Hoja ya msingi ni mgongano wa kimaslahi. NIDA ni moja tu ya mbinu kadhaa zilizopo

Asante sana kwa kulileta hili, binafsi nimeshangaa sana uwezo wa kufikiri wa watu humu, hili sio geni lipo miaka na miaka linajulikana na limesemwa sana.

Walipokwama Watanzania ni nini wafanye kuliondoa hili Tatizo ili uchaguzi uwe huru na haki, tatizo kama tatizo Watanzania wanalijua hawahitaji kuambiwa na kuwa big deal saana.

Ndani ya mitaa ya Benghazi Libya.
 
Mbinu NI nyingi Sana
1.kuwa na vituo fake
2.kuingiza ma box yenye kura tayari
3.kuhonga waangalizi
4.kupindua Tu matokeo kwa ubabe
5.n.k n.k
Ni kweli kanisa, mbinu zinazotumika ni nyingi. Kudhani hiyo ya nida tu, mtu unajidanganya. NIDA kushamiri TZ wala si muda mrefu, lakini hata huko nyuma toka wakati ule Mrema ni mrema kweli hakukuwa na NIDA na alipigwa mchana kweupeeeeee. Eti Mrema ashindwe uchaguzi na Mkapa wakati ule!. Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini hilo.

Hata ukighairishwa uchaguzi na kusema Tufanye mwezi wa 12/2025, ili kufanya maridhiano na kurekebisha hilo la NIDA. Bado wapinzani watapigwa tu, kwa sababu moja tu. Hawa jamaa wana mbinu nyingi, kama Nape alivyosema. Yaani kuna halali, nusu halali na haramu. Halali ni pamoja na mapesa waliyokuwa nayo, hivyo kufanya kampeni ya uhakika. Haramu ndio hiyo ya kutumia mbinu mbadala za udanganyifu kama hiyo NIDA. Na nusu halali ni mchanganyiko wa vyote hivyo viwili.

Twende kwenye uchaguzi, lakini aliyoyasema Pole2 iwe sehemu kubwa ya mjadala/maridhiano 2026 - 2029. Ili uchaguzi wa 2030 uwe umecover dosari zote za uchaguzi wa 2025. Katiba mpya ndio uwe msingi mkuu wa maridhiano katika mazungumzo ya 2026-2029.
 
Miaka nenda rudi nimekuwa nikisema kuwa hakuna maana yoyote ile kushiriki katika chaguzi nchi hii.

Hiyo ni kwa sababu chaguzi zote zimekuwa ni maigizo tu.

Nimekuwa nikisema kwamba, kushiriki uchaguzi ambao utaendeshwa na kusimamiwa na tume ya uchaguzi ambayo imeundwa na mwenyekiti wa CCM ambacho ndo chama tawala, ambaye ndo Rais wa nchi, ambaye pia naye ni mgombea urais kwenye uchaguzi, ni umajinuni.

Ni umajinuni kwa sababu ya mgongano wa wazi kabisa wa kimaslahi uliopo hapo.

Mgongano huo wa kimaslahi unatokana na Ukweli wa kwamba, hao watu wa kwenye tume ya uchaguzi wako beholden [sijui Kiswahili chake] kwa yule aliyewateua.

Hili ni jambo rahisi sana kuliona na kulielewa.

Lakini kwa bahati mbaya, kwa watu walio wengi, si suala rahisi kivile. Na sijui kwa nini iko hivyo.

Kibao kingegeuzwa, yaani hiyo tume ya uchaguzi iundwe na mwenyekiti wa CHADEMA, kwa mfano, ambaye naye ni mgombea urais, sidhani kama CCM ingelikubali kushiriki kwenye uchaguzi chini ya mazingira kama hayo.

Jana Humphrey Polepole kasema kwamba hiyo tume ya uchaguzi imeunganishwa sijui na NIDA, blah blah blah.

Basi tokea hiyo jana, baadhi ya watu eti ndo wameamini sasa kuwa kweli CCM huwa inafanya figisu kwenye chaguzi.

Kwa taarifa yenu sasa, hata kabla ya uwepo wa NIDA, CCM na tume zake za uchaguzi zimekuwa zikifanya figisu.

