Hoja za Matangazo kwenye jezi mpya Simba

Hoja za Matangazo kwenye jezi mpya Simba

Mo anatakiwa atujuze moja, je yeye ni mwekezaji anaegawana faida na simba??? au yeye ni mwekezaji aliewekeza simba iliatangaze biashara zake,

majibu yake yatatusaidia kudai mapato yatokanayo na matangazo yake au kuheshimu haki ya yeye kugeuza jezi ziwe kurasa ya mbele ya gazeti la champions.
 
Timu haiendeshwi na elfu 30 za kununua jezi, hayo matangazo kwenye jezi yanachangia kiasi kikubwa maendeleo ya timu.
Mo anailipa Simba kiasi gani ili kuweka Tangazo lake kwenye jezi ya Simba?

Okay, ngoja tubadili swali. Hivi Mo analipishwa pesa yoyote na Simba kwa kuweka tangazo lake kwenye jezi za Simba?
 
Sidhani kama kuna mtu mwenye akili timamu anayepinga uwepo wa matangazo kwenye jezi ila wengi wanaopinga wanapinga kwa hoja zifuatazo.

1. Mpangilio wa matangazo, matangazo kwenye jezi ya simba yamekaa hovyo hovyo sana, mengine mgongoni, mengine kwenye kola, mpaka yanapoteza mvuto wa jezi na sidhani kama walikosa muundo mzuri wa kuweka matangazo hayo kwa kuwa end product ni kama bango.

2. Mdhamini mmoja kujirudia mara nyingi, Kampuni moja inajirudia zaidi ya mara tano!! , Utajisikiaje ukivaa jezi ya arsenal halafu fly emrirates ipo mara 6!!

3. Mdhamini mkuu wa Simba anajulikana kuwa ni Sportpesa, kiasi anachokitoa kwaajili ya udhamini kinajulikana, huyu mdhamini mwingine anatoa shilingi ngapi ukilinganisha na idadi anayotokea kwenye jezi ya Simba.?

4. Wakati mwingine sio tu hela watu wanaangalia class, Simba imeshakuwa brand kubwa sana Tanzania, kuna vitu vidogo vidogo vinaweza kushusha hadhi ya kitu hata kama kuna hela inaingia, hivi club kubwa kama Manchester United inayomilikiwa na familia ya Glazer wanashindwa nini kutangaza jina na makampuni yao kwenye jezi, au Chelsea ya Roman Abramovich mbona hatuioni ikitangaza matangazo ya kampuni za mafuta za Roman Abramovich?

Jibu ni kwamba Roman Abramovich na Familia ya Glazer hawashindwi kujaza mitangazo kwenye hizo jezi, isitoshe wao ndio wamiliki kwa kiasi kikubwa, ila kinacholindwa ni hadhi ya hizo clubs ndio maana unawaona wadhamini kama Team Viewer wakijinafasi peke yao kama wadhamini wakuu na wadhamini wadogo wakionekana kwenye sehemu nyingine za jezi vizuri bila kuharibu haiba ya jezi

Itaendelea.
Mimi naona ile mo29 ya pale ndo imeharibu jezi( ingetolewa)

Ile vunja bei ingekaa upande wa kushoto pale ilipo mo xtra
Afu iyo mo xtra ingekaa pale kwenye mkono kama visit rwanda inavokaaaga

Ile mosport sasa ndo MO anapokuaga kama mjinga jezi za vunjabei ww MO upele unakuwashia nn

Simba fan hapa
 
U
Mo anatakiwa atujuze moja, je yeye ni mwekezaji anaegawana faida na simba??? au yeye ni mwekezaji aliewekeza simba iliatangaze biashara zake,

majibu yake yatatusaidia kudai mapato yatokanayo na matangazo yake au kuheshimu haki ya yeye kugeuza jezi ziwe kurasa ya mbele ya gazeti la champions.
Unachangia sh ngap kama mwanachma kuendesha team mkuu,iv kwel unaweza kupiga hesabu ya mwanaume mwenzio ambaye anakesha kuhakikisha team inafanya vizur
 
Mo anailipa Simba kiasi gani ili kuweka Tangazo lake kwenye jezi ya Simba?

Okay, ngoja tubadili swali. Hivi Mo analipishwa pesa yoyote na Simba kwa kuweka tangazo lake kwenye jezi za Simba?
Mo halipi,na asilipe chochote,aendelee tu kupiga hela,kikubwa sisi mashabiki wa Simba tunaona timu inafanya vizuri,tangia Mo awekeze Simba haijawai kuvurunda.
sisi kama shabiki wa Simba tunamuhitaji zaidi Mo pale Simba kuliko kitu chochote.
Mungu ibariki Rivers utd.
 
Mpaka sasa nna simba app(2000/-) na uhakika wa kwenda Simba day (5000/-)
Nikihoji matangazo nitakua mwehu.
Mo ongeza matangazo.
 
Hii MO 29 sehemu ilipo na rangi zake sijapenda maana ni sehemu yakuandikia jina, ina-confuse kidogo kwa mimi binfsi jezi ni nzuri eneo hilo ndio sijapenda na unaweza inunua na ukaiboresha kama hivi huyu jamaa. Naona tuinunue ni kali kinoma nahisi usipova huu uzi mwaka utakua umeumaliza vibaya sana

op.classic_241218865_125233683092882_9029022724435501167_n.jpg

unaweza inunua na
 
Mimi nashauri ikiwezekana kwenye jezi zetu za simba usawa wa tumbo jezi zetu inabidi tuweke Profile picture ya Mo
 
Mimi naona ile mo29 ya pale ndo imeharibu jezi( ingetolewa)

Ile vunja bei ingekaa upande wa kushoto pale ilipo mo xtra
Afu iyo mo xtra ingekaa pale kwenye mkono kama visit rwanda inavokaaaga

Ile mosport sasa ndo MO anapokuaga kama mjinga jezi za vunjabei ww MO upele unakuwashia nn

Simba fan hapa
Design ingekuwa hivi , jezi ingependeza.

Unaweza ukakuta moiw sports ni kampuni inayohusika na kutengengeza vifaa vya mchezo hapo ndipo utajua haujui
 
Hii MO 29 sehemu ilipo na rangi zake sijapenda maana ni sehemu yakuandikia jina, ina-confuse kidogo kwa mimi binfsi jezi ni nzuri eneo hilo ndio sijapenda na unaweza inunua na ukaiboresha kama hivi huyu jamaa. Naona tuinunue ni kali kinoma nahisi usipova huu uzi mwaka utakua umeumaliza vibaya sana

View attachment 1925873
unaweza inunua na
Wangeweka pembeni ya mikono
 
Back
Top Bottom