Hoja ya Spika Ndugai: Nitawafukuzaje wabunge ambao Rufaa zao hazijasikilizwa na Baraza kuu kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA?

Hoja ya Spika Ndugai: Nitawafukuzaje wabunge ambao Rufaa zao hazijasikilizwa na Baraza kuu kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA?

Sasa wakiteua hao 19 si ndicho CCM wanakihitaji ili kujustify uchaguzi usio free and fair?
Kwa hiyo wewe unataka wasiteue ili kujustify uchaguzi haukuwa fair? Aidah anafanya nini Bungeni? BAWACHA wanataka kwenda Mahakamani kudai nini sasa?

Haya mambo bana tuwaachie Politicians tu kwa kweli.
 
Spika wa bunge mh Job Ndugai hana tatizo na wabunge wa viti maalumu wa Chadema akina Halima Mdee na wenzake bali anachotaka ni utaratibu wa natural justice kufuatwa....
Mhe. Ndugai kaamua kutukanisha (abuse) malaka yake kama Spika, na elimu yake pia. Hoja sa CDM ni kwamba, majina yote 19 ya wabunge hayakuwasilishwa kwake na Katibu wa CDM, kwa maana chama hakikukaa popote kuwateua watu wale. Baada ya kungua kuwa wamejiteua, CDM iliandika barua kwenda kwa spika kuwakana na kutoa notisi ya kuwafutia uanachama.

Mbona Ndugai alipopewa majina ya wabunge wa CUF ali act mara moja bila kuomba maelezo? Mbona alipofukuzwa Sofia Simba ali act mara moja bila kupepesa macho wala kuhitaji documents zaidi.

Ana maslahi gani na wabunge hawa? Nusrat Hanje wa Geita, alitolewaje jela USIKU na kwenda kuapisha Dodoma asubuhi? Kesi yake ilisikilizwa? Katika mahakama gani?

AKiweza kujibu hoja hizo, atakua ameponya taifa.

Nawasilisha
 
Kwahiyo ukifungwa jela, halafu ukakata rufaa mahakamani kuhusu hukumu yako.

Kabla rufaa yako haijasikilizwa, hukumu yako inafutwa na unakuwa free?
nilimsikia wakili mmoja akisema kwenye jambo hili mfano huu si relevant, mfano relevant ni ikiwa wewe ni mfanyakazi na ukafukuzwa kazi basi ukikata rufaa utaendelea kuwa mfanyakazi mpaka pale rufaa yako itakaposikilizwa; the same case kwa kina mdee wamefukuzwa uanachama na wamekata rufaa wanaendelea kuwa wanachama mpaka pale rufaa zao zitakaposikizwa. Wakishinda watendelea kuwa wanachama wakishindwa uanachama wao utakua umeisha.
 
Sio tu wasiteue ili kujustify uchaguzi haukuwa huru na wa haki bali huu ni msingi mzuri na mzito wa kuleta hoja za tume huru ya uchaguzi na katiba mpya ambayo ndiyo kiini cha utatuzi wa changamoto za kimfumo na kiutawala za taifa hili ambazo zimekuwa hoja za upinzani kwa muda mrefu Chadema in particular.

Aida, kwa mujibu wa tume alishinda uchaguzi na amefata taratibu zote kuwa mbunge. Chadema walieleza wazi kuwa hawawezi kumzuia akitaka kuapa, na ukitazama vizuri utagundua aliachwa kimtego ashinde ili kuleta mgongano wa kusimamia maslahi yake, wananchi wake na chama chake. Hapa ameamua kusimamia maslahi yake.
Kwa hiyo wewe unataka wasiteue ili kujustify uchaguzi haukuwa fair? Aidah anafanya nini Bungeni? BAWACHA wanataka kwenda Mahakamani kudai nini sasa?
Ukiyatazama juu juu utaona ni kama ni ya wanasiasa pekee ila ukweli ni kwamba siasa ndiyo mfumo wa kuamua maisha yetu yaendeje.

Leo watumishi wanalia, wakulima hoi, wafanyabiashara, wanafunzi nk wote vilio kwa maamuzi yaliyotokana na mtu mmoja tu 'mwanasiasa'. Maisha yetu ya kila siku ni siasa, tukisema tuwaachie ni kama kumziria bucha fisi....ye hana hasara.
Haya mambo bana tuwaachie Politicians tu kwa kweli.
 
Jukumu lake spika kama amepokea barua halali ya wao kufukuzwa anatakiwa atii, hiyo kupekuwa pekuwa si kazi yake kina halima kama kitu hakikufuatwa ndo walitakiwa kwenda Mahakamani lakini sipika afanye kila kitu yeye
 
Kwahiyo ukifungwa jela, halafu ukakata rufaa mahakamani kuhusu hukumu yako.

Kabla rufaa yako haijasikilizwa, hukumu yako inafutwa na unakuwa free?
Mfano wa kijinga- itisheni baraza kesi iishe mnaogopa nini?
 