Muulizeni hayati Maalim Seif Sharif Hamad alifanyiwa nini kule Zanzibar kwenye uchaguzi wa mwaka 1995.

Hakukuwepo na NIDA wakati huo.

Hii ya NIDA ni moja tu ya mbinu katika kibanda chao cha kufanyia figisu.

Tatizo la msingi lipo kwenye namna chombo kilicho na mamlaka ya kuendesha chaguzi, kinavyoundwa.

Tatua tatizo la msingi, hayo mengine yatajirekebisha accordingly.

Watanzania wanasikitisha sana kwenye uwezo wao wa common sense.

Kitu kilekile ambacho wengine tumekuwa tukikisema kwa miaka mingi tu sasa, jana kakisema Polepole, imekuwa kama vile ni habari mpya!

Inashangaza sana na inasikitisha pia.
Watu wanatekwa povu kwani Kuna jipya gani ameongea Polepole balo halijulikani?
 
View: https://youtu.be/bsMYAk6cWaE?si=UJ9sO6gsQw5G-9Mu

Na ukisikiliza hapa alichokiongea Nape akiwa Kagera haikuwa bahati mbaya japo wapo waliosema alikuwa amelewa.

Ukimsikiliza huyu DC wa Longido ambaye pia baada ya kutoa ya sirini alitenguliwa unapata picha inabidi tume ifumuliwe yote na kuanza upya , hivi kwa akili timamu nchi itakuwaje na uchaguzi huru kama kuna mbinu za maporini kama guerilla warfare?

View: https://youtu.be/dTvdkX19XOs?si=XLLjLMhv7zUCa5zT

Tume ni mateka wa mwenyekiti wa CCM .

Compromised beyond repair.
 
Serikali hiii huwa wanatumia taarifa zilizopita, uchaguzi huu watatumia kura za 2020, wata chakachua numbee na kuzigawa gawa wajuavyo na kutangaza mshindi.

Huwa nawaambia watu humu, upige usipige wao tayari wanayo matokeo yao.

Zoezi la kujiandikisha lilipo dorola, hao nida walienda mashuleni kuandikisha wanafunzi kwa nguvu nanyi mnaelewa wanafunzi hawawezi kukataa.

Huko nida wanachakata taarifa zenu wana sema waliojitokeza ni wengi hata wasipojitokeza kabisa.
Nilikotoka mimi nilishangaa mgawanyo wa kura unakuta ccm 6000,, CHADEMA 2000, NRA 4000, ADA 5200, TADEA 3100, TLP 2500, NK.

Yani kule vijijini tulishangaa nani anaifahamu NRA au TADEA, lakini vilipata kura za kutisha.
CCM wanacheza na akili za watu.

Samia aliwahi kusema hata ukiipigia CHADEMA , CCM ndiyo itaunda serikali. Kupiga chadema ni sawa na kumwaga sukari baharini.

Ndio maana hawataki wasimamizi wa vyama watangaze matokeo ya vituoni, hawataki simu, wala kupiga picha matokeo yooote hiyo ni kujirahisishia kuiba kura na kujitangaza washindi.

October tusipige kura, iwe siku ya mapumziko.
 
Philosophical thoughts by Bishop Benson Kalikawe Lwakalinda Bagonza (PhD)

WOTE TUKO NJIAPANDA: Tupande gari gani?

Humphrey Polepole ametuweka njia panda sote. Anayedhani hayuko njia panda, yawezekana tayari ni abiria wa gari la mbele. Tutafakari:

1. Kuna watu usipowasikiliza, ni hasara. Ukiwasikiliza ni hasara pia. Humphrey Polepole ni mmoja wao. Usipomsikiliza unakosa mengi. Ukimsikiliza, anakushawishi kutenguka katika basdhi ya misimamo yako. Chagua kwa hekima.

2. Nani ni bora? Shetani aletaye habari njema au malaika aletaye habari mbaya?
Tuangalie kwa makini vipa umbele vyetu:
-Mungu/Taifa/Chama
Vs
-Chama/Taifa/Mungu

Chagua kwa hekima.

3. Twaweza kumpuuza Humphrey Polepole. Je tutapuuza madhara ya kumpuuza? Chagua kwa busara kati ya kupuuza huku usiweze kupuuza madhara ya upuuzi wako.
Kama anasema uwongo anamdanganya nani? Mungu? Wananchi? Yeye mwenyewe?

