! Nawasilisha Mr. Katavi
 
mkuu jaribu kutofautisha kati ya binadamu na Watanzania.
 
Haya mleta hoja.... achana na mpira fanya mambo mengine

Tuache na hobbies zetu

Mada nyingine ni za kipumbavu sana
 
Mpira kwa ujumla katika ulimwengu wa kiroho ni jambo limekaa kimafumbo sana na linapoteza muda kwa MTU badala ya kuutafuta uso wa Mungu wako bize na football
 
Mpira kwa ujumla katika ulimwengu wa kiroho ni jambo limekaa kimafumbo sana na linapoteza muda kwa MTU badala ya kuutafuta uso wa Mungu wako bize na football
umeona eeh
 
Reactions: Sax
Kama ingewezekana ningegonga like hata 100, mtoa mada KICHWA CHAKE KINAPITISHA UPEPO
 
Nimekusoma! Maswali kidogo:

1. Watu wenye ndoa wengine wanajiua, je Ndoa ni ushetani?
2. Yesu hakucheza mpira, je simu, gari kompyuta yesu hakuvitumia, je kuwa navyo ni ushetani
Swali lako la kwanza na mimi nilitaka nikuulize. Asante kwa kuuliza.

Swali 2. Je ingekuwa duniani watu hawajawahi kuona tendo la ndoa (narudia, TENDO LA NDOA) likifanyika. Na ghafla Wakapelekwa sayari nyingine na kuona tendo la la ndoa likifanyika, hawatacheka sana au kushangaa sana?

Au watu wa ulimwengu huu ingekuwa hatujawahi kuabudu (kwa dini zote) halafu ghafla tupelekwe sayari nyingine tukute watu wanaimba, wanainama, wanapiga Magoti, wanalia....je tusingewashangaa na pengine kucheka sana?

Swali 3. Dhahabu ni dhambi, katika maandiko kuna sehemu inataja vipande vya Dhahabu kama sadaka, je sadaka ya Dhahabu ni dhambi?
 
Unaupungufu, wa kufaham, falsafa ya dini, na falsafa ya dunia..
Kwa ufup falafa ya dini, imo, ndani, ya falsafa ya dunia..
Kitu ambacho, nimekuona hukijui, na kitakusumbua sana maishan mwako, ni, namna ya kutenganisha mambo, ya dini(imani), na mambo, ya kawaida. Si, kweli, biblia inatoa mwongozo wa kila kitu, maishani, ukweli, ni, kuwa Mungu, alitupa akili, ili, yuweze kuzitumia kufanya ugunduzi wa vipaji, mbalimbali, na tafiti, mbalimbali.
Sasa kama ni, hvyo, sema bas kuwa hata elimu, tunayosoma ni, dhambi maana biblia haikusema tusome
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…