Wewe mbuzi, mimi siyo CHADEMA. Nashangaa tu hata hayo majina bungeni yalifikaje.
Ungekuwa siyo mbuzi ungejua kuwa majina kwenda kwa Spika yanatoka Tume ya Uchaguzi- sasa Spika anahusika nini? Tumieni basi akili kidogo
 
Jukumu lake spika kama amepokea barua halali ya wao kufukuzwa anatakiwa atii, hiyo kupekuwa pekuwa si kazi yake kina halima kama kitu hakikufuatwa ndo walitakiwa kwenda Mahakamani lakini sipika afanye kila kitu yeye
Mkuu wamekata rufaa tayari kuonyesha CHADEMA wanasukumwa na hasira za haya majamaa kukosa ubunge
 

Attachments

Ingekuwa wabunge wanalipwa mishahara na vyama vyao,sijui kama hao covid wangepeleka makalio yao bungeni. Lakini kwa vile wanalipwa mishahara na kodi zetu,Ndugai hana uchungu na hilo. Nadhani hao covid wakilipwa kuna mgao wanampa huyo mgogo
 
nilimsikia wakili mmoja akisema kwenye jambo hili mfano huu si relevant, mfano relevant ni ikiwa wewe ni mfanyakazi na ukafukuzwa kazi basi ukikata rufaa utaendelea kuwa mfanyakazi mpaka pale rufaa yako itakaposikilizwa; the same case kwa kina mdee wamefukuzwa uanachama na wamekata rufaa wanaendelea kuwa wanachama mpaka pale rufaa zao zitakaposikizwa. Wakishinda watendelea kuwa wanachama wakishindwa uanachama wao utakua umeisha.
Me si mtaalam wa sheria ila nahisi kama kuna jambo tunajichanganya. Nadhani si tu kwamba kitendo cha we kukata rufaa kinakurejeshea haki.

Ninavyo elewa mimi (niko tayari kusahihishwa) ni kuwa hadi rufaa yako ikubaliwe kusikilizwa baada ya kuonekana kuna hoja za msingi kisheria zinazoweza kutengua hukumu/maamuzi ya awali. Nadhani na Mkaruka pia ndiyo hoja yake hii.

Kwa hii hata kama mtu alisha hukumiwa nadhani kuna kitu wanaita 'Bail Pending Appeal' ambapo mshitakiwa anaweza pewa dhamana wakati rufaa yake inasikilizwa baada ya hukumu ya awali kumtia jela.

Sasa hawa covid-19 nadhani hoja yao ni kuwa hawakupewa haki ya kusikilizwa na CC ya chama kitu ambacho si kweli, waliitwa na hawakutokea.

Na pia katiba ya chama inaruhusu kufanya maamuzi kwa jambo la dharura, na issue ya covid-19 ilikuwa na dharura ndani yake i.e kuzuia wasiapishwe kuwa wabunge baada ya ile 'forgery'.
 
Nadhani shida ipo sasa. Nani anapaswa kuinitiate hii kitu? Madai kwamba ile barua ni forged nadhani yalitolewa kwenye media. Kuna msemo unasema hivi "He who alleges must also prove". Wapi, how, when labda ndipo kwenye shida


Sasa hii ndio tendency yenyewe ya kuplay victim. Kushindwa kuchukua hatua stahiki kwa sababu tu unahisi/unaogopa/umeshaconclude kuwa hutotendewa haki ni udhaifu.

Prove what? Wao walichosema ni kuwa hawajapeleka fomu au barua yeyote NEC ya kuwateua wakina Halima. Aliyetakiwa ku initiate hiyo investigation ni NEC na Spika kama watu ambao wamedanganywa. Wao ndio wana makabrasha yaliyowasilishwa kwao na sio Chadema. Hivi mtu una biashara halafu mtu akaja akawalipia cash bidhaa lakini ulipozipeleka benki wakakuambia zile pesa sio zao, ni forgery, utawashika benki na kuwataka wamtafute mtu aliyewasilisha pesa bandia?

Au ni utaenda polisi na zile pesa bandia na kuwataka wamtafute na kumchukulia hatua aliyekulipa kwa pesa bandia. Ndio maana tunasema jukumu ni la NEC na Spika kutafuta ukweli kuhusu uhalali wa barua na makabrasha ya utambulisho waliyopokea kutoka kwa wakina Halima. Chadema wamesema hawajawasilisha kitu NEC na NEC wakathibitisha hivyo hadharani. Sasa unataka Chadema wafanye nini wakati hawajui hata kama kuna barua yeyote iliyowasilishwa?

Kuna msemo kuwa ni dalili za uchizi kurudia kufanya kitu kile kile na kutegemea matokeo tofauti. Chadema sio wageni wa Mahakama na wanajua jinsi wanavyotendewa na Mahakama. Sasa kama wanaamini kuwa hawajawahi kutendewa haki kwa wakati muafaka nini kitawafanya waamini kuwa haki itatendeka safari hii? Unasahau kuna mbunge wao alifungwa na ni baada ya yeye kumaliza kifungo chake ndio Mahakama ikasema kuwa haki haikufanyika?

Au watu wao wangapi wako mahabusu kwa makosa ya ajabu ambayo mara nyingi baada ya wao kusota ndani yanatupiliwa mbali? Vile vile kwenye hili Mahakama inaweza kusikiliza kesi kwa miaka minne na mwisho wa siku hata wakisema kuwa walikuwa na haki itakuwa too late. Aidha, Spika ameisha sema kuwa hamna mahali anapolazimishwa kuwafukuza mapema kama hata wataonekana kuwa hawastahili kuwemo Bungeni!

Kwa huu msimamo wao, mchezo unabaki kwa NEC na Spika. Wao ndio wenye majibu.

Amandla...
 
Me si mtaalam wa sheria ila nahisi kama kuna jambo tunajichanganya. Nadhani si tu kwamba kitendo cha we kukata rufaa kinakurejeshea haki....
Dharula ipi mkuu?
 
Dharula ipi mkuu?
Walipoitwa kujitetea walisema (kila mmoja) kuwa wana udhuru na kuomba wapewe muda wa kusikilizwa siku za mbele ambapo muda huo ingekuwa wamesha apa ubunge kitu ambacho ndicho chama chao kilikuwa kinazuia kisitendeke kutokana na wao kutoteuliwa na chama.
 
Back
Top Bottom