4. Kama ni kweli tufanyeje? Kama ni uwongo tufanyeje? Kwa nini aliyoyasema yanafanana na imani na uzoefu wetu? Kwa nini wanaosema aliyoyasema ni uwongo hata wao wanajiona ni waongo?

5. Viapo vyetu viko njiapanda: kukiuka kiapo kwa kusema kweli au kutunza kiapo kwa kuficha ukweli? Tunapoapa twamwapia mwanadamu au Mungu? Tukishupaza shingo (Impunity), twamfanyia Polepole, Katiba, Katiba, wananchi?

6. Hatujui tumefikaje hapa. Tuna uwezo wa kujua tutokeje. Tulinde kura moyoni? Tutiki wakati imeishatikiwa? Tusubiri reform?
Tupige kura kuamua kama tuchague au tusichague?

Unyenyekevu si udhaifu
TURUDI MEZANI
UKWELI ULIOCHELEWA NI BORA KULIKO UWONGO UNAOFARIJI.
HAKUNA TOBA ILIYOCHELEWA
 
Hofu yetu haipaswi kuishia kwenye CCM kutumia NIDA kwa ajili ya uchaguzi, no CCM kumiliki taarifa zako sensitive kama za NIDA ni hatari kwa usalama wa Taifa na maslahi yake...

Kwa maana nyingine tunatakiwa kuhofia impunity ya CCM kuliko wakati wote, CCM inaweza kuchunguza unapokaa, Ndugu zako, watu wote unaojihusiha nao wakati wowote wanaotaka, hii ni Risk kubwa sana kwa Raia Mmoja Mmoja.

Kumbuka namba ya NiDA imeumgwanishwa na kila kitu hapa nchni hiki kitendo kinaipa CCM nguvu kubwa kutumia taarifa zetu kwa maslahi yetu, but Je CCM wanatumia njia gani kuzihifadhi na hizi taarifa na je zikipotea mikononi mwa CCM
 
Basi tokea hiyo jana, baadhi ya watu eti ndo wameamini sasa kuwa kweli CCM huwa inafanya figisu kwenye chaguzi.
Naam, sisi watanzania wenyewe tupotupo tu --- hili ndo tatizo kubwa kabisa la kwanza
 
Sawa hata kama uwezo wetu wa kufikiri ni finyu sisi tunachotaka tu ni amani wafanye figisu kwenye kura hizo shauri zao tunachotaka tu ni amani ili mkono uende kinywani na tuwe na mazingira rafiki yakunya na kutandaza miti.
 
Mtanzania wa kawaida kabisa akapanga mstari kupiga kura mwaka huu, hakika nitaamini "akili ni nywele na kila mtu ana zake"!!!
 
Hofu yetu haipaswi kuishia kwenye CCM kutumia NIDA kwa ajili ya uchaguzi, no CCM kumiliki taarifa zako sensitive kama za NIDA ni hatari kwa usalama wa Taifa na maslahi yake...

Kwa maana nyingine tunatakiwa kuhofia impunity ya CCM kuliko wakati wote, CCM inaweza kuchunguza unapokaa, Ndugu zako, watu wote unaojihusiha nao wakati wowote wanaotaka, hii ni Risk kubwa sana kwa Raia Mmoja Mmoja.

Kumbuka namba ya NiDA imeumgwanishwa na kila kitu hapa nchni hiki kitendo kinaipa CCM nguvu kubwa kutumia taarifa zetu kwa maslahi yetu, but Je CCM wanatumia njia gani kuzihifadhi na hizi taarifa na je zikipotea mikononi mwa CCM
🤣

Umeandika nini hapo wewe?
 
Miaka nenda rudi nimekuwa nikisema kuwa hakuna maana yoyote ile kushiriki katika chaguzi nchi hii.

Hiyo ni kwa sababu chaguzi zote zimekuwa ni maigizo tu.

Nimekuwa nikisema kwamba, kushiriki uchaguzi ambao utaendeshwa na kusimamiwa na tume ya uchaguzi ambayo imeundwa na mwenyekiti wa CCM ambacho ndo chama tawala, ambaye ndo Rais wa nchi, ambaye pia naye ni mgombea urais kwenye uchaguzi, ni umajinuni.

