PreGE2025 Hoja za Askofu Gwajima ni mbili tu, wanaotaka kumjibu zingatieni hayo kwanza ili tuwaelewe

PreGE2025 Hoja za Askofu Gwajima ni mbili tu, wanaotaka kumjibu zingatieni hayo kwanza ili tuwaelewe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
12,151
Reaction score
44,120
Askofu Gwajima kwa ujasiri mkubwa kabisa amekuja hadharani na kupasua jipu kwa watanzania kuhusu kitendawili cha matukio ya utekaji hapa Tanzania. Gwajima amejenga hoja katika mambo mawili.

1. Kwanini kuna muendelezo wa matukio ya utekaji hapa Tanzania licha ya kuwepo vyombo vya dola vyenye uwezo na mifumo imara na dhabiti ya kuchunguza, kugundua, kuzuia na kufuta kabisa hayo matukio.

Pia soma Pre GE2025 - Askofu Gwajima: Wakuu wa Vyombo vya Usalama wasiondolewe kwenye nafasi zao kwa mapenzi ya mwanasiasa aliyewaweka

2. Kwanini mamlaka zote za nchi zimeshindwa kabisa kuwajibika katika matukio yote ya kutekwa, kuteswa na kupotezwa kwa watu.

Sasa, mtu yoyote, taasisi yote, mamlaka zozote zenye lengo la kutaka kumjibu Gwajima ni vyema zikazingatia hayo mambo makubwa mawili ili tuweze kuwaelewa.
 
mdude.jpg

Rest in peace Mdude.
 
Askofu Gwajima kwa ujasiri mkubwa kabisa amekuja hadharani na kupasua jipu kwa watanzania kuhusu kitendawili cha matukio ya utekaji hapa Tanzania. Gwajima amejenga hoja katika mambo mawili.
1. Kwanini kuna muendelezo wa matukio ya utekaji hapa Tanzania licha ya kuwepo vyombo vya dola vyenye uwezo na mifumo imara na dhabiti ya kuchunguza, kugundua, kuzuia na kufuta kabisa hayo matukio.

2. Kwanini mamlaka zote za nchi zimeshindwa kabisa kuwajibika katika matukio yote ya kutekwa, kuteswa na kupotezwa kwa watu.

Sasa, mtu yoyote, taasisi yote, mamlaka zozote zenye lengo la kutaka kumjibu Gwajima ni vyema zikazingatia hayo mambo makubwa mawili ili tuweze kuwaelewa.
Gwajima kwa hili ameonyesha uzalendo wa kweli kwa nchi yetu...Tanzania kwanza, vingine vitafuata
 
Hakuna mareefu yasiyokuwa na ncha.

Wamwulize, IGP Omary Mahita mda huu yukoje.
Maisha yanaenda na mda,japo mda uko palepale.

Nguvu,majigambo,majivuno,cheo,sauti ya mamlaka,amri n.k
Viko wapi.

Gwajima katembea na biti zote za Chadema.
Japo,hajazungumzia kuhusu Kukamatwa na kubandikwa kwa kesi ya uongo kwa M/kiti taifa wa Chadema.

Ameonyesha unafiki pia.
 
Gwajima amejenga hoja katika mambo mawili.
Ukitumia akili na fikra tunduizi, hapo hoja kuu ni moja ambayo ni Rais kupewa madaraka makubwa na yasiyo hojiwa kupitia katiba mbovu tuliyokuwa nayo.

Nyerere alionya mapema kwa katiba ya sasa angeamua kuwa dikteta basi watu wangekoma.

Ila alisema Tanzania inapata marais wenye hekima na busara, akaongezea kuwa ipo siku atatokea rais chizi kwa katiba hii basi raia watakoma na watajuta!
 
Back
Top Bottom