Hoja ya msingi ni mgongano wa kimaslahi. NIDA ni moja tu ya mbinu kadhaa zilizopo

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,439
Reaction score
145,410
Miaka nenda rudi nimekuwa nikisema kuwa hakuna maana yoyote ile kushiriki katika chaguzi nchi hii.

Hiyo ni kwa sababu chaguzi zote zimekuwa ni maigizo tu.

Nimekuwa nikisema kwamba, kushiriki uchaguzi ambao utaendeshwa na kusimamiwa na tume ya uchaguzi ambayo imeundwa na mwenyekiti wa CCM ambacho ndo chama tawala, ambaye ndo Rais wa nchi, ambaye pia naye ni mgombea urais kwenye uchaguzi, ni umajinuni.

Ni umajinuni kwa sababu ya mgongano wa wazi kabisa wa kimaslahi uliopo hapo.

Mgongano huo wa kimaslahi unatokana na Ukweli wa kwamba, hao watu wa kwenye tume ya uchaguzi wako beholden [sijui Kiswahili chake] kwa yule aliyewateua.

Hili ni jambo rahisi sana kuliona na kulielewa.

Lakini kwa bahati mbaya, kwa watu walio wengi, si suala rahisi kivile. Na sijui kwa nini iko hivyo.

Kibao kingegeuzwa, yaani hiyo tume ya uchaguzi iundwe na mwenyekiti wa CHADEMA, kwa mfano, ambaye naye ni mgombea urais, sidhani kama CCM ingelikubali kushiriki kwenye uchaguzi chini ya mazingira kama hayo.

Jana Humphrey Polepole kasema kwamba hiyo tume ya uchaguzi imeunganishwa sijui na NIDA, blah blah blah.

Basi tokea hiyo jana, baadhi ya watu eti ndo wameamini sasa kuwa kweli CCM huwa inafanya figisu kwenye chaguzi.

Kwa taarifa yenu sasa, hata kabla ya uwepo wa NIDA, CCM na tume zake za uchaguzi zimekuwa zikifanya figisu.

Muulizeni hayati Maalim Seif Sharif Hamad alifanyiwa nini kule Zanzibar kwenye uchaguzi wa mwaka 1995.

Hakukuwepo na NIDA wakati huo.

Hii ya NIDA ni moja tu ya mbinu katika kibanda chao cha kufanyia figisu.

Tatizo la msingi lipo kwenye namna chombo kilicho na mamlaka ya kuendesha chaguzi, kinavyoundwa.

Tatua tatizo la msingi, hayo mengine yatajirekebisha accordingly.

Watanzania wanasikitisha sana kwenye uwezo wao wa common sense.

Kitu kilekile ambacho wengine tumekuwa tukikisema kwa miaka mingi tu sasa, jana kakisema Polepole, imekuwa kama vile ni habari mpya!

Inashangaza sana na inasikitisha pia.
 
737adb7c-b4fa-412f-b008-f8bd4c4dd728.jpeg
 
Ni kweli mlikis

Ema, lakini uwezo wenu wa kilifanua hili ili tuwaelewe ni mdogo!
 
Muhimu ni hilo mfumo wa ccm umeunganishwa moja kwa moja na time ya uchaguzi. Hili ndilo kubwa.

Ccm kuunganishwa na nida mi kwa ajili ya kupata data tu.
 
Mbinu NI nyingi Sana
1.kuwa na vituo fake
2.kuingiza ma box yenye kura tayari
3.kuhonga waangalizi
4.kupindua Tu matokeo kwa ubabe
5.n.k n.k
Siku hizi matokeo yanajazwa tu kwa ubabe kwa msaada wa polisi bila hata kuhesabu kura.
Mtu mpumbavu pekee ndiye anaweza kupoteza muda wake kushiriki uchaguzi wa namna hii
 
Back
Top Bottom