Hoja ya Mbowe: Je, mbunge anaapa mbele ya Spika au anaapishwa na Spika mbele ya Bunge?

Hoja ya Mbowe: Je, mbunge anaapa mbele ya Spika au anaapishwa na Spika mbele ya Bunge?

Kwangu mimi katika yote yaliyozungumzwa kiapo cha mbunge ndio kimenipa tafakuri.

Spika Ndugai baada ya kuwaapisha wabunge 19 wa Chadema kwenye viwanja vya bunge alisema kanuni zinamruhusu kumuapisha mbunge mahali popote palipoandaliwa.
Cha muhimu ni mbunge kuapa mbele ya Spika.

Mbowe ambaye ni KUB mjumbe wa kamati ya kanuni mstaafu anasema kwa mujibu wa katiba mbunge anapaswa kuapishwa na Spika mbele ya bunge ( national assembly) huku Siwa ikiwa inang'aa na si binginevyo.

Nimechukua Biblia takatifu, Katiba ya JMT na ninatafuta kitabu cha kanuni za bunge ili nijielimishe zaidi.

Nawatakia Sabato yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!

Hapana kusahau Yule msiyemtaka gwiji wa magwiji mliyepanga kumwua pia "in attendance" alikuwamo.

Eeh mola wetu na ukamjalie maisha marefu na maono zaidi yatakayofanikisha ukombozi wa kweli wa nchi hii.
 
Kuwa na demokrasia Afrika, hususani Tanzania ni busara za rais aliyepo madarakani.
 
Hapana kusahau Yule msiyemtaka gwiji wa magwiji mliyepanga kumwua pia "in attendance" alikuwamo.

Eeh mola wetu na ukamjalie maisha marefu na maono zaidi yatakayofanikisha ukombozi wa kweli wa nchi hii.
Gwiji wa nini?
 
Imagine chadema bila hao wadada
Siasa za kufuata watu hazina nafasi karne hii, bali siasa za masuala( issues) watu huja na kuondoka! Na hubadilika. Better be principled.
 
Twende na nani 2025 Shangazi au Amsterdam? [emoji16] [emoji23] [emoji23]
 
Kwangu mimi katika yote yaliyozungumzwa kiapo cha mbunge ndio kimenipa tafakuri.

Spika Ndugai baada ya kuwaapisha wabunge 19 wa Chadema kwenye viwanja vya bunge alisema kanuni zinamruhusu kumuapisha mbunge mahali popote palipoandaliwa.
Cha muhimu ni mbunge kuapa mbele ya Spika.

Mbowe ambaye ni KUB mjumbe wa kamati ya kanuni mstaafu anasema kwa mujibu wa katiba mbunge anapaswa kuapishwa na Spika mbele ya bunge ( national assembly) huku Siwa ikiwa inang'aa na si binginevyo.

Nimechukua Biblia takatifu, Katiba ya JMT na ninatafuta kitabu cha kanuni za bunge ili nijielimishe zaidi.

Nawatakia Sabato yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Ukipata ulete mrejesho
 
Sitaki kuamini kuwa Spika wa Bunge hakujua kuwa Katiba inapingana na kanuni walizotengeneza.

Hili suala lilikuwa linafanyika kwa lengo la kupata pesa za wafadhili, lakini walijua mchakato wa kuwapata hao Wabunge ni Batili hivyo walitarajia mambo mawili.

1. Kufanikisha kupata Wabunge hao na pesa kutoka kwa Wafadhili ziendelee kuletwa.
Au
2. Kuwapata Wabunge na wafadhili wakasitisha misaada kutokana na ubatili wa mchakato uliotumika.

Kama ikitokea namba mbili hapo juu maana yake Bunge litakosa pesa lakini pia idadi ya Wabunge itakuwa kubwa na gharama ya kuliendesha itakuwa mzigo zaidi.

Ndiyo maana ya uapisho wenye ukakasi ili kama itatokea lengo mahsusi la kupata pesa za Mabeberu litagonga mwamba hao Wabunge 19 watenguliwe.

Itakuwa ni issue simple sana, anatokea mtu mmoja anafungua kesi Mahakamani dhidi ya mchakato uliotumika kuwapata hao Wabunge wa viti maalumu na namna walivyoapishwa. Wabunge hao watavuliwa nyadhifa zao. Mchezo unakuwa umeisha.
 
Tumia akili ndogo TU, umewahi kuona Padree/mchungaji añafungisha Ndoa nje na Kanisani??

Waswahili tunasema Hilo swala ni TENDO UNENI!! Maana yake nini lazima kuwe na eneo husika na vifaa vyakulikamilisha Hilo TENDO la UNENI. Shida nikwamba huko sisiem mmejaa mabichwa maji😂
 
Back
Top Bottom