Hoja kuu sio kufukuzwa. CDM wanadai hawajawateua hao wabunge kupitia vikao vyao vya kikatiba. Hapo Mh Dugai mbona anapakwepa? Kufukuzwa likikuwa ni zao la kukiuka utaratibu za chama.
Chama chao kimesema hakijawateua kwa kuwa hakuna vikao vilivyokaa. Mbona hakikusikilizwa? Vikao vya rufaa ndio muhimu sasa?
Hata kama utaratibu wa kuwafukuza haukufuatwa, lakini hilo la kuteuliwa na vikao ama la ni factual issue. Kwa hivyo hoja kuu ni kuwa hawakuteuliwa na cdm kama sheria inavyotaka.....hiyo ya kutokuwa wanachama wa chama cha siasa ni nyongeza ambayo haina athari kwenye hoja kuu.
Pathetic!
Umesema jambo la msingi sana...
Na kwa kuongezea tu, mimi kwa ishu hii huwa najiuliza maswali kadhaa nashindwa kupata majibu kabisa na badala yake huishia kuamini tu kuwa, these are one of the dirty CCM political games kwa kutumia watu wenye mamlaka kama huyu Spika kwa manufaa ya CCM kuendelea kuishi na kutawala kwa kitambo kidogo..
#1. Spika anakuwa pale kwa ajili ya kutekeleza na kulinda katiba ya nchi au ya vyama vya siasa?
#2. Wenye wajibu wa kujitetea na kuthibitisha uhalali wa uanchama wa chama cha siasa fulani ni nani? Ni mtu wa tatu (kwa scenario hii ni Spika Ndugai) au mwanachama mwenyewe mwenye mgogoro na chama chake?
#3. Ni chombo gani kisheria chenye kutoa haki kwa watu kwa mujibu wa sheria na katiba ya JMT? Obviously, ni mahakama... au siyo? Je, mbona hapa Spika anaonekana kama anafanya kazi ya "UWAKILI WA KISHERIA" kwa kina mama hawa 19 nje ya utaratibu wa kimahakama?
#4. Je, ni kwanini hawa kina mama 19 kama wanadhani hawatendewi haki na chama chao kwa hiki kinachoitwa "natural justice" wakaenda mahakamani kuishtaki CHADEMA kwa kutotenda haki ili waendelee kuulinda ubunge wao kwa muda fulani? Na kwa ninavyofahamu Mimi, wanaweza kufungua shauri pia mahakamani kuiomba iamuru CHADEMA kusikiliza rufaa yao iwapo tu wanaamini chama kinafanya infringement ya haki zao za kikatiba..
#5. Mwisho kabisa mtu anaweza kujiuliza, kwamba, ina maana Spika Ndugai hajui kabisa kuwa haki za kisheria za watu wakiwemo wabunge hushughulikiwa na mahakama kwa utaratibu huu?
Spika Ndugai nadhani ina matatizo ya akili, siyo bure..
Anachotaka CHADEMA wafanye, anajua kabisa hawatafanya ujinga wake...
Na kwa lugha rahisi kabisa, ni kuwa, Spika anataka kufunika udhaifu na makosa yake kwa kuendelea kufanya mlolongo wa makosa mengine ya kisheria na kikatiba...
Akumbuke jambo moja, kuwa, ALWAYS KARMA IS A BITCH, na haina msamaha kwa watu dizaini ya Ndugai mwenye cheo cha U - Spika kwa leo...
Sijui ni kwanini wanasiasa wakatili na wasiotenda haki hawajifunzi kwa Hayati John Pombe Magifuli....!!