Benny Haraba
JF-Expert Member
- Dec 7, 2012
- 15,670
- 14,647
Kwasasa kulawiti na kubakaAskofu Gwajima kwa ujasiri mkubwa kabisa amekuja hadharani na kupasua jipu kwa watanzania kuhusu kitendawili cha matukio ya utekaji hapa Tanzania. Gwajima amejenga hoja katika mambo mawili.
1. Kwanini kuna muendelezo wa matukio ya utekaji hapa Tanzania licha ya kuwepo vyombo vya dola vyenye uwezo na mifumo imara na dhabiti ya kuchunguza, kugundua, kuzuia na kufuta kabisa hayo matukio.
2. Kwanini mamlaka zote za nchi zimeshindwa kabisa kuwajibika katika matukio yote ya kutekwa, kuteswa na kupotezwa kwa watu.
Sasa, mtu yoyote, taasisi yote, mamlaka zozote zenye lengo la kutaka kumjibu Gwajima ni vyema zikazingatia hayo mambo makubwa mawili ili tuweze kuwaelewa.
Kama hawatajibu hayo maswali 2 ya msingi basi watakuwa nao ni washikiriki wakuu, (steering)