Hoja: Utaratibu wa Mahari unatakiwa ufutwe, jamii ibadilike...!!

Hoja: Utaratibu wa Mahari unatakiwa ufutwe, jamii ibadilike...!!

Heri ya Sabato, poleni na mfungo ndugu zetu waislam na wakristo mnaotimiza agizo hili la kiimani.

Nimeamua kudandia treni ya wanaokataa mambo ya mahari kwa dunia ya sasa, hasa barani Afrika ambapo kwa asilimia kubwa ndipo haya mambo hufanyika

Dunia ambayo mwanamke amekuwa huru sana, anaweza kuamua namna anavyotaka maisha yake yawe bila upande wowote kujali/kuingilia.
●Sio dunia ya kulipana pesa/mali kwa ajili ya kumuoa na kuishi nae tena.
●Sio dunia ya kuamuliwa nani utamuoa au utaolewa nae.
● Sio dunia ya kuambiwa ukajenge nje ya boma la wazazi tena, SIO.
● Ni dunia ya kukutana wawili na kuamua hatma ya maisha yenu bila kuingiliwa na mtu yoyote.

Dunia ya namna hii inatakiwa impunguzie mwanaume mzigo, hasa kwenye mambo ya lobola, mahari, dowry.
●Uhuru uliopitiliza kwa mwanamke umekuja na athari hasi, anaweza kuwa na msururu wa wanaume na hakuna anayehoji.
●Anaweza kuamua nani wa kumuoa na hakuna mtu wa kupinga.
●Kwa nini ulipe gharama kubwa kwa kitu ambacho kiimani wewe sio mmliki? Mtu alishamalizana na wanaume kumi+, mmekutana tu for the sake of establishing a society, kwa nini uwe obliged kutoa mapesa ili tu uishi nae?

Wanawake wa sasa wengi ni viwembe, haya mambo tuliyazoea miaka hiyo kwa vijana wa kiume, ila kwa sasa mdada anaweza kuwa na wanaume hata watano kwa wakati mmoja na wala hajali. Mtu wa namna hiyo akikutana na mwanaume kwa ajili ya kutulia(settling) kuna haja gani ya kulipa dowry kama sio kumdhulumu huyo kijana.

Jamii inatakiwa kufikiri mara mbili, tumeamua kuiga tamaduni za wazungu huko, basi na hii iingizwe taratibu kwenye jamii zetu.

Tuachane na hizi mambo.
Happy day y'all!!
Mahari sio hoja ya jumla ni UTARATIBU WA kiutamaduni HUWEZI kuufuta kinachoweza futwa kirahisi ni mila
 
Haijawahi kubadilisha kitu, ila muktadha wake ndo haupo tena.

Sasa hivi huwezi kujua nani kajitunza na nani hajajitunza.
Hakuna tatizo wanawake kufanya ngono, acheni ujima, muhimu watumie condoms tu wafanye mapenzi vizuri na wao wapate raha. Hayo mambo ya kujitunza na kutojitunza ni ujima wa wanaume ku control.
 
Kwamba kuna mtu hatafuti pesa na wewe upo kumlisha mkuu? Swala la kutafuta pesa ni mtambuka, kila mtu kwa namna yake anatafuta pesa mzee.

Elewa hoja, naongelea maadili zaidi ya materials!! Vijana wajitunze ili mahari yalipwe, huwezi kumlazimisha kijana kulipa mahari kwa binti aliyeharibiwa na wanaume double digits, sijui hata kama unaelewa!!
Ni risk kubwa watu kuoana kabla hawajaishi pamoja kwa muda, kujitunza na maadili ni porojo za watu wa dini, watu wazingatie condom tu wasomane kwanza.
 
We're getting free meals everyday wewe unasema no free lunch?
Free lunch wanapewa vijana wa mtaani halafu anakuja kijana anataka kusettle eti alipe 5m ili aoe mwanamke aliyetumika na wanaume wa kutosha.
Acha kutumia lugha ya kudhalilisha ya kishenzi, mwanamke kama hafanyi biashara ya ngono kujiuza huwezi kusema ametumika.
 
Maana ya mahari imepotea, zamani ilikiwa ni shukrani kwa wazazi kwa KUKUTUNZIA mke wako.Je hiko kilichokuwa KINATUNZWA,siku hizi kuna wahuni wanakila bure,mume anatoa mahali hakipati hiko kilicho tunzwa.

Kama jamii yetu tukubali tu tumekengeuka ila mahali ilikuwa na maana nzuri,ilikuwa inahamasisha uwajibikaji kwa wazazi kwenye kumlea na kumtunza binti yao, vilevile kwa binti ilikuwa inachochea yeye kujitunza,kabla ya kukutana na mmewe.
 
Maana ya mahari imepotea, zamani ilikiwa ni shukrani kwa wazazi kwa KUKUTUNZIA mke wako.Je hiko kilichokuwa KINATUNZWA,siku hizi kuna wahuni wanakila bure,mume anatoa mahali hakipati hiko kilicho tunzwa.

Kama jamii yetu tukubali tu tumekengeuka ila mahali ilikuwa na maana nzuri,ilikuwa inahamasisha uwajibikaji kwa wazazi kwenye kumlea na kumtunza binti yao, vilevile kwa binti ilikuwa inachochea yeye kujitunza,kabla ya kukutana na mmewe.
Hakuna tofauti yoyote katika mapenzi kwa mwanaume kati ya mwanamke ambaye hajawahi kabisa kufanya mpenzia na aliyefanya mapenzi na mtu mmoja, wawili, watano au kumi. Tuache ujinga, ni psychology yako tu iliyotokana na utamaduni na dini pamoja na inferiority complex hasa ukiwa masikini kapuku.
 
Back
Top Bottom