Hoja ya Mbowe: Je, mbunge anaapa mbele ya Spika au anaapishwa na Spika mbele ya Bunge?

Hoja ya Mbowe: Je, mbunge anaapa mbele ya Spika au anaapishwa na Spika mbele ya Bunge?

Kwangu mimi katika yote yaliyozungumzwa kiapo cha mbunge ndio kimenipa tafakuri.

Spika Ndugai baada ya kuwaapisha wabunge 19 wa Chadema kwenye viwanja vya bunge alisema kanuni zinamruhusu kumuapisha mbunge mahali popote palipoandaliwa.
Cha muhimu ni mbunge kuapa mbele ya Spika.

Mbowe ambaye ni KUB mjumbe wa kamati ya kanuni mstaafu anasema kwa mujibu wa katiba mbunge anapaswa kuapishwa na Spika mbele ya bunge ( nationak assembly) huku Siwa ikiwa inang'aa na si binginevyo.

Nimechukua Biblia takatifu, Katiba ya JMT na ninatafuta kitabu cha kanuni za bunge ili nijielimishe zaidi.

Nawatakia Sabato yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Chaguzi ndogo nyingi zimefanyika huko nyuma ni lini washindi waliapishwa nje ya bunge? Tena ikiwa si ktk kipindi cha bunge? Kulikuwa na haraka gani ikwa spika kisha pewa majina?
 
Binafsi natanguliza shukrani za dhati kwa CC ya CHADEMA kwa kufanya maamuzi sahihi kwa wakati Sahihi, Kwa kweli lile lilikuwa jaribio kubwa ambalo lingetuweka kwenye mtego wa misimamo yetu, kwamba kweli sisi ni baridi ama Vuguvugu. Kwa juu juu wale "wafuasi" 19 walihisi wao ni Mwamba usioweza kutingishwa lakini haikuwa hivyo, nobody embrace them. Pamoja na mambo mengi tuliyojifunza katika sakata hili juu ya upindishwaji wa sheria, jambo linalotupa shaka sana ni kwa nini Wanaohitaji zaidi hao wabunge wa VM ni ccm na sio CHADEMA? kwanini wao wanaumia zaidi na maamuzi ya Kamati kuliko wenye chama wenyewe? Kumbuka before that AG hakuwahi kuwa upande wa Kuitetean chadema kwa jambo lolote ila kwa hili anasema Taratibu zilifuatwa, Kumbuka Pia SPIKA anakichukia chama lakini kwenye hili alisema "Atawalinda kwa gharama zozote ", what is behind all this?
who is behind all this?
Kwanini wanaumia wao?
Kwanini wao wanataka zaidi ya sisi?
Kwa nini wanatetea hao 19 katika jambo hili?
Nani anafaidika exactly na hao Covid 19?

Ukiweza kujibu maswali hayo yote utaelewa ni kwanini wanaoumia zaidi ni wao kuliko sisi baada ya maazimio ya Chama.

Binafsi nipo nasheherekea maamuzi ya chama nikiwa Mezani 🍻🍻
 
Kwangu mimi katika yote yaliyozungumzwa kiapo cha mbunge ndio kimenipa tafakuri.

Spika Ndugai baada ya kuwaapisha wabunge 19 wa Chadema kwenye viwanja vya bunge alisema kanuni zinamruhusu kumuapisha mbunge mahali popote palipoandaliwa.
Cha muhimu ni mbunge kuapa mbele ya Spika.

Mbowe ambaye ni KUB mjumbe wa kamati ya kanuni mstaafu anasema kwa mujibu wa katiba mbunge anapaswa kuapishwa na Spika mbele ya bunge ( nationak assembly) huku Siwa ikiwa inang'aa na si binginevyo.

Nimechukua Biblia takatifu, Katiba ya JMT na ninatafuta kitabu cha kanuni za bunge ili nijielimishe zaidi.

