Hoja ya kuongezewa muda wa Rais kubakia madarakani itaendelea kwa Rais Samia Suluhu Hassan?

Hoja ya kuongezewa muda wa Rais kubakia madarakani itaendelea kwa Rais Samia Suluhu Hassan?

Waliopendekeza tano tena kwa Magu did'nt see SSH coming -Iam Samia Suluhu Hassan rais halali wa Tanzania🙂. Happy combination of things ,President SSH anakula 4,5, tena 5. Wazanzibari oyee tumeshika usukani hadi 2035, it our turn to eat-nani kama mama?🙂🙂🙂🙂🙂🙂
 
Ali Kessi , Juma Nkamia na Deo Sanga Mungu kawaumbua kweli Hawa walamba makalio ya marehemu Jiwe .
 
Mama samia akienda vizuri hata miaka 20 sawa tu, kama ilivyo kwa Gadafi kuongoza miaka mingi mpaka mabeberu waliona wivu na kumfanyia hiyana.
Bado hujajifunza kitu kwa kilichotokea,maana yake ni kwamba kama ingekuwa mchakato wa kumuongezea muda Rais ungekuwa umefanikiwa sahizi anaeingia madarakani angeongoza labda term moja miaka 7 au 10,je hiyo miaka 7 au 10 ingeangukia kwa mtu haumpendi au ndio mbovu kupindukia tungefanyaje!?
 
Swali lako si sahihi. Waliokuwa wakisema hivyo, walikuwa wakijikita kwenye utendaji wa JPM waliouona. Hivyo wanasema aongezewe muda ili aendeleze hayo waliyoyaona. (Itoshe kusema JPM mwenyewe alilipinga wazo hilo mara kadhaa). Si sahihi kwako kuuliza hivi sasa kama udadisi huo utaendelea kwa Rais Samia kwa kuwa watu hawajaona ufanisi wake.
Kwahiyo ingekuwa amashaongezewa muda yakatokea haya yaliyotokea tungefanyaje na anaekuja hatujui utendaji wake?
 
Kwahiyo ingekuwa amashaongezewa muda yakatokea haya yaliyotokea tungefanyaje na anaekuja hatujui utendaji wake?
Kama hoja ilikuwa kumuongezea muda JPM, maneno yangetaja kabisa tunamuongezea JPM muda kwa ajili ya utendaji wake. Siyo tunamuongezea Rais muda, kitu ambacho kingemhusu kila Rais ajaye. Ilitokea Namibia Sam Nujoma aliongezewa muda wa miaka mitano kama Sam Nujoma. Akatawala kwa miaka 15. Aliyefuata alikuwa Pohamba ambaye aliishia miaka 10 tu ya kikatiba. Vivyo hivyo ingekuwa kwa JPM.
 
Praise and worship team ya hayati. Wanawaza na kuwazua nani Sasa wa kumwabudu? Nami nasema wa kumwabudu ni Mungu tu aliyetupa uzima huu. Mkome kumwabudu binadamu
 
Umenichekesha.
Nimecheka kwa sauti alafu Niko peke yangu.
Sasa hii ndio tofauti baina ya Ziwa na Bahari .Kumbe misifa ndio kazi yenu baadae unawaona watu wote wajinga kumbe umelewa misifa hatutaki misifa tunataka vitendo lkn naamini Mama Samia atawaonyesha kwa vitendo na sio misifaa.
 
Bora tu iongelewe mapema, Africa imekuwa na huu upumbavu wa kucheza na katiba kadri watawala wanavyotaka kama toilet paper
Mkuu, sikatai unalosema, lakini pia, kuna hatari ya kuwa paranoid kuhusu kuibiwa shamba utakalorithi mwaka 2025, wakati shamba lako la leo ulilonalo linaibiwa sana tu.

Sasa hapo ukijikita kulinda shamba utakalorithi mwaka 2025 wakati shamba lako la leo unaibiwa tayari, ni lazima nikuone mjinga tu.
 
Kama hoja ilikuwa kumuongezea muda JPM, maneno yangetaja kabisa tunamuongezea JPM muda kwa ajili ya utendaji wake. Siyo tunamuongezea Rais muda, kitu ambacho kingemhusu kila Rais ajaye. Ilitokea Namibia Sam Nujoma aliongezewa muda wa miaka mitano kama Sam Nujoma. Akatawala kwa miaka 15. Aliyefuata alikuwa Pohamba ambaye aliishia miaka 10 tu ya kikatiba. Vivyo hivyo ingekuwa kwa JPM.
Ukishabadilisha katiba useme tumetaka huyu tu ndio tunamuongezea muda,halafu aingie mwingine hamkupenda apate fursa kama ile mliyompa mtangulizi wake ni process ngumu maana ni mpaka yeye mwenyewe awe muungwana,yani hiyo itategemea yeye anatakaje?maana mwanzo mlikuwa na nguvu hata ya kumlazimisha mliemtaka lakini sasa itategemea aliepo anatakaje?akiwa anataka kung'ang'ania anapanga tu safu yake itakayompeleka alipopadhamiria.
 
Awali ya yote tupeane pole kwa msiba mkubwa wa kuondokewa na Mh Rais John Pombe Magufuli,hakika hayakuwa haya maisha ya dunian ila ni kitu chenye kupita tu.

Hapa karibuni kulikuwa na hoja ya kumuongezea muda wa kubakia madarakani Mh Rais John Pombe Magufuli na wengine wakaenda mbali na kusema kwamba akikataa tumlazimishe, pasipo na kujua kwamba ahadi ya uhai na maisha siri hii ipo kwa Mwenyezi Mungu. Leo hayupo Tena kwenye mgongo wa ardhi, hayupo tena.

Je, wale wahafidhina wa mitano Tena na kuongezwa kwa muda wa kukaa RAIS MADARAKANI, wataendelea na HOJA hii kwa MH RAIS Mama SAMIA SULUHU au walii-personalise kwa Hayati Mh RAIS Magufuli?

Aongezewe au Asiongezewe.
Wanaona aibu kubwa sn
 
Sasa hivi watakuwa wanajilaumu hata kuzuia Membe kumchallenge Bwana Mkubwa kwa kudai wana kautaratibu kao. Sasa ngoja tuone hako kautaratibu kao ya kwamba Mwenyekiti hawi challenged kama kataendelea 2025.
 
Back
Top Bottom