#COVID19 Hoja za Askofu Gwajima zimewaumbua wataalam wetu na waliomuingiza 'mkenge' Rais Samia kwenye chanjo ya Corona

Povu la nini sasa mkuu? Sijaona hoja uliyojibu.
Acha porojo.
 
Wasukuma nimewachukia sababu ya jiwe ila gwajiboy ana hoja nzuri, inabidi asikilizwe tu hata kama Yupo kwenye kundi la sukuma gang
 


Kuna watu Tanzania ukiwaambia usiku kuna giza watakuambia usiku kuna mwanga. Huwezi kushindana na watu ambao watajaribu kutafuta kila njia ya kupinga kila kitu ili wapate sifa tu . Rais hawezi kupeza muda na watu kama hawa
 
Katika kujiuliza kwenu mnafikiri ile Chanjo ni kwa ajili ya Nini?
Si ndo uwaulize wao walioileta kama wao wanashindwa kusema ni kwanini bado tunavaa barakoa wakati tayari tumeshachanjwa. Shida nyie watu kusoma mpaka form4 mnajiona ni wasomi sana wakina gwajima mnawaona ni wapumbavu na wajinga lakini maswali yao mnashindwa kuyajibu.
 
Hivi hao wenye ukwasi mkubwa wanaoondoka si watakuwa wamechanja, unataka kusema Dr masawee au keenja hawakuchanja,

Tuambieni ukweli kama ndo operesheni maliza wazee tujue.

Ila mimi sidungi hata kwa hela sitski
 
Haya mimi nitajaribu kujibu hoja zake zinazohusu sayansi tuu siyo siasa.

1) Chanjo zinafundisha mwili kupambana na virusi vya corona kwa hiyo hata ukiambukizwa baada ya kuchanjwa, mwili wako unajua jinsi gani ya kuvishambulia virusi vya corona. Waliochanjwa wakiambukizwa corona wengi hawaugui sana kwa sababu miili yao tayari inajua jinsi ya kupambana na virusi vya corona vikiingia mwilini.

2) Waliochanjwa kuvaa barakoa ni kuwalinda wale ambao hawajachanjwa. Mfano mtu aliyechanjwa anaambukizwa corona lakini haumwi, yupo fiti lakini bado anakuwa ni mbebaji wa virusi vya corona, carrier. Huyu carrier wa virusi vya corona anaweza kuwaambukiza watu na kama akiwaambukiza watu ambao hawajachanjwa anaweza kuwaletea matatizo au kuwauwa haswa wenye matatizo ya kiafya au wenye umri mkubwa.

3) Mataifa tofauti kutengeneza chanjo inasaidia kupunguza gharama za chanjo na inarahisisha kuzisambaza. Mfano chanjo za Pfizer na Moderna zina gharama sana kusafirishwa kwa sababu zinahitaji kuwekwa kwenye mafriji au zinaharibika. Sasa zikitengenezwa karibu na zinapotumika, zinapunguza gharama na inarahisisha kuzisambaza.

4) Kuhusu madhara ya hizo chanjo, kila dawa ina madhara. Hata dawa kama Aspirin au Paracetamol ambazo wengi tumeshazitumia zina madhara yake i.e. side effects. Cha kuuliza hapa ni jee, madhara ya chanjo ya corona ni makubwa kuliko madhara ya kuugua na corona? Wangapi wamekufa na ugonjwa wa corona vs wangapi wamekufa na chanjo ya corona? Wangapi wamelazwa hospitali na ugonjwa wa corona vs wangapi wamelazwa hospitali na chanjo ya corona? Ukishapata haya majibu ndiyo fanya uamuzi ni lipi bora, kuugua corona au kuchanjwa corona.
 
Kachome chanjo Mkuu wangu usiwasikilize wazushi.
Siwezi kujipeleka kichwa kichwa kufanyiwa majaribio mkuu. Anzeni kuchanja nyinyi kwanza ili siku mkigeuka mazombi tuwatibu mana tukichanja wote kwa wakati mmoja tukigeuka mazombi hakutakuwa na wa kumtibu mwenzake
 

Dah, siri ya watu wawili tu? Nchi la milioni 60? Wana kipaji gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…