Nawatakia Sabato yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Hata kama kanuni hazisemi waape ndani ya Bunge, ni utamaduni wa miaka nenda rudi kama kuna Mbunge mpya kikao kinachofuata baada tuu ya sala ni KIAPO. Hakuna rejea ya Mbunge aliyewahi kuapitisha nje ya vikao vya mkutano wa Bunge
 
Mbowe anajua mpango mzima wa kina Mdee. Ila kwa vile ni mtu wetu na tumempa kazi yetu ya kukisambaratisha chama kama ilivyokuwa kwa NCCR ya Mrema basi hatuna budi kumpongeza kwa hatua anazochukua siku baada ya siku kukimong'onyoa. Bila Mbowe kuturahisishia kazi mwaka 2015 kwa kumchukua mwenzetu Lowasa akasaidie kukimong'onyoa na kukisambaratisha chama namna hii, basi leo hii huenda CCM tungekuwa chama cha upinzani maana ukawa before Dr Slaa na Lipumba watimke ilikuwa ni tishio kubwa sana kwetu. Imagine kufukuzwa hao wabunge 19 wenye ushawishi ndan ya chama, wataondoka na watu wangapi ndan ya chama ambao huenda hawatofurahishwa na kufukuzwa kwao
Shukuru Tume ya Uchaguzi,Policcm na TISS kucheza bao la mkono ili kuokoa jahazi 2015 vinginevyo ENL angekuwa anaendea na awamu ya Pili akiwa CDM.Mbowe alicheza vizuri kwa kubadili gia angani baada ya Dr.Slaa kukimbia.
 
Kwangu mimi katika yote yaliyozungumzwa kiapo cha mbunge ndio kimenipa tafakuri.

Spika Ndugai baada ya kuwaapisha wabunge 19 wa Chadema kwenye viwanja vya bunge alisema kanuni zinamruhusu kumuapisha mbunge mahali popote palipoandaliwa.
Cha muhimu ni mbunge kuapa mbele ya Spika.

Mbowe ambaye ni KUB mjumbe wa kamati ya kanuni mstaafu anasema kwa mujibu wa katiba mbunge anapaswa kuapishwa na Spika mbele ya bunge ( nationak assembly) huku Siwa ikiwa inang'aa na si binginevyo.

Nimechukua Biblia takatifu, Katiba ya JMT na ninatafuta kitabu cha kanuni za bunge ili nijielimishe zaidi.

Nawatakia Sabato yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Uvccm wameumizwa zaidi na kufukuzwa kwa Covid 19 kuliko hata Bawacha wenyewe
 
Duh huu uzi wa warembo wakali jf photos si mchezooo ngj niende huko

Ova
 
Mmeshalegea, mliambiwa mkajidai vichwa ngumu hiyo ndio Chadema, kawachukueni muwapeleke lumumba.
Na alivyo kichwa maji yule bosi wao atawateua kushika nyadhifa mbalimbali wote akiamini anawakomesha chadema (zero IQ)
 
Chama changu kinachezeshwa kwata na ccm. Hii hatua iliyochukuliwa na chama ilijadiliwa na upande wa pili.

Wakifutwa uanachama wadada wanakwenda mahakamani kupinga kufutwa,kesi inapigwa miaka miwili wadada wanarudishiwa uanachama wao, cdm watakatarufaa kesi inapingwa hukumu inatoka baada ya miaka mingine miwili au muda mfupi kabla ya uchaguzi 2025.

Ninasikitika kwa Chama changu kutokuona mgogoro huu kupitia intelijensia yake. Ni kweli kilichofanywa na hawa wadada kinaudhi ila tulikuwa wapi kama viongozi kuliona hilo, tetesi zilikuwepo muda mrefu mkapuuzia badala ya kuchukua hatua mapema. Au hatua mnazopenda kuichukua ndiyo hizi?

Na Ndugai ameapa kuwalinda kwa hiyo hakuna cha kuwatoa akina Halima Bungeni.
Mbona bomba tu!,Acha yule kubwa jinga Ndugai awalinde,lakini kitu cha muhimu ni kufahamu kuwa Hao Wabunge watakuwa ni Wabunge wasio na Chama;Kwa hiyo Ukweli kuwa Bunge halina Upinzani utabaki pale pale kwa mantiki hiyo Lengo la CCM la kulazimisha Upinzani wawepo bungeni halitafanikiwa,Dunia itafahamu kuwa Bunge ni la Chama kimoja.
 
KWELI MZEE MGAYA NI MZIGO....HUJUI TOFAUTI YA BUNGENI NA BUNGE.

