PreGE2025 Hoja za Askofu Gwajima ni mbili tu, wanaotaka kumjibu zingatieni hayo kwanza ili tuwaelewe

PreGE2025 Hoja za Askofu Gwajima ni mbili tu, wanaotaka kumjibu zingatieni hayo kwanza ili tuwaelewe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Askofu Gwajima kwa ujasiri mkubwa kabisa amekuja hadharani na kupasua jipu kwa watanzania kuhusu kitendawili cha matukio ya utekaji hapa Tanzania. Gwajima amejenga hoja katika mambo mawili.
1. Kwanini kuna muendelezo wa matukio ya utekaji hapa Tanzania licha ya kuwepo vyombo vya dola vyenye uwezo na mifumo imara na dhabiti ya kuchunguza, kugundua, kuzuia na kufuta kabisa hayo matukio.

2. Kwanini mamlaka zote za nchi zimeshindwa kabisa kuwajibika katika matukio yote ya kutekwa, kuteswa na kupotezwa kwa watu.

Sasa, mtu yoyote, taasisi yote, mamlaka zozote zenye lengo la kutaka kumjibu Gwajima ni vyema zikazingatia hayo mambo makubwa mawili ili tuweze kuwaelewa.
sindano za gwajima hakuna wa kumjibu.ni kubweka tu
 
Sio lazima ajibiwe kwa kufuata mwongozo wako. Kila mmoja ana style yake ya kumjibu
mfano?
toa mfano; haya sio mzaha mzaha, ndio mana Gwaj alitanguliza Tanzania kwanza, hoja zijibiwe kwa masrai ya Taifa sio kumrenga mtu
 
Hatutofautiani sana, mi naona kulikwepa suala la Tal alilinda maana ya hoja yake.

Embu tusaidiane angelichomekeaje hapo?
Kwamba kabambikiwa kesi, si mpaka angelikuwa na approval?

Embu nipanue mawazo kidogo.
Ni kweli,ila kwa vile alikuwa amejitambulisha kama mtanzania na mwananchi wa kawaida na sio Mbunge wa ccm,wala Askofu,pia mneki.

Basi angeelezea pia,swala la wananchi kubambikiwa kesi na mamlaka.
Kwa mtu ambaye ni Pablic figure,na mtu mnyoofu kuweza kupewa kesi kama ile ni aibu.

Hoja zake,sawa tumezipokea.
Ila bado kwa wabobevu wa mambo bado tunaona unafiki bado.
Japo,amejitahidi kutembea na biti ya hoja za Wapinzani.
Maana,hoja kubwa za wapinzani ni mabadiriko katika sheria na kanuni katika Katiba yetu ambayo haiendani na matakwa ya sasa.

Hivyo,kukwepa kugusia swala kama hilo,ndo linapelekea bado kuonekana hayuko siliasi kwa 100%.
 
mfano?
toa mfano; haya sio mzaha mzaha, ndio mana Gwaj alitanguliza Tanzania kwanza, hoja zijibiwe kwa masrai ya Taifa sio kumrenga mtu
Rudi kwanza shule kajifunze kiswahili ikiwa we kweli ni Mtanzania.
Sio masrai ni maslahi
Sio kumrenga ni kumlenga
 
Back
Top Bottom