Hoja ya kuongezewa muda wa Rais kubakia madarakani itaendelea kwa Rais Samia Suluhu Hassan?

Hoja ya kuongezewa muda wa Rais kubakia madarakani itaendelea kwa Rais Samia Suluhu Hassan?

Nasisitiza, atake asitake lazima tumuongezee muda hata kwa kulazimisha.

Jamani MUNGU fundi nyie [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Anatuangalia mipango yetu alafu anasema ihiiii in magus voice[emoji23][emoji23][emoji23]
Niseme tu kuna haja ya kurudi na kujifanyia tathmini
Kupitia huu msiba kuna mengi ya kujifunza
Ni namna nyingine Mungu kajidhihirisha mimi ni Mungu nipo ambae nipo
Once again nakubali Mungu mkali sana[emoji1430]
Kama tungejua kesho yetu tungeishi Kama vile hii dunia ni mapito tu
 
What if kama umepeleka HOJA Kama hiyo na katiba ikabadilishwa,then all of the sudden RAIS huyo anafariki dunia Kama ilivyotokea hivi sasa,then akapatikana RAIS mwingine ambae ni mbovu na muovu,je tutarud Tena kubadilisha katiba na kupunguza muda wa RAIS KUBAKIA MADARAKANI??
Wangeweza kufikilia hilo wasingejaribu kumuongezea hata mwaka. Tatizo walimchukulia kamungu mtu ambacho akiwezi kufa.
 
Hiyo hoja itazima kama moto wa kifuu ukinyeshewa na mvua ya masika.

Hapa ndipo utagundua watu walivyo na degree za unafiki - sasa hivi wanamsoma Mama ili waone namna bora ya kumpamba pamba!! Subiri Bunge lianze ili ushuhudie wazee wa mishipa ya aibu iliyokatikaga!!
 
Awali ya yote tupeane pole kwa msiba mkubwa wa kuondokewa na Mh Rais John Pombe Magufuli,hakika hayakuwa haya maisha ya dunian ila ni kitu chenye kupita tu.

Hapa karibuni kulikuwa na hoja ya kumuongezea muda wa kubakia madarakani Mh Rais John Pombe Magufuli na wengine wakaenda mbali na kusema kwamba akikataa tumlazimishe, pasipo na kujua kwamba ahadi ya uhai na maisha siri hii ipo kwa Mwenyezi Mungu. Leo hayupo Tena kwenye mgongo wa ardhi, hayupo tena. He is very dead and very gone!

Je, wale wahafidhina wa mitano Tena na kuongezwa kwa muda wa kukaa RAIS MADARAKANI, wataendelea na HOJA hii kwa MH RAIS Mama SAMIA SULUHU au walii-personalise kwa Hayati Mh RAIS Magufuli?

Aongezewe au Asiongezewe.
kwani Samia ameshatimiza vipindi viwili vya miaka mitano mara ile?
 
Moja ya maradhi ya kudumu ya watu wa Kanda ya Ziwa ni kupenda kusifiwa kupitiliza …

Sie huku Pwani ukinizidishia Sifa naanza kuwa na tahadhari nawe!

Chawa wa awamu ya sita ndani ya tano wawe makini …Mf Lemutuz kaanza kumsifia Mama eti Kanyaga Twende…tumechelewa sana…yaan mara Hii Magu alikuwa anatuchelewesha!?…

Machawa mataahira hayana fursa awamu hii bila shaka
Sisi wa kanda ya ziwa its nature!! Ndiyo maana mzee wa mji (boma) akifika nyumbani toka matembezini kwa mfano watu wote kwenye boma lazima wasimamishe kazi zao zote wakamsalimie mzee kwa kupiga magoti kila mmoja kwa wakati wake...kuanzia Mkewe hadi watoto wote!! Watoto wakiume tu ndiyo hawapigi magoti.

Kisha mzee hubaki na watoto wake wa kiume tu kuongea nao kupata ripoti ya kutwa hasa reportya mifugo kuhusu malisho, maziwa yaliyokamuliwa na magonjwa kama yapo nk
kama mtoto wa kike akiwa na shida basi itapitia kwa mama yake yeye hana mamlaka ya kumwambia ama kumhoji baba yake - Mzee wa boma ni mtu mtu mkubwa!!

Ndiyo maana watoto wa kiume wote huitwa Ngosha!! Yaani Kidume.

Kama mzee wa boma akisafiri basi humteua kijana wake mkubwa kushika mji..(madaraka) huyo ndiyo atafanya kazi zote za boma kwa mujibu wa kanuni za mji ama kabila ambazo zipo wazi. Kama mama mwenye mji ( bi mkubwa) akiwa na jambo hana mamlaka ya uamuzi wa utekelezaji hadi ashirikiane na kijana - kijana akigoma basi jambo halitafanyika.
 
Awali ya yote tupeane pole kwa msiba mkubwa wa kuondokewa na Mh Rais John Pombe Magufuli,hakika hayakuwa haya maisha ya dunian ila ni kitu chenye kupita tu.

Hapa karibuni kulikuwa na hoja ya kumuongezea muda wa kubakia madarakani Mh Rais John Pombe Magufuli na wengine wakaenda mbali na kusema kwamba akikataa tumlazimishe, pasipo na kujua kwamba ahadi ya uhai na maisha siri hii ipo kwa Mwenyezi Mungu. Leo hayupo Tena kwenye mgongo wa ardhi, hayupo tena. He is very dead and very gone!

Je, wale wahafidhina wa mitano Tena na kuongezwa kwa muda wa kukaa RAIS MADARAKANI, wataendelea na HOJA hii kwa MH RAIS Mama SAMIA SULUHU au walii-personalise kwa Hayati Mh RAIS Magufuli?

Aongezewe au Asiongezewe.
Inawezekana walikuwa wakitoa maoni hayo kutokana na utendaji Wa marehemu so Mh. Samia nae akifanya vema sana huenda kukawa na maoni kama hayo!
 
Back
Top Bottom