#COVID19 Hoja za Askofu Gwajima zimewaumbua wataalam wetu na waliomuingiza 'mkenge' Rais Samia kwenye chanjo ya Corona

#COVID19 Hoja za Askofu Gwajima zimewaumbua wataalam wetu na waliomuingiza 'mkenge' Rais Samia kwenye chanjo ya Corona

Upumbavu ndio huu, ujinga huna ninaamini. Hapa nasema wewe sio ignorant, ni fool! Maawali yote aliyouliza Dr. Gwajima na unayoshadidia yanajibiwa na jibu moja tu - hakuna popote, narudia popote ambapo mtaalamu yeyote au mtengeneza chanjo amesema kuwa hizi ni chanjo za KUZUIA corona au KUZUIA maambukizi! Kila mtaalamu (asiye kanjanja) kasema chanjo hizo zinazuia severe sickness (hospitalization) na vifo!! Na tunachojitaji kwa muda huu ni kutoumwa na kutokufa!! Basi!!

Swali ambalo mnashindwa kujibu sasa hivi ni kuna watu wangapi wamechanjwa lakini wakaugua na kufa!! Mpaka sasa wanaukufa 100% ni ambao hawajachanjwa na watu wawili katika kila 100 waliochanjwa ndio wanapata mild symptoms (maana yake 98 hata kusikia kichwa kinauma hawasikii).

Kuweni wakweli na kama mna scientific data mzitoe. Mambo haya ni ya kisayansi - sio ya kiroho wala kisiasa. Ingekuwa ya kiroho badala ya Gwajima kurusha maswali - ANGEPONYA!!

Upumbavu umewajaa mpaka unaelekea kuchua nafasi ya ujinga kiasi mtakuwa hamfundishiki!!
Povu la nini sasa mkuu? Sijaona hoja uliyojibu.
Acha porojo.
 
Wasukuma nimewachukia sababu ya jiwe ila gwajiboy ana hoja nzuri, inabidi asikilizwe tu hata kama Yupo kwenye kundi la sukuma gang
 
Nilitegemea wataalam wetu wa afya pamoja na washauri wa Rais waliomshauri kuagiza chanjo ya corona watakuwa mstari wa mbele kujibu hoja za askofu badala yake wamekuwa watu wa kumshambulia yeye binafsi na kumpa vitisho badala ya kujibu hoza zake kitaalam.

Katika hoja ya kwanza, Askofu gwajima ana hoji: Endapo mtu akichanjwa bado ataendelea kuambukiza na kuambukizwa virusi vya corona na kama ndivyo, kuna maana gani ya kuchanja?

Hoja ya pili Askofu anahoji endapo mtu amechanjwa bado atatakiwa kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuvaa barakoa ili kujikinga na maambukizi. Askofu anataka kujua, kama kweli chanjo ya corona ni kinga kwanini mtu aliyechanjwa anatakiwa tena kuvaa barakoa?

Askofu anaendelea kuhoji, mataifa makubwa kama vile marekani yote yana chanjo zao. Kwa mfano, marekani wana chanjo ya jonhson&jonhson na moderna, china wana sinovac, uiongereza wana Astrazeneca, germany wana Pfizer, urusi wana ya kwao, Cuba pia wana ya kwao na mataifa mengine yana chanjo zao. Je ni kwanini haya mataifa yenyewe kwa yenyewe yanaogopana kutumia chanjo ya mwingine?

Gwajima ana hoji kwamba katika kipindi cha zaidi ya miezi sita iliyopita wataalam wetu wanaotaka tupambane na corona kwa njia ya chanjo ndio hawa hawa walisema tusiziamini chanjo kwamba zinaweza kuwa na madhara na kwamba tutumie njia za asili ikiwemo kujifukiza wakajenga hadi banda la kujifukizia pale muhimbili wengine wakafanya mahojiano TBC kuonyesha wasi wasi wao juu ya chanjo ya corona, kwanini leo wamebadilika?

Swali la nyongeza: kwenye fomu ya chanjo ya corona kuna kipengele kinasema serikali haitahusika kwa namna yoyote ile endapo mtu aliyechanjwa atapata maudhi ambayo kwa sasa hayafahamiki. Tunataka wataalam wetu watwambie kama hii chanjo wameifanyia utafiti wa kutosha kwanini wanasema tena kwamba mtu aliyechanjwa anaweza kupata maudhi ambayo hayafahamiki?

Napenda sana wataalam wajibu hoja za gwajima kwa sababu vile wanavyomshambulia badala ya kujibu hoja zake ni kudhihirisha kwamba hawana utaalam wa walichosomea kitu ambacho ni hatari kwa uhai na afya za watanzania.

Kuna watu Tanzania ukiwaambia usiku kuna giza watakuambia usiku kuna mwanga. Huwezi kushindana na watu ambao watajaribu kutafuta kila njia ya kupinga kila kitu ili wapate sifa tu . Rais hawezi kupeza muda na watu kama hawa
 
Katika kujiuliza kwenu mnafikiri ile Chanjo ni kwa ajili ya Nini?
Si ndo uwaulize wao walioileta kama wao wanashindwa kusema ni kwanini bado tunavaa barakoa wakati tayari tumeshachanjwa. Shida nyie watu kusoma mpaka form4 mnajiona ni wasomi sana wakina gwajima mnawaona ni wapumbavu na wajinga lakini maswali yao mnashindwa kuyajibu.
 
Hivi hao wenye ukwasi mkubwa wanaoondoka si watakuwa wamechanja, unataka kusema Dr masawee au keenja hawakuchanja,

Tuambieni ukweli kama ndo operesheni maliza wazee tujue.

