Hoja ya msingi ni mgongano wa kimaslahi. NIDA ni moja tu ya mbinu kadhaa zilizopo

Siku hizi matokeo yanajazwa tu kwa ubabe kwa msaada wa polisi bila hata kuhesabu kura.
Mtu mpumbavu pekee ndiye anaweza kupoteza muda wake kushiriki uchaguzi wa namna hii
Sijwahi kupiga kura na sitakaa nipige kura
 
Ni kweli unavyosema. Unaposema alichosema Polepole ni blah blah huo ni uongo? Kabla ya kauli ya jana ya Polepole wewe ulikuwa unajua mifumo ya NIDA, INEC, CCM ilivyounganishwa ili ku favor CCM?

Polepole katusaidia pakubwa sana. Hayo ya kuwepo kwa mabadiriko ya Katiba na Tume huru ya Uchaguzi yamepigiwa kelele miaka nenda rudi.

Alichokisema Polepole ni ili watu wapime wao wenyewe kama wakapige kura au la japo yeye kashauri wasiende. Maana kiuhalisia hakuna Uchaguzi ni kiini macho
 
Muhimu ni hilo mfumo wa ccm umeunganishwa moja kwa moja na time ya uchaguzi. Hili ndilo kubwa.

Ccm kuunganishwa na nida mi kwa ajili ya kupata data tu.
Ndiyomaana Polepole jana akasemaaa , ni utaratibu mzuri kama utakuwa kwenye mikono salama ,lakini ukiwa umeshikwa na watu wenye mikono michafu hugeuka ni bomu zito maana nisawa na adui kumiliki weapon code yako .

Sinihivyo mkuu?
 
Mbaya zaidi ccm na usalama wa taifa ni kama kitu kimoja!
 
Cha msingi kukijua ni mgongano wa kimaslahi [conflict of interest].

Uwepo tu wa mgongano wa kimaslahi ni tatizo linalozaa hayo mashambulizi mengine.

Mimi, kwa kujua kuwa kuna mgongano mkubwa wa kimaslahi, nilitambua kuwa CCM wana nafasi kubwa sana ya kufanya figisu za kila aina, ikiwemo kuwa na access ya databases kama hizo za NIDA na zinginezo.

Tatizo la msingi [underlying problem] ni mgongano wa kimaslahi uliopo.

Mwenyekiti wa CCM hapaswi kuunda uongozi wa tume ya uchaguzi.

That is common sense 101.
 
kwamba ndomana serikali chakavu ya ccm haitaki tume huru isije ikawa huria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…