Ni umajinuni kwa sababu ya mgongano wa wazi kabisa wa kimaslahi uliopo hapo.

Mgongano huo wa kimaslahi unatokana na Ukweli wa kwamba, hao watu wa kwenye tume ya uchaguzi wako beholden [sijui Kiswahili chake] kwa yule aliyewateua.

Hili ni jambo rahisi sana kuliona na kulielewa.

Lakini kwa bahati mbaya, kwa watu walio wengi, si suala rahisi kivile. Na sijui kwa nini iko hivyo.

Kibao kingegeuzwa, yaani hiyo tume ya uchaguzi iundwe na mwenyekiti wa CHADEMA, kwa mfano, ambaye naye ni mgombea urais, sidhani kama CCM ingelikubali kushiriki kwenye uchaguzi chini ya mazingira kama hayo.

Jana Humphrey Polepole kasema kwamba hiyo tume ya uchaguzi imeunganishwa sijui na NIDA, blah blah blah.

Basi tokea hiyo jana, baadhi ya watu eti ndo wameamini sasa kuwa kweli CCM huwa inafanya figisu kwenye chaguzi.

Kwa taarifa yenu sasa, hata kabla ya uwepo wa NIDA, CCM na tume zake za uchaguzi zimekuwa zikifanya figisu.

Muulizeni hayati Maalim Seif Sharif Hamad alifanyiwa nini kule Zanzibar kwenye uchaguzi wa mwaka 1995.

Hakukuwepo na NIDA wakati huo.

Hii ya NIDA ni moja tu ya mbinu katika kibanda chao cha kufanyia figisu.

Tatizo la msingi lipo kwenye namna chombo kilicho na mamlaka ya kuendesha chaguzi, kinavyoundwa.

Tatua tatizo la msingi, hayo mengine yatajirekebisha accordingly.

Watanzania wanasikitisha sana kwenye uwezo wao wa common sense.

Kitu kilekile ambacho wengine tumekuwa tukikisema kwa miaka mingi tu sasa, jana kakisema Polepole, imekuwa kama vile ni habari mpya!

Inashangaza sana na inasikitisha pia.
Vipi ikiwa Polepole ni mradi mwingine wa chama tawala?
 
Ni kweli kanisa, mbinu zinazotumika ni nyingi. Kudhani hiyo ya nida tu, mtu unajidanganya. NIDA kushamiri TZ wala si muda mrefu, lakini hata huko nyuma toka wakati ule Mrema ni mrema kweli hakukuwa na NIDA na alipigwa mchana kweupeeeeee. Eti Mrema ashindwe uchaguzi na Mkapa wakati ule!. Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini hilo.

Hata ukighairishwa uchaguzi na kusema Tufanye mwezi wa 12/2025, ili kufanya maridhiano na kurekebisha hilo la NIDA. Bado wapinzani watapigwa tu, kwa sababu moja tu. Hawa jamaa wana mbinu nyingi, kama Nape alivyosema. Yaani kuna halali, nusu halali na haramu. Halali ni pamoja na mapesa waliyokuwa nayo, hivyo kufanya kampeni ya uhakika. Haramu ndio hiyo ya kutumia mbinu mbadala za udanganyifu kama hiyo NIDA. Na nusu halali ni mchanganyiko wa vyote hivyo viwili.

Twende kwenye uchaguzi, lakini aliyoyasema Pole2 iwe sehemu kubwa ya mjadala/maridhiano 2026 - 2029. Ili uchaguzi wa 2030 uwe umecover dosari zote za uchaguzi wa 2025. Katiba mpya ndio uwe msingi mkuu wa maridhiano katika mazungumzo ya 2026-2029.
Hii movie nzuri sana kuifuatilia
 
Mpaka Muda huu :
  • Mshindi keshajulikana
  • Jumla ya kura na asilimia za kishindo za mshindi na za hao wasindikizaji wake zishajulikana, na zimeshaandikwa zinasubiri tu muda ziwekwe hadharani...
Yanayoendela ni Maigizo...
 
Back
Top Bottom