Ila mimi sidungi hata kwa hela sitski
 
Nilitegemea wataalam wetu wa afya pamoja na washauri wa Rais waliomshauri kuagiza chanjo ya corona watakuwa mstari wa mbele kujibu hoja za askofu badala yake wamekuwa watu wa kumshambulia yeye binafsi na kumpa vitisho badala ya kujibu hoza zake kitaalam.

Katika hoja ya kwanza, Askofu gwajima ana hoji: Endapo mtu akichanjwa bado ataendelea kuambukiza na kuambukizwa virusi vya corona na kama ndivyo, kuna maana gani ya kuchanja?

Hoja ya pili Askofu anahoji endapo mtu amechanjwa bado atatakiwa kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuvaa barakoa ili kujikinga na maambukizi. Askofu anataka kujua, kama kweli chanjo ya corona ni kinga kwanini mtu aliyechanjwa anatakiwa tena kuvaa barakoa?

Askofu anaendelea kuhoji, mataifa makubwa kama vile marekani yote yana chanjo zao. Kwa mfano, marekani wana chanjo ya jonhson&jonhson na moderna, china wana sinovac, uiongereza wana Astrazeneca, germany wana Pfizer, urusi wana ya kwao, Cuba pia wana ya kwao na mataifa mengine yana chanjo zao. Je ni kwanini haya mataifa yenyewe kwa yenyewe yanaogopana kutumia chanjo ya mwingine?

Gwajima ana hoji kwamba katika kipindi cha zaidi ya miezi sita iliyopita wataalam wetu wanaotaka tupambane na corona kwa njia ya chanjo ndio hawa hawa walisema tusiziamini chanjo kwamba zinaweza kuwa na madhara na kwamba tutumie njia za asili ikiwemo kujifukiza wakajenga hadi banda la kujifukizia pale muhimbili wengine wakafanya mahojiano TBC kuonyesha wasi wasi wao juu ya chanjo ya corona, kwanini leo wamebadilika?

Swali la nyongeza: kwenye fomu ya chanjo ya corona kuna kipengele kinasema serikali haitahusika kwa namna yoyote ile endapo mtu aliyechanjwa atapata maudhi ambayo kwa sasa hayafahamiki. Tunataka wataalam wetu watwambie kama hii chanjo wameifanyia utafiti wa kutosha kwanini wanasema tena kwamba mtu aliyechanjwa anaweza kupata maudhi ambayo hayafahamiki?

Napenda sana wataalam wajibu hoja za gwajima kwa sababu vile wanavyomshambulia badala ya kujibu hoja zake ni kudhihirisha kwamba hawana utaalam wa walichosomea kitu ambacho ni hatari kwa uhai na afya za watanzania.
Haya mimi nitajaribu kujibu hoja zake zinazohusu sayansi tuu siyo siasa.

1) Chanjo zinafundisha mwili kupambana na virusi vya corona kwa hiyo hata ukiambukizwa baada ya kuchanjwa, mwili wako unajua jinsi gani ya kuvishambulia virusi vya corona. Waliochanjwa wakiambukizwa corona wengi hawaugui sana kwa sababu miili yao tayari inajua jinsi ya kupambana na virusi vya corona vikiingia mwilini.

2) Waliochanjwa kuvaa barakoa ni kuwalinda wale ambao hawajachanjwa. Mfano mtu aliyechanjwa anaambukizwa corona lakini haumwi, yupo fiti lakini bado anakuwa ni mbebaji wa virusi vya corona, carrier. Huyu carrier wa virusi vya corona anaweza kuwaambukiza watu na kama akiwaambukiza watu ambao hawajachanjwa anaweza kuwaletea matatizo au kuwauwa haswa wenye matatizo ya kiafya au wenye umri mkubwa.

3) Mataifa tofauti kutengeneza chanjo inasaidia kupunguza gharama za chanjo na inarahisisha kuzisambaza. Mfano chanjo za Pfizer na Moderna zina gharama sana kusafirishwa kwa sababu zinahitaji kuwekwa kwenye mafriji au zinaharibika. Sasa zikitengenezwa karibu na zinapotumika, zinapunguza gharama na inarahisisha kuzisambaza.

4) Kuhusu madhara ya hizo chanjo, kila dawa ina madhara. Hata dawa kama Aspirin au Paracetamol ambazo wengi tumeshazitumia zina madhara yake i.e. side effects. Cha kuuliza hapa ni jee, madhara ya chanjo ya corona ni makubwa kuliko madhara ya kuugua na corona? Wangapi wamekufa na ugonjwa wa corona vs wangapi wamekufa na chanjo ya corona? Wangapi wamelazwa hospitali na ugonjwa wa corona vs wangapi wamelazwa hospitali na chanjo ya corona? Ukishapata haya majibu ndiyo fanya uamuzi ni lipi bora, kuugua corona au kuchanjwa corona.
 
Kachome chanjo Mkuu wangu usiwasikilize wazushi.
Siwezi kujipeleka kichwa kichwa kufanyiwa majaribio mkuu. Anzeni kuchanja nyinyi kwanza ili siku mkigeuka mazombi tuwatibu mana tukichanja wote kwa wakati mmoja tukigeuka mazombi hakutakuwa na wa kumtibu mwenzake
 
Hakuna wa kuweza kumjibu Gwajima , sababu hzo chanjo ni agenda ya Siri ambayo gwajima yeye mwenyewe anaijua na Raisi anaijua...!! Sema Raisi kabanwa na wala sio maamuz yake hayo ....!!Hana namna , na sote tutachanjwa, itategemea na pressing speed ya wababe wa dunia, so ni Suala la mda tuu..

Dah, siri ya watu wawili tu? Nchi la milioni 60? Wana kipaji gani?
 
Back
Top Bottom