Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Hoja ya Mhe. Nape (MB) Bungeni kuhusu kukaguliwa akaunti ya deni la taifa sina shida na hoja na anazo haki zote kwa mujibu wa Katiba, sheria na kanuni za Bunge, isipokuwa nachelea kuamini kwamba uzito wa hoja hii unaweza kutambuka wigo wa mhimili wa Bunge na kuleta shida kwenye mhimili wa serikali (japo Bunge linaisimamia serikali). Shida iko hivi:-
1. Uelewa wangu unanishawishi kwamba hoja inaweza kuwa kizungumkuti kwa VP.
2. Anayeshikilia nafasi ya VP kwa sasa ndiye alikuwa jikoni wakati wa awamu ya 5 hivyo kwenye awamu ya 6 yeye ni Institutional Memory wa yaliyotokea kwenye awamu ya 5 kwa awamu ya 6.
3. Je, kwenye uchunguzi huo wa akaunti hiyo ya deni la taifa kwa awamu ya 5 siyo kwamba utamuhitaji VP akae pembeni kupisha uchunguzi huru huo? Je, Tz tunao utamaduni huo?
4. Chama cha mtoa hoja kinawezakuwa salama kweli kama ukaguzi huo ukifanyika na kuthibitika kwamba utaratibu haukufuatwa. Ikumbukwe kwa chama cha mtoa hoja mchakato wa uchaguzi mkuu unaofuata huwa unaanza pale serikali inapomaliza kuundwa; ya uchaguzi mkuu unaokuwa umemalizika, kwa maana ya kwamba hata muda huu hoja inapotolewa tayari chama kiko kwenye maandalizi ya uchaguzi mkuu unaofuata.
5. Kama uchunguzi wa Bunge ukigundua madudu kwenye akaunti ya deni la taifa kwa wakati wa awamu ya 5 je, siyo kwamba hoja ya mtoa hoja inawaweka pabaya Ma-CAG wa awamu za 5 na 6?
6. Je, kama awamu ya 6 ikimaliza muda wake, nani anajuwa kama awamu ya 7 nayo itakuja na watoa hoja wa aina hii kwenye hoja hii ya akaunti ya deni la taifa? Taifa litakuwa linajenga utamaduni gani wa kutafutana mchawi kila awamu?
7. Je, mahusiano mazuri yaliyoko baina ya wakuu wa mihimili ya Bunge na Serikali yanawekwa rehani endapo taarifa ya ukaguzi/uchunguzi itathibitisha mashaka ya mtoa hoja?
NB.
Juzi nilisoma gazeti moja kwamba deni la taifa limefika Tzs.64 tr hoja ya mtoa hoja ilitaja Tzs.9 tr kama ndiko deni la taifa lilifika. Sasa kwa hesabu ndogo tu zisizo za kitaalam, kama awamu ya 5 ilifikisha deni la taifa Tzs.9 tr ina maana kwa mujibu wa gazeti hilo na hoja ya mtoa hoja kuna ongezeko la Tzs.55 tr za awamu ya 6 ambayo pia mtoa hoja ni kiongozi wa awamu hii kwa nafasi yake ya Ubunge kama alivyokuwa pia kwa awamu ya 5 anayotaka ichunguzwe. Aidha, kati ya Tzs.9 tr za awamu ya 5 na Tzs. 55 tr za awamu ya 6 (kufanya jumla ya Tzs.64 tr awamu gani imekopa zaidi? Japokuwa hoja ya mtoa hoja imejikita katika kutilia mashaka juu ya uwazi na matumizi ya awamu ya 5 kwenye akaunti hiyo ya deni la taifa na siyo nani kakopa zaidi).
Lakini pia hoja hiyo ya mtoa hoja inatambuka zaidi na kuwateta wataalam wa mipango kwasababu kama awamu ya 6 imekopa basi ni kwa ajili ya kumalizia miradi mikubwa ya maendeleo ya awamu ya 5 maana miradi mipya ya awamu ya 6 haijawa mingi kiasi cha kukopa Tzs.55 tr ndani ya miezi 7 wakati awamu ya 5 ilifikisha deni la taifa kwenye Tzs.9 tr kwa miaka mi-5. Sasa hapa wataalam wa mipango ndiyo wamekosea au kiongozi wa mhimili wa serikali ambayo mtoa hoja ndiyo alikuwa kinara wa kuiweka madarakani?
Nadhani tupime kina kabla hatujavua nguo kuvuka mto.