HAKIKA MGAYA NI CHENGA#
 
Katiba imesema "before the parliament",na spika wakati anawaapisha akina Halima,alitoa ufafanuzi kuwa kabla ya kamati kutunga sheria ndogo ilikuwa ni lazima wabunge waapishwe bungeni mbele ya wabunge!Kwamba hiyo ilitoa changamoto kwasababu wabunge wakikosa kuapishwa bunge la kwanxa ilibidi wasubiri mpaka mkutano mwingine ili waapishwe!Hiyo ilipelekea wabunge kuchelewa kutekeleza majukumu yao kusubiri kuapishwa!

Kwa maelezo hayo ya Ndugai ni wazi hata spika anaelewa "before the parliament" inamaana gani ndio maana hakukuwahi kutokea mtu kuapishwa nje ya bunge!

Bunge la 11 lilifanya marekebisho ya sheria ili mtu aweze kuapishwa nje ya bunge,cha ajabu wakasahau kubadili katiba ambayo mpaka leo inatamka wabunge wataapishwa ndani ya mkutano wa bunge!

Ndio nasema Katiba ni sheria mama,sheria zozote zinazokinzana na katiba ni batili
Nimekuelewa bwashee!
 
Katiba inasemahivi soma kwenye screenshot

Oath of
Members of
Parliament
Act No.15
of 1984,
Art.13
68. Every Member of Parliament shall be required to take and subscribe
before the National Assembly the oath of allegiance before commencing to take
part in the business of the National Assembly save that he may take part in the
election of Speaker before taking that oath.

kwa kiswahili ni hivi

Kiapo cha
Wabunge
Sheria ya
1984 Na.15
ib.13
68. Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha
uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini
Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla
hajaapishwa.

usije kusema nimetunga na screenshot ya katiba juu

View attachment 1636519

Ndiyo maana uwa ninasema hatuhitaji katiba mpya maana hata iliyopo ni nzuri ina mengi ambayo hayazingatiwi. Ila tunahitaji mfumo wa vyombo vinavyoweza kusimamia katiba
Before National Assembly kwa kiswahili ni " Katika bunge "?

Jawabu Tafadhali!
 
Mimi nilivyomuelewa mheshimiwa sana ndugai ni kuwa ilimradi mbunge awe mbele ya spika tu,,
Haijalishi iwe wapi,kichakani twende,mlimani sawa tu,,sokoni yaani popote tu,,nilivyoelewa,,kabda wataalamu waliosomea kanuni za bunge waje wafafanue
 
Before National Assembly kwa kiswahili ni " Katika bunge "?

Jawabu Tafadhali!
Hizo ni katiba za tanzania sijatafsiri ndiyo tafsiri ya katiba ya kiswahili. Na hizi ni screenshot za katiba yetu usije sema ni tafsiri yangu. Na kumbuka katika masuala ya kisheria hata hukumu zetu zinaandikwa kwa Kingereza kwasababu ya limitation ya lugha ya Kiswahili.

Kwa Kingereza Screenshot ya Katiba ya Tanzania ni hii
katiba.jpg


Kwa kiswahili wameitafisiri hivi siyo mimi

1606561304381.png
1606561304381.png


Na mara zote vyombo vya kisheria hutumia tafsiri ya Kingereza.

Unless unataka kujustify kilichofanyika ila ukweli uko wazi tu katiba inapingana na kilichofanyika. Au hiki nilichokupostia si Katiba ya Tanzania?
 
Hizo ni katiba za tanzania sijatafsiri ndiyo tafsiri ya katiba ya kiswahili. Na hizi ni screenshot za katiba yetu usije sema ni tafsiri yangu. Na kumbuka katika masuala ya kisheria hata hukumu zetu zinaandikwa kwa Kingereza kwasababu ya limitation ya lugha ya Kiswahili.

Kwa Kingereza Screenshot ya Katiba ya Tanzania ni hii
View attachment 1636716

Kwa kiswahili wameitafisiri hivi siyo mimi

View attachment 1636717View attachment 1636717

Na mara zote vyombo vya kisheria hutumia tafsiri ya Kingereza.

Unless unataka kujustify kilichofanyika ila ukweli uko wazi tu katiba inapingana na kilichofanyika. Au hiki nilichokupostia si Katiba ya Tanzania?
Nimekuelewa bwashee ila nadhani Spika Ndugai alitumia katiba ya kiswahili!
 
Back
Top Bottom